Tawhiid


image


Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)


  • Tawhiid.
  • Kimaana:  Ni Umoja au Upweke wa Mwenyezi Mungu (s.w).
  • Kimatumizi:   Ni fikra, mtazamo wa kimapinduzi katika kumkomboa

mwanaadamu na aina zote za utumwa wa kibinaadamu na kuwa   mtumishi huru wa Muumba wake.  


 

  • Aina za Tawhiid.

Kuna aina kuu tatu za Tawhiid kama zilivyoainishwa katika aya za Qur’an.

 

(i)  Tawhid Al-Uluuhiyyah – Upweke wa Allah (s.w) katika Uungu wake.

Nayo ni Kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) katika Uungu wake kwa kutokuwa na mungu mwingine yeyote wa kumuelekea kwa ibada au maombi isipokuwa yeye peke yake.

Rejea Qur’an (2:163), (3:62) na (112:1-4).

 

   (ii)  Tawhiid Al-Asmaa Wassifaat – Upweke wa Mwenyezi Mungu (s.w) katika Majina     

                                                                 na Sifa.

Nayo ni kutomsifu Mwenyezi Mungu (s.w) kwa sifa za viumbe au majina ya viumbe na pia kutomsifu kiumbe yeyote kwa sifa za Mwenyezi Mungu (s.w).

Rejea Qur’an (57:1-6) na (59:22-24).

 

 (iii) Tawhiid Rabbuubiyya – Upweke wa Mwenyezi Mungu (s.w) katika Ubwana,Utawala 

                                                   na Mamlaka Yake.  

Kumpwekesha Allah (s.w) katika Ubwana na Utawala wake ni kutofuata na sheria na taratibu za maisha kinyume na zile alizoziweka yeye kwa kumfanya ndiye Mlezi, Mlinzi, Mwendeshaji wa kila kitu.

Rejea Qur’an (4:59), (31:14-15), (25:52), (3:149), (3:100) na (5:57).



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani offline       ðŸ‘‰    3 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    4 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Nguzo za uislamu
Katika kipengele hiki tutajifunza nguzo za uislamu.aina tano za nguzo za uislamu,dhana ya nguzo za uislamu,lengo na umuhimu wa nguzo za uislamu Soma Zaidi...

image Mji wa Makkah na kabila la kiqureish
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Sababu za Quran kuwa mwongozo sahihi wa maisha ya mwanadamu
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mtazamo wa uislamh juu ya ibada
Katika kipengele hich tutajifunza dhana ya ibada katika uislamu,maana ua ibada Soma Zaidi...

image Kumuamini malaika wa mwenyezi Mungu...
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Miiko au Mambo yanayoharibu/kubatilisha funga
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mtazamo wa uislamu juu ya dini
Kwenye kipengele hichi tutajifunza mitazamo ya kikafiri juu ya dini. Soma Zaidi...

image Kumuamini malaika wa mwenyezi Mungu
Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu
Ni upi mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu (EDK form 1: mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu Soma Zaidi...

image Matendo ya hijjah na umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...