Kuamini Qadar ya Allah (s.w)
Kwa mujibu wa Hadith iliyosimuliwa na Umar (r.a), kuamini Qadar ni nguzo ya sita ya Imani ya Kiislamu. Katika hadithi hii ndefu, Umar (r.a) anasimulia:
Siku moja tulipokuwa tumeketi pamoja na Mtume (s.a.w) alitutokea mtu mmoja ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe kama theluji na nywele zake nyeusi sana, hakuwa na dalili zozote za msafiri, ingawa alikuwa mgeni kwetu sote. Halafu alikaa mbele ya Mtume hali magoti yake yakikabiliana na yale ya Mtume na akaweka mikono yake katika mapaja ya Mtume halafu akasema: “Ewe Muhammad nifahamishe juu ya Uislamu ” na Mtume akasema: “Ni kushuhudia kuwa hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah, kusimamisha Swala, Kutoa Zakat, Kufunga mwezi wa Ramadhani na Kuhiji Makkah kwa mwenye kuweza ” Halafu yule mgeni akasema: “Umesema kweli”. Tulistajaabu kwa nini aliuliza halafu akasadikisha. Halafu akasema: “Nifahamishe juu ya Imani”. Mtume akasema: “Ni Kumuamini Allah, Malaika Wake, Vitabu vyake, Mitume Wake, Siku ya Mwisho na Qadar, Kheri yake na Shari yake”. Kisha akasema: “Nifahamishe juu ya Ihsan”. Na Mtume akamjibu:“Ni kumuabudu Allah kama kwamba unamuona, kwani ingawa humuoni, Yeye anakuona ”. Halafu akasema: “Nifahamishe juu ya Siku ya Kiyama”. Mtume akamjibu kwamba hajui mwenye kuulizwa zaidi ya mwenye kuuliza Akasema: “Nifahamishe dalili zake”.Mtume. Akasema: “Ni wakati ambao mjakazi atamzaa bibi yake, na utakapoona wachungaji maskini, wenye nguo zilizoraruka na wasio na viatu wanashindana kujenga maghorofa”.Yule mgeni alipoondoka, Mtume alikaa kimya kwa muda halafu akasema: “Ee Umar, unamfahamu muulizaji? ” Sote tukajibu kuw a Allah na Mtume wake ndio w ajuao. Mtume akasema: “Huyo ni Jibril, amekuja kuw afundisheni dini yenu ”. (Muslim)
Maana ya Qadar
Neno “Al-Qadar” limetumika katika Qur-an kwa maana ya “kiasi”, kipimo”, kukadiria kipimo maalumu”. Hebu turejee aya zifuatazo ambamo neno Qadar limetumiwa:
“Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kiasi (chake makhsusi)” (54:49).
“... Na (Mwenyezi Mungu) Ameumba kila kitu na Akakikadiria kipim o (chake)” (25:2)
“Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa (mwembamba) kama chaparare la mtende kuu kuu”. (36:39).
Tukizingatia aya hizi, tunajifunza kuwa Allah(s.w) ameumba ulimwengu huu na vyote vilivyomo kwa mujibu wa kanuni zinazotawala mzunguko wa jua, mwezi, nyota, dunia na sayari nyingine. Kutokana na mizunguko ya jua, mwezi na dunia tunapata urefu wa mchana na usiku, hesabu ya miezi, majira, n.k. Kuna kanuni zinazotawala ukuaji wa mimea. Kutokana na kanuni hizo, mimea huzaa matunda yenye rangi na ladha mbali mbali.Kwa ujumla Allah (s.w) ameumba kila kitu kwa lengo, maalumu na ameweka kanuni madhubuti zinazokiwezesha kila kiumbe kifikie lengo lake kama anavyotukumbu sha katika Qur-an:
“Litukuze jina la Mola w ako aliye Mtukufu. Aliyeumba (kila kitu) akakitengeneza. Na akakikadiria (kila kimoja jambo lake) na akakiongoza (kufanya jambo hilo). (87:1-3)
Pia matukio yote yako katika Qadar ya Allah (s.w). Hapana tukio lolote linalotokea liwe la kheri au la shari kwa mwanaadamu, ila limo katika Qadar ya Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika Qur-an:
Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni kwa udongo, kisha kwa tone la manii, kisha akakufanyeni wanaume na wanawake. Na mwanamke yoyote hachukui mimba wala hazai ila kwa ilimu Yake (Mwenyezi Mungu). Na mwenye kupewa umri hapewi umri (zaidi) wala hapunguziwi umri wake ila yamo hayo katika Kitabu (cha Mw enyezi Mungu). Bila shaka (kuyapitisha) haya ni sahali kwa Mwenyezi Mungu. (35:11)
Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu
ila umekwishaandikwa katika Kitabu (cha Mwenyezi Mungu) kabla Hatujauumba. Kwa yakini hilo ni sahali kwa Mwenyezi Mungu. (57:22)
Mtazamo wa Uislamu juu ya Qadar
Kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu, ni makosa makubwa kudhani kuwa mtu anaweza kufanya jambo lolote lile kinyume na Qadar ya Allah (s.w). Na ni makosa makubwa pia kudhani kuwa mtu anaweza kumlaumu Allah (s.w) kwa maovu anayotenda. Utatanishi wote wanaoupata watu juu ya suala hili unaondoka kwa sababu Uislamu umegawanya maisha ya binaadamu katika maeneo makuu mawili:
(a)Eneo ambalo binaadamu hana hiari, na
(b)Eneo ambalo binaadamu anao uchaguzi.
Binaadamu hana hiari kabisa katika baadhi ya mambo katika maisha yake. Mambo hayo humtokea atake asitake. Hana uwezo wa kuyachagua wala kuyabadilisha. Kwa mfano mtu hana hiari ya kuwachagua wazazi wake. Hawezi kuchagua tarehe ya kuzaliwa wala nchi atakayozaliwa. Hawezi kuchagu a rangi ya ngozi yake wala aina ya nywele, rangi ya macho, kimo au vipawa vingine.
Damu itazunguka mwilini bila kuipangia yeye safari hiyo, moyo wake utadunda bila yeye kuuamrisha. Mwili mzima wa binaadamu unafanya kazi bila yeye kuupigia kura. Kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu binaadamu hataulizwa au kuhisabiwa juu ya jambo lolote ambalo yeye hakuwa na hiari nalo. Yaani hakuna mtu atakayeulizwa kwanini wewe ulizaliwa siku ya Jumanne badala ya Jumatano? Au kwa nini ulifariki mwezi wa Shaabani badala ya kusubiri hadi mwezi wa Ramadhani? Au kwanini ulikuwa mrefu namna hii badala ya kuwa na kimo cha wastani? Kwa hakika ni rehema kubwa ya Allah (s.w) kwamba mambo hayo hatuyadhibiti sisi wenyewe.
Hebu fikiria kama moyo ungelikuwa unapiga kwa amri yetu, tungeliwazaje kulihakikisha hilo tunapolala usingizini au tunaposahau? Matatizo yangekuwa hayo hayo lau myeyusho wa chakula (digestion) ungelikuwa uko chini ya udhibiti wetu, n.k.
Kuna eneo ambalo binaadamu anao uhuru wa kuchagua hili au lile. Mtu anaweza kwa mfano kuchukua bastola na kumuulia mtu mwingine na kupora mali yake au anaweza kuchukua chakula na kumpa mwenye njaa. Mtu anaweza kutumia pesa zake kwa kuwanunulia nguo wazazi wake, au anaweza kwenda nazo kilabuni kunywea pombe. Mtu anaweza kumuamini Allah (s.w) na kumtii na anaweza kukataa kumuamini na akaamua kumuasi. Mtu anaweza kusema kweli au akiamua anaweza kusema uwongo. Anaweza kumtendea mwenziwe haki au anaweza kumdhulumu. Katika eneo hili binaadamu ni Mas-uli, yaani atahisabiwa na Allah (s.w) kwa yote aliyoyafanya kwani ni mambo ambayo binaadamu amepewa uhuru wa kuchagua kutenda hili au lile.
“Hakika Sisi Tumem uongoa, (tumembainishia) njia. Basi atakuwa mwenye shukurani au mwenye kukufuru ”. (76:3)
“Na sema: Huu ni ukweli uliotoka kwa Mola wenu, basi anayetaka naamini na anayetaka na akufuru.” (18:29)
“Je, hatukumpa (binaadamu) macho mawili? Na ulimi na midomo miwili? Na tukambainishia zote njia mbili?” (90:8-10)
Hivyo ni dhahiri kuwa katika eneo hili binaadamu hajapangiwa na Allah (s.w) lipi aje kulifanya atake asitake. Allah (s.w) amempa mwongozo wa kuufuata lakini kampa na hiari ya kuufuata au kuuacha. Na ndio maana ataulizwa. Ukweli kuwa watu wanaweza kumuasi Allah (s.w) ni ushahidi tosha kuwa watu
wanao uhuru wa kuchagua kutenda mema au maovu, kwani lau si hivyo watu wote wangekuwa kama Malaika.
Hata hivyo, kwanza, isidhaniwe kuwa maadamu watu wanao uhuru wa kuchagua kutenda lolote basi Allah (s.w) hajui mpaka jambo hilo litokee. Yeye anayajua yote atakayofanya mja hadi hatima yake ya mwisho siku ya kiyama hata kabla mtu huyo hajazaliwa.
“Na hakuna mnyama yeyote (kiumbe chochote) katika ardhi ila riziki yake iko juu ya Mwenyezi Mungu. Na anajua makao yake ya milele na mahali pake pa kupita tu (hapa duniani). Yote yamo katika kitabu kinachodhihirisha (kila kitu).” (11:6).
Allah (s.w) anayajua atakayoyachagua mtu kuyafanya lakini hakumshurutisha kuyafanya.
Pili, isidhaniwe pia kuwa maadamu mtu amechagua kumuasi Allah (s.w), basi mtu huyo anapotenda uovu huo Allah (s.w) huchukia lakini hana uwezo wa kumzuia. Mtu hawezi kufanya lolote ila kwa idhini ya Allah (s.w). Yaani mtu anaweza tu kutenda jema au ovu kwa sababu ya kutumia vizuri au vibaya neema alizopewa na Allah (s.w). Kwa mfano tusema mtu amekusudia kwenda kuswali Ijumaa lakini kabla hajaondoka Allah (s.w) akamnyang’anya mtu huyo neema ya akili au fahamu, au akakosa nguvu hata za kukaa, ni dhahiri kuwa hataweza kuswali Ijumaa. Na hivyo hivyo kwa mtu aliyekusudia kwenda kuvunja duka na kupora mali kabla ya kufanya hivyo akavunjika mgongo au akatiwa upofu machoni, ni dhahiri kuwa hawezi kutenda lile alilolikusudia. Hivyo mema au maovu hayatendeki kinyume na uwezo wa Allah (s.w).
Suala la Uongofu
Badhi ya watu hujiuliza: Kama sote tuna fursa sawa sawa ya kuchagua kutenda mema au maovu mbona Qur-an yasema 273
Mwenyezi Mungu humuongoza amtakaye na humuacha kupotea am t a k aye?
Uongofu utokao kwa Mwenyezi Mungu uko wa namna mbili: Kwanza uongofu kwa maana ya kumfahamisha mtu njia sahihi ya kufuata. Na pili uongofu kwa maana ya msaada utokao kwa Mwenyezi Mungu.
Uongofu kwa maana ya kwanza, yaani kujulishwa njia ya heri na ya shari, na kujulishwa jambo lipi mtu atende na lipi aliwache, ni uongofu ambao kila mtu anaupata. Na uongofu huo ni wa namna tatu kwanza ni: fitra, yaani kupandikizwa uongofu katika nafsi yake mtu:
Na kwa nafsi na aliyeitengeneza.Kisha akaifahamisha uovu wake na wema. (91:7-8)
Na uongofu wa namna ya pili ni kipawa cha akili, ambacho kinaweza kutumika kuisadikisha imani. Na namna ya tatu ni uongofu aliopewa binaadamu kwa kupitia Mitume na Vitabu vya Mwenyezi Mungu. Hivyo kila mtu amepata uongofu kutoka kwa Mwenyezi Mungu angalau kwa njia mbili za mwanzo.
Uongofu kwa maana ya msaada wanaupata wale tu wanaoamua kuufuata kikweli kweli ule uongofu waliopewa. Tuseme mathalan mtu fulani amepotea mjini au hajui njia ya kwenda mahali fulani akaamua kumuuliza askari: Baada ya kumuelekeza mtu yule aliyepotea aseme: Sikuamini, mwongo mkubwa wee!! Askari atamwambia: Sawa fuata njia unayoijua. Lakini iwapo mtu aliyepotea baada ya kuelekezwa atasema: Ahsante sana kwa kunielekeza nafikiri nitafika ninakokusudia, askari anaweza kumwambia: Subiri kidogo mimi nakwenda huko huko nitakupeleka hadi unapokwenda. Huu ni mfano tu, na Mwenyezi Mungu hawezi kufananishwa na askari au kiumbe yeyote.Kusudio hapa ni kuonesha kuwa watu wanaofuata muongozo wa Mwenyezi Mungu huzidishiwa uongofu:
Na wale wanaokubali kuongoka anawazidishia uongofu na anawapa (jaza) ya ucha Mungu wao. (47:17)
Sisi tunakusimulia habari zao kwa kweli. Hakika wao walikuwa ni vijana waliomuamini Mola wao Nasi tukawazidisha uongofu.(18:13)
Ili kuweka wazi zaidi uongofu wa aina hii ya pili hebu tuizingatie kwa makini aya aifuatayo:
Hakika wale walioamini na kufanya vitendo vizuri, Mola wao atawaongoza kwa sababu ya imani yao (wende katika Pepo) Itakuwa inapita mito mbele yao katika mabustani yenye neema. (10:9).