image

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat As-Sajida

Nao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya?

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat As-Sajida

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat As-SajidaNao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya?" (Ndio).Bali wao hawakiri kwamba watakutana na Mola wao! Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti aliyewakilishwa kwenu, kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu." (32:10-11)Na ungaliwaona waovu wakiinamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao, (na kusema) "Mola wetu! Tumekwisha kuona na tumekwisha kusikia, basi turudishe, tutafanya vitendo vizuri; hakika (sasa) tumeyakinisha." Na Tungalitaka Tungempa kila mtu uwongofu wake, lakini imehakikika kauli iliyotoka Kwangu: Kwa yakini Nitaijaza Jahannamu kwa wote hawa; majini na watu (ambao ni wabaya).(32:12-13)


Basi ionjeni (adhabu) kwa sababu ya kusahau makutano ya siku yenu hii; na Sisi Tutakusahauni (Motoni), na onjeni adhabu idumuyo kwa yale mliyokuwa mkiyatenda. Hakika wanaoziamini aya Zetu ni wale tu ambao wanapokumbushwa huanguka kusujudu na humtukuza Mola wao kwa sifa Zake, nao hawatakabari. (32:14-1 5)


Huinua mbavu zao kutoka vitandani wakati wa usiku ili kumuabudu Mola wao kwa kuogopa Moto na kutaraji Pepo; na hutoa (zaka na sadaka) katika yale tuliyowapa. Nafsi yoyote haijui yaliyofichiwa katika hayo yanayofurahisha macho (huko Peponi): ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyafanya. (32:16-17)


Je! Mwislamu kamili atakuwa sawa na yule aliye fasiki? Hawawi sawa. Wale walioamini na wakafanya vitendo vizuri watakuwa na Mabustani ya makazi mazuri. Ni andao lao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda. (32:18-1 9)


Na wale waliofanya uovu, makazi yao ni Motoni, watakapotaka kutoka humo watarudishwa mumo humo na wataambiwa: "Onjeni tu adhabu ya Moto ambayo mlikuwa mkiikadhibisha." (32:20)Mafunzo
Mafunzo tuyapatayo kutokana na aya hizi ni kuwa:
Kwanza,
makafiri kwa kuzugwa na maisha ya dunia huacha kutumia akili zao na vipawa vyao vya tafakuri walivyotunukiwa na Allah (s.w) na kujitia upofu, uziwi na ububu kuwa dunia hii haina muumba na kuwa binaadamu hatarejeshwa kwa Muumba huyo na kuulizwa juu ya matendo yake yote aliyoyafanya katika mgongo huu wa ardhi. Hivyo kwa dhana yao hii makafiri huishi kwa jeuri katika ardhi na kufisidi watakavyo. Ni kutokana na tabia yao hii Allah (s.w) amewaandalia adhabu kali ya moto kama tu navyoj ifu nza katika aya ifuatayo:"Na bila shaka tumewaumbia moto wa Jahannamu wengi katika majini na wanaadamu (kwa sababu hii). Nyoyo wanazo, lakini hawafahamu kwazo (hawataki kufahamu kwazo) na macho wanayo, lakini hawaoni kwayo na masikio wanayo lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika." (7:1 79)Pili, Makafiri pamoja na kukanusha kwao kuwepo kwa Allah (s.w) na Siku ya Mwisho, watakapofishwa na kurejeshwa mbele ya Mola wao, ukweli utadhihiri na uongo utajitenga na watayakinisha kuwa wao walikuwa waovu. Hivyo watajuta juu ya uovu wao na watamuomba Mola wao, awarudishe tena duniani ili wawe waumini watenda mema. Haya ni majuto yasiyo na manufaa, kwani walitahadharishwa juu ya maisha ya Akhera lakini walikanusha na kufanya maskhara:


"Na husema:Je, tutakapopotea katika ardhi (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya? (Ndio) Bali wao hawakiri kwamba watakutana na mola wao!" (32:10).Tatu, Allah (s.w) hatakuwa anawadhulumu makafiri atakapowaadhibu, bali watakuwa wamejidhulumu wenyewe nafsi zao. Allah (s.w) aliwaumba na kuwapa akili na uhuru wa kuchagua maisha yakuwa Muumini au Kafiri baada ya kufahamishwa wazi kuwa waumini wataishi maisha ya nuru hapa duniani na kulipwa neema za Peponi huko akhera na kuwa makafiri wataishi maisha ya gizani hapa duniani na kustahiki adhabu kali ya motoni huko akhera kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:


"Yeye (Allah) ndiye aliyekuumbeni (nyote). Na kuna wengine wenu ni makafiri na wengine wenu ni waumini. Na Allah anayaona (yote) mnayoyafanya." (64:2)


"Allah ni mlinzi (kiongozi) wa wale walioamini. Huwatoa katika giza na kuwaingiza katika nuru. Lakini waliokufuru walinzi (viongozi) wao ni matwaghuti (mashetani). Huwatoa katika nuru na kuwaingiza katika giza. Hao ndio watu wa motoni humo watakaa milele." (2:25 7)Nne, Tofauti na makafiri ambao hungojea kujuta kwa makosa yao pale watakapoona adhabu ya Allah(s.w) huko akhera, waumini siku zote na nyakati zote katika maisha yao hapa duniani huhofia ghadhabu za Allah (s.w) na kujitahidi kumuelekea Mola wao katika sura hii sifa za waumini zimeorodheshwa kama ifuatavyo:(i)Wanapokumbushwa kwa aya za Allah(s.w) hunyenyekea kwa kusujudu. Kiutendaji inamaana kuwa waumini wanapopewa maagizo na Mola wao humtii mara moja na kuingia katika utendaji.
(ii)Humtukuza Mola wao kwa kutaja sifa zake (tukufu) na hawatakabari.
(iii)Huinua mbavu zao kutoka vitandani wakati wa usiku (wa manane) ili kumuabudu Mola wao kwa kuswali (Qiyamullayl) kwa kuogopa moto na kutaraji pepo.
(iv) Hutoa katika yale aliyo waruzuku Mola wao kwa ajili ya kusimamisha Uislamu na kuwahurumia wanaadamu wenziwao.
Pamoja na waumini kufanya haya na mema mengineyo, daima huomba dua ifuatayo:


" Mola wetu! Tuondolee adhabu ya Jahannamu, bila shaka adhabu yake ni yenye kuendelea. Hakika hiyo (Jahannamu) nikituo kibaya na mahali (pabaya kabisa)pakukaa” (25:65-66)Tano, Waumini wa kweli (Waislamu kamili) ni bora kuliko watu wengine wote kwa sababu ndio pekee kwa kufuata mwongozo wa Allah (s.w) wanaoweza kuiongoza jamii kwa haki na uadilifu na kuleta furaha na amani ya kweli katika jamii..Sita, Dhalimu mkubwa kuliko madhalimu wote ni yule anayekumbushwa aya za Mola wake kisha akazikataa. Kukataa aya za Allah (s.w) si lazima utamke kuwa umezikataa bali kutozitekeleza kwa makusudi ndio hasa kuzikataa. Hivyo, wale tunaojiita waumini lakini tunaendesha maisha yetu kinyume na aya za Allah (s.w), tujue kuwa tu madhalimu wakubwa kama wale walioikanusha Qur-an kwa uwazi na Mtume (s.a.w) akalalamika juu yao:


Na Mtume alikuwa akisema: "Ee, Mola wangu! Hakika watu wangu wameifanya Qur-an hii kuwa ni kitu kilichohamwa. (25:30)


Kuihama Qur-an ni kutoisoma kwa mazingatio na kutoiingiza katika utendaji wa maisha ya kila siku.
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 276


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Nafsi ya mwanaadamu
Soma Zaidi...

Maana ya Kuamini Mitume wa Allah (s.w) katika maisha ya kila s iku.
Waumini wa kweli wa Mitume wa Allah (s. Soma Zaidi...

SHIRK
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Kutopupia dunia
"Ewe mwanangu! Soma Zaidi...

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat at-Tawbah
Mwenyezi Mungu amekuwia radhi (amekusamehe). Soma Zaidi...

Kumuamini malaika wa mwenyezi Mungu...
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Upeo wa Elimu waliyokuwa nayo Mitume
Soma Zaidi...

Lengo la ibada maalumu
Lengo la ibada maalumu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Athari za kumuamini mwenyezi Mungu katika maisha ya kila siku
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Maisha ya Mitume
Soma Zaidi...

“Allah (s.w) humwingiza katika rahma zake amtakaye na kumwacha kupotea amtakaye”
Soma Zaidi...

Ni haramu kwa Waumini kuwaoa au kuolewa na Wazinifu, Washirikina na Mahabithi
Soma Zaidi...