Mtazamo wa Uislamu juu ya maana ya dini

Uislamu unaitazama dini katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Hii ni tofauti na mtazamo wa kikafiri juu ya dini.

Maana ya Dini kwa mtazamo wa Uislamu

Kwa mtazamo wa Uislamu “Dini” ni utaratibu wa maisha wanaoufuata binaadamu katika kuendesha maisha yao ya kila siku ya kibinafsi na kijamii. Ni katika maana hii ya dini Allah (s.w) huuliza katika aya ifuatayo:

 

“Je, (watu) wanataka dini isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu na hali kila kilichomo mbinguni na ardhini kimejisalimisha kwake kipende kisipende. Na kwake wata rejeshwa wote.” (3:83).


Kutokana na aya hii tunajifunza kuwa:Kwanza, kuna dini nyingi zinazofuatwa na watu hapa ulimwenguni, lakini dini iliyostahiki watu wenye “akili timamu” waichague, ni ile dini inayofuatwa na maumbile yote.


Pili, dini ya maumbile yote ya mbinguni na ardhini si nyingine, ila ni ile ya kujisalimisha katika kufuata sheria za maumbile alizoziweka Muumba.

 

Tukirejea kwenye sayansi ya maumbile (natural science) tunajifunza kuwa kila kitu kilicho hai na kisicho hai (living and nonliving thing) ili kiwepo ni lazima kifungamane na sheria za maumbile za kibailojia, kifizikia na za kikemia (Biological, Physical and Chemical laws). Kwa mtazamo huu hata miili yetu pia imejisalisha kwa muumba kwa kufuata sheria za maumbile pasina hiari kama inavyosisitizwa katika aya ifuatayo:

 


“Basi uelekeze uso wako katika dini iliyo sawa saw a ndilo umbile Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu (yaani dini hii ya Kiislamu inawafikiana bara bara na umbile la binaadamu).Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Mwenyezi Mungu.

 

Hiyo ndio dini iliyo ya haki lakini w atu wengi hawajui.” (30:30)
Kwa ufupi, aya hii inatukumbusha kuwa miili yetu imejisalimisha kwa Allah (s.w) bila ya hiari kwa kufuata bara bara sheria za maumbile zinazofungamana na ufanyaji kazi wa kila kiungo cha mwili.Chakula kinayeyushwa tumboni, moyo unasukuma damu, mapafu, ini, figo, na viungo vingine mwilini hufanyakazi kwa kufuata sheria za Muumba na wala sio kwa kufuata sheria walizozitunga wanaadamu katika mabunge yao.

 


Tatu, Uislamu ni mfumo wa maisha uliofungamana na kanuni na sheria alizoziweka Muumba ili watu waendeshe maisha yao ya kibinafsi na kijamii sambamba na hali halisi ya maumbile yaliyowazunguka.

 

Wale watakaoamua kwa hiari yao kufuata kanuni na sheria alizoziweka Allah (s.w) katika kukiendea kila kipengele cha maisha yao ya kila siku watakuwa ni Waislamu, waliojisalimisha kwa Muumba wao kama ilivyojisalimisha miili yao na maumbile yote ya mbinguni na ardhini.

 

Hawa wataishi kwa furaha na amani hapa ulimwenguni, kwani wataepukana na maisha yale ya kupingana na maumbile yaliyowazunguka. Ama wale watakaokataa kufuata kanuni na sheria alizoziweka Muumba na badala yake wakaweka mfumo wa maisha unaopingana na kanuni na sheria hizo watakuwa ni makafiri, walioamua kupingana na maumbile yote yaliyowazunguka. Kwa vyovyote vile watakuwa wameamua kuishi maisha ya upinzani na vurugu.

 

Nne, kimantiki, ni lazima iwepo siku ya Hisabu ambapo watu wote watahudhurishwa mbele ya mahakama ya Muumba na Mmiliki wa maumbile yote, ili walipwe kutokana na uamuzi wao katika kuchagua na kufuata “dini”. Wale waliojisalimisha kwa Allah (s.w) na kufuata “dini” yake, pamoja na kuishi maisha ya nuru (ya Amani na Heshima) hapa duniani, watakuwa na maisha ya furaha na amani ya kudumu huko Peponi. Ama wale waliompinga Allah (s.w) kwa kuweka na kufuata mifumo ya maisha kinyume na “dini” yake, pamoja na kuishi maisha ya giza (ya khofu na huzuni) hapa duniani, watakuwa na maisha ya dhiki na adhabu kubwa huko Motoni kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:

 

“Mwenyezi Mungu ni Mlinzi (kiongozi) wa wale walioamini. Huwatoa katika giza na kuwaingiza katika nuru.Lakini w aliokufuru, w alinzi (viongozi) w ao ni Matwaghuut.Huwatoa katika nuru na kuwaingiza katika giza.Hao ndio watu wa Motoni, humo wakakaa milele”. (2:257)

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 1931

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

(c)Vipawa vya Mwanaadamu

Vipawa vya mwanaadamu ni sababu nyingine inayomfanya mwanaadamu asiweze kuishi bila ya kufuata dini moja au nyingine.

Soma Zaidi...
Mambo muhimu anayofanyiwa muislamu kabla ya kufa

Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Neema za Allah(s.w) Juu ya Bani Israil

Katika Qur'an tunakumbushwa neema mbali mbali walizotunukiwa Bani Israil (Mayahudi) na Mola wao ili kuwawezesha kusimamisha Ufalme wa Allah(s.

Soma Zaidi...
Lengo la kushushwa vitabu vya mwenyezi Mungu (s.w)

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Aina kuu za dini

Katika kipengele hichi tutajifunza aina kuu mbili za dini.

Soma Zaidi...
Maana ya muislamu.

Kwenye kipengele hichi tutajifunza ni nani muislamu.

Soma Zaidi...
Kumuamini malaika wa mwenyezi Mungu

Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...