Kuwa wenye shukurani mbele ya Allah (s.w)
Mwanaadamu ametunukiwa neema mbali mbali na Mola wake kuliko viumbe wengine wote kama tuanvyojifunza katika aya mbali mbali za Qur'an.
(a) Kuwa wenye shukurani mbele ya Allah (s.w)
Mwanaadamu ametunukiwa neema mbali mbali na Mola wake kuliko viumbe wengine wote kama tuanvyojifunza katika aya mbali mbali za Qur'an.
"Na hakika tumewatukuza wanaadamu na tumewapa vya kupanda barani na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewatukuza kuliko wengi katika wale tuliowaumba, kwa utukufu ulio mkubwa (kabisa)." (17: 70)
βBila shaka tumemuumba mwanaadamu kwa umbo lililo bora kabisa." (95:4) Pamoja na neema zilizoainishwa kwa upeo mpana katika aya (17:70),
Mwanaadamu ameboreshwa kuliko viumbe wengine kwa kutunukiwa vipawa vya ziada vifuatavyo:
1. Akili inayomuwezesha kufikiri na kutafakari
2. Utambuzi wa ubinafsi unaomuwezesha kujitambua, kuyatambua mazingira yake na mahusiano yake na muumba na vile vyote Alivyoviumba
3. Kipawa cha elimu - uwezo wa kujielimisha na kuelimisha wengine.
4. Uhuru wa kuamua na kutenda.
Neema zote hizi ametunukiwa binaadamu ili aweze kufikia lengo la kuumbwa kwake ambalo ni kumuabudu Allah (s.w) katika kila kipengele cha maisha yake (Qur'an 51:56) na kisha kuwa Khalifa katika jamii. Hivyo, binaadamu atakuwa ni mwenye kumshukuru Allah (s.w) iwapo atamuabudu Allah (s.w) ipasavyo katika kila kipengele cha maisha yake na atakuwa ni mwizi wa fadhila endapo atatakabari na kuwaabudu wengine kinyume na Allah (s.w).
Anaye shukuru kwa kumuabudu Allah (s.w) ipasavyo anafanya hivyo kwa faida ya nafsi yake ya kuishi kwa furaha na amani katika maisha ya hapa duniani na kupata maisha bora zaidi huko akhera. Anayekufuru kwa kuacha kumuabudu Allah (s.w) iipasavyo, anaitia khasarani nafsi yake mwenyewe kwa kuishi maisha ya mashaka na khofu hapa duniani na kustahiki adhabu kali isiyo na mfano wake katika maisha ya akhera. Allah (s.w) hafaidiki kwa chochote kutokana na kushukuru kwetu na pia hapungu kiwi na chochote kutokana na kukufuru kwetu. Allah (s.w) ameliweka hili wazi mara tu baada ya kutufahamisha lengo la kuumbwa kwetu.
"Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu. Sitaki kwao riziki wala Sitaki wanilishe. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ndiye Mtoaji wa riziki, Mwenye nguvu, Madhubuti". (51:56-58).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Dua za Mitume na Manabii π2 Kitabu cha Afya π3 Bongolite - Game zone - Play free game π4 Madrasa kiganjani π5 Simulizi za Hadithi Audio π6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Kwa nini Elimu imepewa nafasi ya kwanza katika Uislamu?
Kwa nini katika uislamu elimu imepewa nafasi ya kwanza ( EDK form 1 Dahana ya elimu)
Soma Zaidi...Neema za Allah(s.w) Juu ya Bani Israil
Katika Qur'an tunakumbushwa neema mbali mbali walizotunukiwa Bani Israil (Mayahudi) na Mola wao ili kuwawezesha kusimamisha Ufalme wa Allah(s.
Soma Zaidi...Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu
Njia ambazo Allah hutumia kuwasiliana na wanadamu nakuwafundisha elimu mbalimbali. (Edk form 1 dhana ya Elimu)
Soma Zaidi...Kutowatii Wazazi katika kumuasi Allah (s.w)
"Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu
Soma Zaidi...