Post hii itakujuza jinsi ya kiswali swala ya tahajudi. Pia utajifunza jinsi ya kuswali swala za usikubyaanibqiyamublayl
4. Swala ya Tahajjud
Swala ya Tahajjud ni miongoni mwa swala zilizokokotezwa sana katika Qur-an na Hadithi. Neno “Tahajud” lina maana ya kuamka kutoka usingizini. Swala hii huswaliwa usiku wa manane, hasa katika theluthi ya mwisho wa usiku karibu na al-Fajiri.
Swala hii vile vile hujulikana kwa jina la “Qiyaamul-layl”. Yaani kisimamo cha usiku kwa sababu inakuwa na visimamo virefu ambapo Qur-an husomwa kwa urefu. Mkokotezo wa swala ya Tahajjud unadhihirika katika aya za Qur-an zifuatazo:
Na katika usiku jiondoshee usingizi (kid ogo) kwa (kusoma) hiyo (Qur-an ndani ya Swala).Hiyo ni (Ibada) zaidi kwako. Huwenda Mola wako akakuinua cheo kinachosifika. (17:79).
Miongoni mwa sifa za waja wema wa Allah (s.w) ni pamoja:
“Na wale wanaopitisha baadhi ya saa za usiku kwa ajili ya Mola wao kwa kusujudu na kusimama ”. (25:64).
J e , afanyaye ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama na kuogopa Akhera na kutarajia rehema ya Mola wake (ni sawa na asiyefanya hayo)? Sema: “Je, wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?” Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu. (39:9)
Pia Mtume (s.a.w) amekokoteza Swala za Usiku kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo.
Abu Umamah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Jizoesheni kusimama Usiku (kwa swala) kwa sababu ilikuwa ndio tabia ya Wacha-Mungu w aliokutangulieni na ni njia ya kukukurubisheni karibu na Mola wenu na ni njia ya kufutiwa dhambi na ni kizuizi cha kutenda maovu (dhambi)”. (Tirmidh).
Idadi ya rakaa alizoswali Mtume (s.a.w) katika hii swala ya Tahajjudi ni nane (8) na kisha akamalizia na rakaa tatu za Witri. Katika hizi rakaa nane alitoa salam kila baada ya rakaa mbili. Mtume (s.a.w) alikuwa akisoma Qur-an kwa kitambo kirefu kwa kila rakaa kiasi kwamba miguu yake ilikuwa inavimba kama tunavyojifunza katika Hadithi ifuatayo:-
“Mughirah (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa akisimama katika (sw ala ya usiku) kwa kitambo kirefu kiasi kw amba miguu yake ilivimba, akaulizwa: Kwanini unafanya hivi ambapo umesamehewa dhambi zako zilizotangulia na zitakazokuja? Akauliza: “Nisiwe mja mwenye Shukrani?” (Bukhari na Muslim).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Post hii itakufundisha mambo ambayo yatasababisha swqla yako isikubaliwe.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha jinsi ya kuswali hatuwa kwa hatuwa.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza watu ambao ni halali kuwaoa na wale ambao ni haramu kuwaoa.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha sunnah 9 za swala. Sunnah hizi ni zile ambazo ukiziwacha swala yako haibatiliki.
Soma Zaidi...Tumesha mzika maiti sasa imebakia mali yae nyumbani, watoto, wake na menginyeo.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha faida na umuhimu wa kijenga uchumi katika jamii ya kiislamu.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza mambo ambayo akiyafanya mtu aliyefunga, basi funga yake itaharibika.
Soma Zaidi...