Navigation Menu



image

Maana ya Kumuamini Allah (s.w) katika Utendaji wa kila siku

Maana ya Kumuamini Allah (s.w) katika Utendaji wa kila siku

Maana ya Kumuamini Allah (s.w) katika Utendaji wa kila siku




Hatua ya tatu na ya mwisho katika kuiendea Imani ya kweli juu ya Allah (s.w) ni hatua ya utendaji. Hivyo kiutendaji anayemuamini Allah (s.w) ni yule anayefuata maamrisho yake yote na kuacha makatazo yake yote pamoja na kuyaendea maisha yake ya kibinafsi na ya kijamii kwa kufuata mwongozo wake pekee
Rejea kurasa za mwanzo juu ya "Nani Muumini?"
Aidha Muumini wa kweli ni yule atakayejitenga mbali na ama zote za shirk. Shirk ni kujaalia kinadharia au kiutendaji kuwa yupo mungu au miungu wengine pamoja na Allah (s.w) wanaosaidiana kuendesha nidhamu ya ulimwengu.
Kuna aina kuu nne za shirk:-



l.shirk katika Dhati ya Allah (s.w).



2.Shirk katika sifa za Allah (s.w).



3.Shirk katika Hukumu za Allah (s.w)



4.Shirk katika Mamlaka ya Allah (s.w).



Shirk katika Dhati ya Allah (s.w)
Kumshirikisha Allah (s.w) katika dhati yake ni kuchukua vitu au viumbe kama vile masanamu, hirizi, majabali, moto, ngombe, binadamu, n.k. na kuvinasabisha na Uungu na kuvielekea kwa unyenyekevu kwa kuviomba na kuvitegemea kama anavyostahiki kuombwa na kutegemewa Allah (s.w).



Shirk katika Sifa za Allah (s.w)
Kumshirikisha Allah (s.w) katika sifa zake ni kukinasibisha au kukipachika kiumbe chochote sifa anazostahiki kusifiwa kwazo Allah (s.w) pekee au kundunisha Allah (s.w) kwa kumfananisha na viumbe vyake. Hata kumsifu Mtume kupitakiasi ni shirk kama tunavyotahadharishwa katika hadith ifuatayo: “Imepokelewa kutoka kwa Umar (r.a) kuwa, Mtume (s.a.w) amesema: Msizidishe katika kunisifu kama w alivyozidisha Wakristo (Manasara) katika kumsifu m w an a w a Ma ry am (Is a (a. s). Mim i n i mja w a Allah tu kwa hiyo niiteni: “Mja wa Allah na Mtume wake” (Sahihi Bukhari).
Pia Waislam wanakatazwa kujisifu na kujitukuza au kuwasifu na kuwatukuza wengine kiasi cha kukiuka mipaka ya Allah (s.w) katika aya ifuatayo:“... Yeye ndiye anayekujueni sana tangu alipokuumbeni katika ardhi na mlipokuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msizitakase (msizisifu) nafsi zenu, yeye anamjua sana aliyetakasika. ” (53:32)
Waumini wa kweli pia wanatarajiwa wawe ni wenye kumtegemea Allah (s.w) pekee kwa kila jambo wan alolihitajia na kuomba moja kwa moja msaada wake, Baraka, Rehema zake, Msamaha wake n.k kwa kutumia sifa zake (majina yake) zinazolandana na yale tuyaombayo:“Sema; mwombeni (Allah) kwa jina la Allah au muombeni (kwa jina la) Rahman, kwa jina lolote mnalomwita (katika haya itafaa); kwani ana majina mazuri mazuri..” (17:110)



Shirk katika Hukumu za Allah (s.w)
Kumshirikisha Allah (s.w) katika hukumu zake ni kutoa hukumu kinyume na alivyohukumu Allah (s.w) juu ya masuala mbali mbali. Kwa mfano Allah (s.w) anahukumu kuwa adhabu ya mwizi ni kukatwa kiganja chake cha mkono wa kulia; wazinifu wachapwe viboko mia, n.k. Pakitokea sheria inayotoa hukumu kinyume na Allah (s.w), itakuwa imemshirikisha Allah (s.w) katika hukumu zake. Inasisitizwa katika Qur-an kuwa wale wasiohukumu kwa kufuata sheria ya Allah (s.w) ni Makafiri, Madhalimu na Mafaasiq.


“... Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio Makafiri.” (5:44)


“... Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio Madhalimu.” (5:45)


“... Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio Mafaasiq.” (5:47)



Shirk katika Mamlaka (Uongozi wa) ya Allah (s.w)
Allah (s.w) ndiye aliyemuumba mwanaadamu kwa lengo na ndiye mwenye haki pekee ya kumuwekea mwanaadamu sharia na mwongozo wa maisha. Akitokea mtu au kikundi cha watu kuchukua jukumu la kumtungia mwanaadamu sheria kinyume na ile ya Allah na kumtaka atii sheria hiyo ni kuchukua nafasi ya Allah (s.w). Hivyo atakayewaamrisha watu wamtii


kinyume na sharia ya Allah (s.w) au atakaye waamrisha watu waishi kinyume na mwongozo wa Allah (s.w) atakuwa amechukua nafasi ya Uungu. Mayahudi na Wakristo wameshutumiwa katika Qur-an:


“Wamewafanya wanazuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu...” (9:31)
Mtume (s.a.w) katika kufafanua aya hii ameeleza kuwa kuwafanya wanazuoni au viongozi wengine kuwa mungu badala ya Allah (s.w) ni kuwatii kinyume na sharia ya Allah (s.w). Hivyo kukitii kiumbe chochote kinyume na utii kwa Allah (s.w) ni kukifanya kiumbe hicho mungu.
Kina cha Uovu wa Shirk
Shirk ni dhambi kubwa kuliko zote kama tunavyofahamishwa katika Qur-an:


“Hakika Allah hasamehi (dhambi ya) kushirikishw a na kitu na husamehe yasiyo haya kwa amtakaye. Na anayemshirikisha Allah bila shaka amebuni dhambi kubwa. ” (4:48)


“Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi (dhambi ya) kushirikishwa na kitu na husamehe yasiyokuwa haya kw a amtakaye. Na anayemshirikisha Allah bila shaka yeye amepotea upotofu ulio mbali.” (4:116)


Dhambi ya shirk hufuta mema yote aliyoyatenda mja kabla ya kushirikisha.


“Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa wale waliokuwa kabla yako,kuwa “kama ukimshirikisha (Allah) bila shaka amali zako zitaruka patupu, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye khasara” (39:65)
* *** *** *** *** *** * *




                   







           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 963


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Kujiepusha na kuua nafsi bila ya Haki
Kuua nafsi bila ya Haki, ni kuiua nafsi isiyo na kosa linalostahiki hukumu ya kifo. Soma Zaidi...

Mtazamo wa uislamu juu ya dini
Kwenye kipengele hichi tutajifunza mitazamo ya kikafiri juu ya dini. Soma Zaidi...

Kumuamini malaika wa mwenyezi Mungu...
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

mwanadamu hawezi kuishi bila ya Dini
Soma Zaidi...

Kujiepusha na Kibri na Majivuno
Soma Zaidi...

Upeo wa Elimu waliyokuwa nayo Mitume
Soma Zaidi...

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat at-Tawbah
Mwenyezi Mungu amekuwia radhi (amekusamehe). Soma Zaidi...

Kutowatii Wazazi katika kumuasi Allah (s.w)
"Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu Soma Zaidi...

Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika surat Hashir
Huwaoni wale wanafiki wanawaambia ndugu zao walio makafiri miongoni mwa watu waliopewa Kitabu (kabla yenu) Mayahudi (Wanawaambia): "Kama mkitolewa, (mkifukuzwa hapa) tutaondoka pamoja nanyi, wala hat utamtii yoyote kabisa juu yenu. Soma Zaidi...

Kwa nini uislamu umeipa elimu nafasi ya kwanza
Elimu imepewa nafasi kubwa sana katika uislamu. Soma Zaidi...

Mgawanyiko wa elimu usiokubalika katika uislamu
Ni mgawanyo upi wa elimu haukubaliki. Ni ipi elimul akhera na elimu dunia? (Edk form 1 Dhana ya elimu) Soma Zaidi...

Kuongea na Allah (s.w) nyuma ya Pazia
Hii ni njia ambayo mwanaadamu huongeleshwa moja kwa moja na Allah (s. Soma Zaidi...