KUGUNGISHA NDOA YA KIISLAMU HATUWA KWA HATUWA


image


Hapa utajifunza jinsi ya kuozesha hatuwa kwa hatuwa. Pia utajifunza masharti ya kuoa na masharti ya kuolewa.


Kufunga Ndoa Kiislamu

Iii ndoa ifungike Kiislamu ni lazima yatekelezwe yafuatayo:
(i)Mume atekeleze masharti ya kuoa.
(ii)Mke atekeleze masharti ya kuolewa.
(iii)Pawe na Walii au Idhini yake.
(iv)Pawe na mashahidi wawili au zaidi.
(v)Pawe na idhini (ridhaa) ya mwenye kuolewa.
(vi)Pawe na Ijabu na Kabuli.

 


(i) Masharti ya Kuoa
(a)Mke anayemuoa awe Muislamu mwema au ahlul-kitaab mwema.
(b)Awe anaoa kwa hiari yake (halazimishwi).
(c)Asiwe maharimu wa mke anayemuoa.
(d)Awe baleghe na mwenye akili timamu.
(e)Asiwe katika Ihramu ya Hijja (asiwe amehirimia Hijja).
(f)Asiwe na ndoa ya wake wane ambao anaishi nao katika ndoa.

 


(ii)Masharti ya Kuolewa
(a)Mume anayemuoa awe muislamu mwema.
(b)Asiwe katika ndoa ya mume mwingine.
(c)Asiwe katika eda ya mume mwingine.
(d)Awe mwema (Rejea Qur-an, 5:5).
(e)Asiwe maharimu kwa mume anayemuoa.
(f) Awe na akili timamu.
(g)Asiwe katika Ihramu ya Hijja.
(h) awe anaolewa kwa ridhaa yake, sio kwa kulazimishwa.

 


(iii)Walii au Idhini yake
Ndoa ya Kiislamu haikamiliki mpaka awepo walii wa binti anayeolewa ambaye ndiye muozeshaji au pawe na idhini yake kama tunavyojifunza katika hadithi zifuatazo:
Abu Mussa (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: "Hakuna ndoa ila kwa kuozeshwa na walii ". (Ahmed, Tirmidh, Abu Daud na Ibn Majah).

 


Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: Hapana mwanamke atakayemuozesha mwanamke mwingine, wala hapana mwanamke atakayejioza mwenyewe.Hakika mwanamke mzinfu ni yule anayejiozesha mwenyewe. (Ibn Majah)

 


Kazi ya Walii ni kufungisha ndoa yeye mwenyewe. Lakini anaweza kuwakilishwa na mtu mwingine, mwanamume mjuzi, afungishe ndoa kwa niaba yake.
Katika sheria ya Kiislamu mawalii wanaoweza kuozesha ni hawa wafuatao kwa mujibu wa daraja zao:

 

1.Baba Mzazi wa mwanamke anayeolewa.
2.Babu mzaa baba yake.
3.Ndugu yake wa kiume wa baba mmoja na mama mmoja.
4.Ndugu yake wa kiume wa baba mmoja.
5.Mtoto wa kiume wa ndugu yake wa kiume wa baba mmoja na mama mmoja (Mpwa wake).
6.Mtoto wa kiume wa ndugu yake wa kiume wa baba mmoja.
7.Baba yake mdogo (Ami) aliyezaliwa na baba yake kwa baba mmoja na mama mmoja..
8.Baba yake mdogo (Ami) aliyezaliwa na baba yake kwa baba tu.
9.Mtoto wa kiume wa baba yake mdogo wa kwa baba yake mdogo na mama.
1O.Mtoto wa kiume wa baba yake mdogo kwa baba tu.
11.Serikali (Hakim au Kadhi) katika nchi za Kiislamu.

Walii wa daraja ya chini katika orodha hii hawezi kuozesha mpaka iwe walii wa daraja ya juu yake hayupo. Kwa mfano, babu hawezi kuozesha kama baba mzazi yupo, ndugu yake hawezi kuozesha ikiwa babu yupo, na kadhalika. Ikiwa waliii wa daraja ya chini ataozesha na hali yakuwa walii wa daraja ya juu yupo, na hakuridhia, basi ndoa haitasihi. Mtu ambaye hayumo katika orodha ya mawalii wala si mtoto wa kiume wa hao waliotajwa hapo juu hawezi kuozesha. Endapo mawalii wote watakosekana, Kadhi au kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu atamuozesha binti huyo.

 


Walii ili aweze kuozesha ni lazima atimizwe masharti yafuatayo:

 

(a)Awe Muislamu mwanamume.
(b)Asiwe mtumwa (awe muungwana).
(c)Awe mwenye akili timamu.
(d)Awe anaozesha baada ya kupatikana idhini ya mwenye kuolewa.

 

(e)Awe muadilifu.
(iv)Pawe na Mashahidi wawili
Ndoa haisihi bila ya kushuhudiwa na mashahidi wawili wenye sifa zifuatazo:
(a)Wawe watu Wazima waliokwisha baleghe. Watoto hawawezi kuwa mashahidi.
(b)Wawe na akili timamu.
(c) Wawe Waislamu wanaume.
(d)Wawe waadilifu.
(e)Wawe waungwana (sio watumwa).
(v)Ridhaa (Idhini) ya mwenye Kuolewa

 


Iii ndoa ya Kiislamu ikamilike ni lazima idhini ya mwanamke anayeolewa ipatikane.Mtume (s.a.w) ameliweka hili wazi kama tunavyojifunza katika hadithi zifuatazo:
Abu Hurairah(r.a) ameeleza lw,,va Mtume (s.a.w) ameema: Msichana baleghe atatakiwa idhiniya Iwolewa kwake. Akfryamaza k?nya, itachulwliwa kuwa ameiwbali, na akikataa hatalazimishwa kuolewa. (7nnidh, Abu Daud, Nasai).

 


Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: Mwanamke aliyewahi kuolewa hataolewa mpaka akubali, wala mwanamke bikra hataozwa mpaka atakwe idhini. Waliuliza: Idhini yake itakuwa vipi? Akasema (Mtume): Kama atanyamaza kimya ". (Bukhari na Muslim).

 


(vi)Pawe na Ijabu na Kabuli
Ijabu: ni yale maneno anayosema walii kumwambia mume anayeoa kama hivi:"Nimekuoza Aisha binti Salim" wala asiseme: "Ninakuoza..."
Kabuli ni maneno ya mume ya kukubali kumuoa binti anayetaka kumuoa kwa kusema: "Nimekubali kumuoa Aisha bint Salim", wala asisema: "Ninakubali kumuoa..."
Kwa hiyo Ijabu ni kauli rasmi anayotoa walii au muwakilishi wake mbele ya mashahidi wawili ya kumuoza mke kwa mume na Kabuli ni kauli rasmi anayoitoa mume ya kumkubali mke katika ndoa.

 

mfano:
Walii: Shaaban bin Abdurahman.
Shaaban: Labbayka.
Walii: Umekubali kumuoa Aisha bint Salim?
Shaaban: Naam, Nimekubali kumuoa 'Aisha bint Salim.
Walii atamuuliza Shaaban kama hivyo mara mbili na mara ya tatu atamalizia kama ifuatavyo:
Walii: (Mara ya tatu): Ewe Shaaban bin Abdurahman, nakuoza kwa namna alivyoamrisha Mwenyezi Mungu, nayo ni kukaa naye kwa wema na kutokana naye kwa wema vile vile.
Ijabu: Nimekuoza Aisha binti Salim kwa ridhaa yake mwenyewe, (Kutajwa mahari si lazima).
Kabuli: Nimekubali kumuoa Aisha bint Salim
Muhimu: Kilicho lazima katika kufungisha ndoa ni kupatikana kwa Ijabu na Kabuli. Kwa mfano, Walii badala ya kumuuliza Shaaban mara mbili: "Umekubali kumuoa.. .", anaweza kumuoza Shaban moja kwa moja kwa kauli ya Ijabu: Shaaban bin Abdurahman Nimekuoza..

 

Baada ya ndoa kufungwa ni sunnah kumshika mkono mwenye kuoa na kumuombea dua kama alivyofanya Mtume (s.a.w) kwa Abdul-Rahman bin Awf (r.a) kwa kusema:

 

'Mwenyezi Mungu akubariki" (Bukhari na Muslim)

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    2 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    3 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    4 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    6 Magonjwa na afya    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Namna ya kuswali hatuwa kwa hatuwq
Post hii itakufundisha jinsi ya kuswali hatuwa kwa hatuwa. Soma Zaidi...

image Taratibu za mahari katika uislamu
Hapa utajifunza taratibu za kutaja mahari katika uislamu. Soma Zaidi...

image Tofauti ya uchumi wa kiislamu na uchumi wa kikafiri
Uchumi wa kiislamu unatofautiana sana na uchumi wa kikafiri. Hapa utajifunza tofauti hizo. Soma Zaidi...

image Nguzo za udhu ni sita
Post hii itakufundisha kuhusu nguzo kuu sita za udhu. Soma Zaidi...

image Yaliyo haramu kwa mwenye hadathi kubwa.
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ya haramu kwa mwenye hadathi kubwa Soma Zaidi...

image Usawa na uhuru wa kuchuma mali katika uislamu
Uchumi wa uislamu umeweka taratibu mbalimbali katika kuchuma mali. Soma Zaidi...

image Taratibu za kumiliki hisa na mali ya shirika
Katika Uislamu kuwa na hisa kwenye mali inaruhusiwa. Hapa utajifunza taratibu za kumiliki hisa. Soma Zaidi...

image Taratibu za kutaliki katika uislamu.
Hapa utajifunza taratibu zinazofuatwa wakati wa kukusudia kumuacha mke. Pia utajifunza sababu za kiwepo kwa eda baada ya kuachwa mwanamke. Soma Zaidi...

image Yaliyo haramu kwa mtu asiyekuwa na udhu
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ambauo ni haramu kwa mtu asiye na udhu. Soma Zaidi...

image Swala ya tahiyatul masjidi yaani maamkizi ya msikitini, pamoja na swala za qabliya na baadiya
Post hii inakwenda kukujuza kuhusu swala za qabliya, baadiya na tahiyatul masjid. Soma Zaidi...