Jinsi ya kuswali swala vitani

Post hii itakufundisha taratibu zinazofanyika ilibkuswalibukiwa vitani.

Kusimamisha Swala Vitani

Muislamu haruhusiwi kuswali swala ya faradhi nje ya wakati wake hata akiwa katika vita vya kupigania Dini ya Allah(s.w). Bali Allah (s.w) ametuhafifishia swala, tukiwa vitani na kutuelekeza tuswali ifuatavyo:

 

“Na unapokuwa pamoja nao (Wa is lamu katika vita) ukawaswalisha, basi kundi moja miongoni mwao wasimame pamoja nawe (waswali) na washike silaha zao. Na watakapomaliza sijda zao basi na wende nyuma yenu (kulinda); na lile kundi jingine ambalo halijaswali lisw ali pamoja naw e, nao washike hadhari yao na silaha zao (humo ndani ya swala, maana) wale waliokufuru wanataka mghafilike na silaha zenu na vitu vyenu ili wakuvamieni mvamio wa mara moja. Wala si vibaya kwenu ikiwa mnaona udhia kwa sababu ya mvua au mnaona ugonjwa, kuondoa silaha zenu,.

 

Na mshike hadhari yenu. Hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia makafiri adhabu itakayowadhalilisha”. (4:102)
Namna ya kusimamisha swala katika uwanja wa vita kutokana na maelekezo ya aya hii ni kwamba, askari wagawanyike katika makundi mawili ambayo yataswalishwa na Imamu mmoja na swala itafupishwa kama ilivyo katika swala ya safari. Kundi moja litaanza kuswali na Imamu wakiwa na silaha zao na kundi lingine litabaki katika ulinzi. Imamu ataswali rakaa moja na hili kundi la kwanza na watakaponyanyuka kuswali rakaa ya pili Imamu atabakia pale akiendelea kusoma Qur-an na kila mtu katika wale wanaomfuata, atamaliza upesi upesi rakaa ya pili na baada ya kutoa Salaam atarudi nyuma upesi kuchukua nafasi ya ulinzi. Baada ya kundi la pili kupokelewa nafasi zao, watakwenda kujiunga na Imamu ambaye bado anaendelea na rakaa yake ya pili. Wote watakapojiunga na swala, Imamu atamalizia swala yake ya rakaa mbili. Baada ya Imamu kutoa salaam kila mmoja katika wale wanaomfuata atasimama na kumalizia rakaa yake ya pili.

 


Aya hii ya (4:102) inayotuelekeza namna ya kuswali tukiwa katika vita vya kupigania Dini ya Allah (s.w) inafuatiwa na aya inayotoa amri ya kusimamisha swala kwa nyakati zake kama tunavyosoma:

 

Mwishapo kuswali kuweni mnamkumbuka Mwenyezi Mungu - msimamapo na mkaapo na (mlalapo) ubavu. Na mtakapopata amani, basi simamisheni swala (kama kawaida). Kwa hakika swala kw a Waislamu ni faradhi iliyow ekewa nyakati maalumu. (4:1 03)

 


Hebu fikiri: Kama askari wa Allah (s.w) aliyejitoa muhanga kwa mali yake, ahli zake na nafsi yake kwa ajili ya kupigania dini ya Allah (s.w) hakuruhusiwa kuiacha swala au kuiswali nje ya wakati wake, je wewe uliyezama kwenye shughuli nyingine ndio utegemee kusamehewa kwa kupitisha wakati wa swala ukaswali wakati unapojiona kuwa huna shughuli. Aya hii inatufahamisha kwa uwazi kuwa swala tano zimefaradhishwa kwetu pamoja na nyakati zake makhsusi.

 


Tukiondoa ruhusa tulizopewa kuziswali swala kidharura tunapokuwa vitani, na tukiondoa udhuru wa kusahau na kupitiwa na usingizi hapana ruhusa yoyote iliyotolewa katika Qur-an au Hadithi inayokubalika kuswali kadha kama wengi wafanyavyo. Je, mtindo huu wa kuswali kadha tunauiga kwa nani? Je, huku sio kupuuza swala? Kama tunapuuza swala kwa nini tusitarajie kupata ghadhabu za Allah (s.w) badala ya kujidanganya na kujipa matumaini ya kupata malipo mema kutoka kwake kutokana na kadha zetu hizo. Ujira wa wapuuzaji wa swala unabainishwa katika Qur-an:

 

Basi, adhabu itawathibitikia wanao swali. Ambao wanapuuza zao. (10 7:4-5).

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1323

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

MARADHI MENGINE 10 YANAYOTOKANA NA MBU ( matende, ngirimaji, homa ya manjano, n.k

Tofauti na maradhi yaliyotajwa hapo juu pia tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwepo kwa maradhi mengine hatari yanayosambazwa na mbu, kama vile ngirimaji pamoja na matende.

Soma Zaidi...
Kwanini wengi wanaoswali hawafikii lengo la swala zao

Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Utaijuwaje kama swala yako imekubalika

Hapa tunakwenda kuona jinsi ya kuzitathmini swala zetu.

Soma Zaidi...
MALI ZISIZORUHUSIWA KUTOLEWA ZAKA

*Suala la kumilikiwa binaadam (utumwa), japokuwa linaendelea kutajwa kwenye Sharia (katika vitabu), ni suala ambalo haliko.

Soma Zaidi...
Kugungisha ndoa ya kiislamu hatuwa kwa hatuwa

Hapa utajifunza jinsi ya kuozesha hatuwa kwa hatuwa. Pia utajifunza masharti ya kuoa na masharti ya kuolewa.

Soma Zaidi...
Swala ya jamaa.

Kipengele hiki tutajifunza kusimamisha swala ya jamaa,swala za ijumaa.

Soma Zaidi...
Ijuwe swala ya Tawbah na jinsi ya kuiswali

Post hii itakufundisha kuhusu swala ya sinnah ya tawba.

Soma Zaidi...