image

Maadili kati surat Al-Hujurat (49:1-13)

Enyi mlioamini!

Maadili kati surat Al-Hujurat (49:1-13)

(5) Maadili kati surat Al-Hujurat (49:1-13)


Enyi mlioamini! Msitangulize (neno lenu) mbele ya (neno la) Mwenyezi Mungu na Mtume wake; na Mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. Enyi mlioamini! msipaze sauti zenu kuliko sauti ya Mtume wala msiseme naye kwa sauti ya nguvu kama mnavyosemezana nyinyi kwa nyinyi, visije vitendo vyenu vikakosa thawabu, na hali hamtambui. (49:1-2)



Kwa hakika wale wanaoangusha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao ndio Mwenyezi Mungu amezisafisha nyoyo zao kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu. Basi yatakuwa kwao maghufira na thawabu kubwa (kabisa). Wale wanaokwita nyuma ya nyumba; (uko ndani kwako, wanakuja kukugongea dirisha na kukwita); wengi wao hawafahamu (adabu).Na kama wangalingoja mpaka uwatokee, ingekuwa bora kwao.Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira (na) Mwenye rehema. (49:3-5)


Enyi mlioamini! Kama fasiki, (asiyekuwa wa kutegemewa) akikujieni na habari (yoyote ile msimkubalie tu) bali pelelezeni (kwanza), msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa wenye kujuta juu ya yale mliyoyatenda. Na jueni ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko pamoja na nyiye. (Basi msikilizeni yeye anavyokuambieni). Lau yeye angekutiini katika mambo mengi (mnayoyasema) bila shaka mngetaabika. Lakini Mwenyezi Mungu ameupendezesha kwenu Uislamu na ameupamba nyoyoni mwenu, na amekufanyeni mchukie ukafiri na ufasiki na uasi. Hao ndio walioongoka. (49:6-7)


Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na neema (zake mmepata haya). Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima. Na ikiwa makundi mawili katika waislamu yanapigana, basi fanyeni suluhu baina yao; na likiwa moja la hayo linamdhulumu mwenziwe, basi lipigeni lile linaloonea mpaka lirudie katika amri ya Mwenyezi Mungu. Na kama likirudi, basi yap atanisheni baina yao kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki.Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaohukumu kwa haki. Kwa hakika Waislamu wote ni ndugu; basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na Mcheni Mwenyezi Mungu, ili mrehemewe. (49:8-10)


Enyi mlioamini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao; huenda wakawa bora kuliko wao; wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao; huenda wakawa bora kuliko wao. Wala msitukanane kwa kabila, wala msiitane kwa majina mabaya (ya kejeli): Jina baya kabisa kuambiwa mtu ni asi baada ya kuwa ni Muislamu. (Na kufanya haya ni uasi) Na wasiotubu, basi hao ndio madhalimu (wa nafsi zao). (49:11)


Enyi mlioamini! Jiepusheni sana na (kuwadhania watu) dhana (mbaya) kwani (kuwadhania watu) dhana (mbaya) ni dhambi. Wala msipeleleze (habari za watu). Wala baadhi yenu wasiwasengenye wengine. Je! Mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa? La, Hampendi; (Basi na haya msiyapende). Na Mcheni Mwenyezi Mungu. Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba (na) Mwingi wa kurehemu. Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanamume (mmoja, Adamu) na (yule yule) mwanamke (mmoja; Hawwa). Na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbali mbali) ili mjuane (tu basi; siyo mbaguane). Hakika ahishimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mungu zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye habari (za mambo yote). (49:12-13)


Mafunzo
Kutokana na aya tulizozisoma tunajifunza yafuatayo:
Kwanza
, waumini wa kweli ni wale ambao hawafanyi jambo lolote kinyume na alivyo agiza Mwenyezi Mungu na Mtume wake.



Pili, waumini wa kweli wanatakiwa wawe na adabu katika kuongea. Wakiongea na wakubwa zao ki-umri au kicheo, wanalazimika kushusha sauti zao.



Tatu, waumini wote ni ndugu moja na waislamu wameamrishwa na Allah (s.w) kuudumisha udugu huu kwa kujizatiti katika kusuluhisha waliogombana wakiwa mmoja mmoja au katika kundi.



Nne, ili kudumisha udugu baina yao, waislamu wanaamrishwa na Mola wao kujiepusha na uzushi, dharau, kutukanana, dhana mbaya, kusengenya na kujiona na kujikweza.



Tano, waumini wanaaswa wasitoe hukumu dhidi ya watu kutokana na tetesi tu. Hawanabudi kufanya uchunguzi juu ya shutuma zilizokuja na kisha kutoa hukumu baada ya kupatikana ushahidi wa wazi




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 636


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat As-Sajida
Nao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya? Soma Zaidi...

Njia ambazo Allah hufundisha wanadamu elimu mbalimbali
Ni kipi chanzo cha Elimu, na ni kwa namna gani Allah hufundisha Elimu kwa wanadamu? Soma Zaidi...

Kutopupia dunia
"Ewe mwanangu! Soma Zaidi...

Kwa nini hakuna haja ya Mtume mwingine baada ya Muhammad
Na tukiutafiti Uislamu kwa makini kama mfumo kamili wa maisha tunaona unadhihiri ukweli wa aya hii ya Qur-an. Soma Zaidi...

Maana ya Kuamini Mitume wa Allah (s.w) katika maisha ya kila s iku.
Waumini wa kweli wa Mitume wa Allah (s. Soma Zaidi...

Kuwa wenye shukurani mbele ya Allah (s.w)
Mwanaadamu ametunukiwa neema mbali mbali na Mola wake kuliko viumbe wengine wote kama tuanvyojifunza katika aya mbali mbali za Qur'an. Soma Zaidi...

Maswali juu ya mtazamo wa uislamu kuhusu dini
Mtazamo wa uislamu kuhusu dini (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

KUAMINI SIKU YA MALIPO
Soma Zaidi...

Madai ya Makafiri dhidi ya kuwepo kwa Allah (s.w) na Udhaifu wa Madai hayo.
2. Soma Zaidi...

Kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila dini?
Mwanadamu hawezi kuishi bila dini, kwani dini imekusanya mfumo mzima wa maisha yake. Soma Zaidi...

Kujiepusha na Kibri na Majivuno
Soma Zaidi...

Nguzo za Imani kwa mujibu wa mafunzo ya kiislami.
Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu nguzo sita za imani katika Uislamu. Soma Zaidi...