(f)Kusimamisha Swala



Swala iliyosimamishwa vilivyo ndiyo nyenzo kuu ya kumtakasa Muislamu na kumpa sifa zinazomuwezesha kustahiki kufanya kazi takatifu ya kusimamisha Uislamu katika jamii. Swala ikisimamishwa vilivyo humuwezesha mja kumcha Allah (s.w) ipasavyo katika kukiendea kila kipengele cha maisha yake ya kibinafsi na pia ni msingi wa kumpelekea mja kusimamisha Uislamu katika jamii.



(g)Kuamrisha mema na kukataza mabaya na kusubiri juu yale yatakayokusibu
Kuamrisha mema na kukataza maovu ni masuala yanayohitaji mamlaka na nguvu (authority and power). Hata hivyo kuwa na mamlaka na nguvu sio lazima ianzie kileleni katika ngazi ya Dola, bali mamlaka na nguvu ya kuamrisha mema na kukataza mabaya huanzia kwa mtu binafsi, kisha kwa familia yake kisha kwa ndugu na jamaa zake wa karibu. Kuamrisha mema na kukataza maovu ni wajibu kwa waumini wote (Qur'an 3:104, 3:110, 8:25, n.k).



Kuamrisha mema na kukataza maovu ni suala la mapambano hata katika ngazi ya mtu binafsi na katika ngazi ya familia. Ni shughuli inayohitajia kuwa na subira ya hali ya juu. Subira ina maana pana ikiwa ni pamoja na:


1.Wewe mwenye kubakia na msimamo wa kufanya mema na kujiepusha na maovu
2.Kuwahimiza na kuendelea kuwashupalia kufanya mema
na kuacha maovu wale ambao unamamlaka juu yao.
3.Kuwa tayari kulaumiwa na yeyote atakayelaumu.
4.Kuwa tayari kukabiliana na magumu yoyote
yata kayo kufika.
5.Kutotarajia kupata matunda ya haraka haraka kutokana na kazi ya kuamrisha mema na kukataza mabaya.