Hapa utajifinza uharamu wa riba na sababu za kuharamishwa kwake.
Uharamu wa Riba katika Uislamu
Kwanza, Uislamu umeharamisha riba kwa sababu ni dhulma (unyonyaji).Ukichukua mkopo wa riba uliochukuliwa kwa madhumuni ya kukidhi haja ya matumizi ya lazima ya nyumbani, utozaji wa riba unakiuka lengo la Allah la kuumba (kuleta) mali kwa wanadamu. Utaratibu aliouweka Allah ni kwamba kwa kuwa mali ameileta kwa wanaadamu wote:
“Yeye (Allah) Ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi...” (2:29).
Ni lazima matajiri (wenye mali) wawapatie wanyonge na wenye dhiki mahitaji yao muhimu ya maisha.
Pili, riba imeharamishwa katika Uislamu kwa sababu inahamisha mali kutoka kwa maskini au wanyonge na kuipeleka kwa tajiri ambayo huzidi kuondoa usawa katika mgawanyo wa mali. Hii ni kinyume na mahitaji ya jamii. Uislamu unataka kila mtu apate mahitaji muhimu ya maisha. Hivyo wale walio na ziada ya mahitaji muhimu ya maisha wanatakiwa wawape wasionacho kabisa au wale waliopungukiwa kwa upendo na udugu. Riba inakanusha kabisa msimamo huu.
Tatu, riba imeharamishwa katika Uislamu kwa sababu hufanya kundi la watu katika jamii liishi kivivu bila ya kufanya shughuli yoyote ya uzalishaji, likitegemea kuishi kwa riba kutokana na mali zao walizozikusanya katika mabenki, bima, na vyombo vingine vya riba. Jamii inakosa mchango wa watu hawa katika uzalishaji na si hivyo tu, bali watu hawa wanakuwa mzigo na bughudha katika jamii. Ufasiki (uharibifu) wa aina zote katika ardhi hufanywa na kundi hili.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Hapabutajifunza endapp mwanamke anahitaji kuachwa ni nini anatakiwa afanye.
Soma Zaidi...Nazingatio muhimu katika uchumi unaofuata sheria za kiislamu.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi.
Soma Zaidi...Kabla ya kuhubiriwa uislamu watu wa Maka walikuwa na tarayibu zenye dhuluma ndani yake katika ugawaji wa mirathi.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...