"Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu
"Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu ni kwangu, hapo nitakuambieni mliyokuwa mkiyatenda." (31:15).
Aya inabainisha wazi kuwa hatupaswi kuwatii wazazi wetu pale watakapotuamrisha kumuasi Allah (s.w). Tukiwatii tutakuwa tumemshirikisha Allah (s.w) kwa kuwafanya wazazi wetu miungu badala yake kama inavyo bainika katika Qur'an.
βMayahudi na Wakristo) wamewafanya wanavyuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Allah (s.w) β¦." (9:31)
Iliposhushwa aya hii Adi bin Hatimu (r.a) ambaye alisilimu kutoka kwenye Ukristo, alimtaka Mtume (s.a.w) atoe ufafanuzi kwa sababu alidai kuwa kinadharia hawakuwa wanawafanya watawa wao miungu. Katika kufafanua, Mtume (s.a.w) alimuuliza Adi, "Je hawakuwa watawa wenu wanawahalalishia alivyo viharamisha Allah (s.w) na nyinyi mkawatii?" Alijibu Adi, "Ndiyo" Mtume (s.a.w) akamuuliza tena, "Je watawa wenu hawakuwa wanakuharamishieni alivyo halalisha Allah (s.w) na nyinyi mkawatii? Adi akajibu tena "Ndiyo." Basi Mtume (s.a.w) akasema, "Huko ndio kuwafanya miungu".
Hivyo, kumtii mzazi au kiongozi au yeyote yule katika kumuasi Allah (s.w) ni kumfanya mungu badala ya Allah (s.w). Pia ukitii matashi ya nafsi yako kinyume na amri au makatazo ya Allah (s.w) utakuwa umeifanya nafsi yako mungu badala ya Allah (s.w).
"Je, umemuona yule aliyefanya matamanio yake, (kile anachikipenda), kuwa Mungu wake? Basi je, utaweza kuwa mlinzi wake (ukamhifadhi na hayo, na hali ya kuwa hataki?). "(25:43).
Lakini, tunaamrishwa katika aya hii (31:15) kuwa pamoja na kutowatii wazazi wetu katika kumshirikisha Allah (s.w), tusiwe jeuri na fedhuli kwao, bali tuzungumze nao kwa upole kwa kauli njema na tuendelee kuwatii na kuwafanyia wema katika mambo yote ya halali.
Wakati mwingine wazazi wanaweza kutishia kuacha laana tutakapowakatalia kwa kauli nzuri kutowatii katika yale yatakayotupelekea kumuasi na kumshirikisha Allah (s.w). Tusiyumbishwe na tishio hili kwa sababu marejeo yetu sote ni kwa Allah (s.w) na ni mjuzi kamili juu ya dhamira (nia) zetu na vitendo vyetu - "β¦kisha marejeo yenu ni kwangu, Hapo nitakuambieni mliyokuwa mkiyatenda" (31:15).
Umeionaje Makala hii.. ?
Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...(i) Kutiishiwa Upepo Qur'an inatufahamisha kuwa Nabii Sulaiman alitiishiwa upepo akaweza kuutumia apendavyo kwa amri yake.
Soma Zaidi...Nao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya?
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hichi tutajifunza makundi ya dini za watu. Na makundi hayo ni matatu.
Soma Zaidi...Mwanadamu ukifikiria vyema. Kuhusu nafsi yako, hakika utapatabfikra yabuwepp wa Mwenyezi Mungu
Soma Zaidi...Mwanaadamu ametunukiwa neema mbali mbali na Mola wake kuliko viumbe wengine wote kama tuanvyojifunza katika aya mbali mbali za Qur'an.
Soma Zaidi...Elimu imepewa kipaumbele kikubwa kwenye uislamu. Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu nafasi ya Elimu katika uislamu.
Soma Zaidi...