(h) Kujiepusha na Kibri na Majivuno"Wala usiwatizame watu kwa upande mmoja wa uso (usiwafanyie watu jeuri) Wala usiende katika nchi kwa maringo; Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunaye, ajifaharishaye" (31:18)"Wala usitembee (usiende) katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala huwezi kufikia urefu wa mlima. Haya yote ubaya wake ni wenye kuchukiza mbele ya Mola wako" (17:37-38)Kibri ni tabia ya kukataa ukweli na kuwadharau watu kama tu navyoj ifu nza katika Hadithi ifuatayo:
"Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa, Mtume wa Allah am esem a, "Yule ambaye moyoni mwake mnachembe ya kibri hataingia peponi" Swahaba mmoja akauliza: "Je kama mtu anapenda nguo nzuri na viatu?" Mtume (s. a.w) akasema, "Allah (s.w) ni mzuri na anapenda vizuri. Kibri ni kukataa ukweli na kupuuza watu ". (Muslimu)Vile vile kibri na majivuno ni tabia ya kishirikina kama tunavyojifunza katika Hadithi nyingine ifuatayo:


"Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema; Allah akasema; Utukufu ni nguo yangu na kibri ni kilemba changu. Yeyote atakaye shindania kimoja wapo katika hivi ataangamia." (Muslimu)Mtu mwenye kibri na majivuno daima atakuwa ni mpinzani wa harakati za kusimamisha Uislamu katika ardhi, kwani atapendelea utawala ule ambao utamfanya kuwa mungu katika jamii.