(c)Kuwafanyia Wema WazaziAllah (s.w) anatuusia kuwafanyia wema wazazi wawili na hasa kuzidisha wema zaidi kwa mama kwa sababu za msingi ambazo Allah (s.w) mwenyewe anatukumbusha.“….. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na (kumnyonyesha na kuja) kumwachisha kunyonya katika miaka miwili….. " (31:14).


“…..Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu na akamzaa kwa taabu. Na kubeba mimba yake hata kumwachisha ziwa (uchache wake) ni miezi thelathini (3 0) …." (46:15).Namna ya kuwafanyia wema wazazi kumefafanuliwa vyema katika mafunzo ya Surat Bani Israil tuliyoyapitia nyuma.