image

Hijabu na kujikinga na zinaa

Hijabu na kujikinga na zinaa

(h) Hijabu na kujikinga na zinaa



Katika kutokomeza zinaa katika jamii, Uislamu hauanzii na kutoa adhabu kali ya kuwachapa wazinifu viboko 100 mbele ya hadhara au kuwapiga mawe mpaka wafe, bali umeanza na kukataza kuikurubia zinaa Qur'an (17:32) na kuweka mazingira yatakayopelekea kutoikurubia zinaa kwa kutoa maelekezo mbali mbali ya hijabu kama inavyodhihiri katika aya zifuatazo:


“Waambie Waislamu wanaume wainamishe macho yao (wasiangalie kwa jicho la matamanio), na wazilinde tupu zao, hili ni takaso kwao; bila shaka Mwenyezi Mungu Anazo habari za (yote) wanayoyafanya." (24:30)


"Na waambie Waislamu wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika (navyo ni uso na vitanga vya mikono - na wengine wanasema na nyayo). Na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao, na wasionyeshe mapambo yao ila kwa wanaume zao, au baba zao, au baba za waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenziwao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, (watumwa wao), au wafuasi wanaume wasio na matamanio (kwa wanawake) au watoto ambao hawajajua mambo yaliyohusu uke. Wala was ipige miguu yao ili yajulikane wanayoyaficha katika mapambo yao. Na tubieni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waislamu ili mpate kufaulu." (24:31)



"Enyi wake wa Mtume, nyinyi si kama yeyote tu katika wanawake wengine. (Nyinyi wakeze Mtume). Kama mnataka (kufanya jambo la ) kumcha Mwenyezi Mungu, basi msiregeze sauti (zenu mnaposema na wanaume) ili asitamani mtu mwenye ugonjwa moyoni mwake (kufanya mabaya na nyiye) na semeni maneno mazuri."
"Na kaeni majumbani mwenu, wala msionyeshe mapambo yenu kama walivyokuwa wakionyesha mapambo yao wanawake wa zama za ujahili na simamisheni Sala na toeni Zaka, na Mtiini Mwenyezi Mungu na mtume Wake. Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi watu wa nyumba (ya Mtume), na (anataka) kukutakaseni kabisa kabisa." (33:32-3 3)


"Ewe Mtume! Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiislamu wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya Hivyo kutapelekea upesi wajulikane (kuwa ni watu wa hishima ili) wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu." (33:59)


Kutokana na aya hizi tunapata maelekezo yafuatayo juu ya hijabu:
(i)Ili kuepukana na zinaa wanaume na wanawake wameamrishwa kuinamisha macho yao. Kui namisha macho ni msemo wenye maana ya kutowaangalia wanawake (kwa upande wa wanaume) au wanaume (kwa upande wa wanawake) kwa jicho la matamanio. Mara nyingi jicho la matamanio limekuwa ndio chanzo cha fitna baina ya mume na mke wasio maharimu, yaani walio ajinabi (wanaoweza kuoana).



(ii)Wanaume na wanawake pia wamehimizwa katika aya hizi kuwa wafanye jitihada za makusudi za kulinda tupu zao. Kulinda tupu ni kufanya jitihada za makusudi kujiepusha na maasia yote yanayosababishwa na utupu. Hili ni pamoja na kujiepusha na zinaa, ubasha, usagaji na kuchezea tupu ili kukidhi matashi ya ngono. Kukidhi matashi ya ngono ni halali tu ndani ya ndoa tena kwa kuliendea tendo hilo kama alivyoliruhusu Allah (s.w). Ubasha ni tendo ovu na haramu hata kwa mtu na mkewe. Wanawake ambao kimaumbile na kisaikolojia ni kivutio (attractive) cha wanaume wamepewa maelekezo zaidi ya Hijabu katika aya za (24:31), (33:32-33) na (33:59) kama ifuatavyo:



(iii)Wavae nguo inayofunika mwili mzima isipokuwa tu uso na viganja vya mikono (wengine wanasema na nyayo za miguu).
(iv)Wavae Shungi (jalabibi) iliyoshuka vizuri kiasi cha kufunika kifua mpaka kutovuni.
(v)Wavae vazi pana linaloshuka vizuri bila ya kubana kiasi cha kuonesha makunjo ya mwili.
(vi)Vazi la baibui au kanzu liwe na mikono mirefu yenye 211 vifungo karibu na viganja vya mikono ili isitokee mwanya wa vazi hilo kuvuka na kuiacha mikono uchi wakati wa kufanya shughuli mbalimbali.



(vii)Pamoja na wanawake kuruhusiwa kuvaa mapambo (kinyume na wanaume), hawaruhusiwi kudhihirisha mapambo yao ila kwa wale waliotajwa katika aya (24:31).



(viii)Wanawake hawaruhisiwi hata kudhihirisha sauti ya mapambo yao. Pia wanawake hawaruhisiwe kudhihirisha hata harufu na rangi ya vipodozi vyao. Wanaruhisiwa kujipodoa kwa mafuta na manukato butu (yasiyo na harufu kali). Ni haramu kwa wanawake kujipaka rangi za midomoni, kuchani, viganjani na kwingineko penye kud h ih irika.



(ix)Ikibidi wanawake waongee na wanaume wasio maharimu zao, wanalazimika kuzikaza sauti zao. Wanawake kulegeza sauti zao mbele ya wanaume wasio maharimu ni miongoni mwa vichocheo vya zinaa.



(x)Wanawake wamekatazwa kutoka ovyo majumbani mwao pasi na sababu za msingi. Na wakitoka kwa sababu za msingi wachunge miiko yote ya Hijabu iliyoelekezwa katika aya hizi pia wajiepushe na michanganyiko ya wanaume na wanawake isiyozingatia mipaka ya Uislamu. Ni haramu kwa mwanamume na mwanamke ajinabi kukaa faragha wakiwa wawili tu. Ikibidi wanaume na wanawake kukutana pamoja kwa ajili ya jambo la kheri wasiwe chini ya watu watatu.



Pamoja na maelekezo haya ya Hijabu, bado Uislamu umechukua hatua nyingine ya kuikinga jamii na zinaa na majanga yatokanayo kwa kuhalalisha na kuhimiza ndoa (rejea Qur'an 4:24, 5:5). Pia katika Hadithi ya 'Abdullah bin Mas'ud (r.a), Mtume (s.a.w) aliwausia vijana:


“Enyi kongamano la vijana! Na aoe yule aliye na uwezo miongoni mwenu, Hakika kuoa kunainamisha macho na asiyeweza kuoa na afunge; hakika funga hukata matamanio" (Bukhari na Muslim).



Wanawake wa Kiislamu pamoja na washauri wao (mawalii wao) wanashauriwa watoze mahari kidogo kulingana na hali ya muoaji mtarajiwa, ili kurahisisha ndoa.
Hivyo, katika majumuisho ya sehemu hii tunajifunza kuwa Uislamu unatokomeza zinaa katika jamii kwa kufuata hatua zifuatazo:



(1)Kuwakataza watu kuikurubia zinaa na kuonesha ubaya wa zinaa (Qur'an 17:32)
(2)Kutoa maeelekezo ya Hijabu kwa wanaume na wanawake ambayo yakitiiwa ipasavyo yanawawezesha watu kuepukana na zinaa.
(3)Kuhimiza ndoa ambayo ndiyo njia pekee iliyo nzuri katika kutosheleza matashi ya kimaumbile ya ngono.
(4)Kutoa adhabu kali kwa wazinifu ili iwe onyo kwao na kwa jamii nzi ma.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 408


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Kwa nini uislamu umeipa elimu nafasi ya kwanza
Elimu imepewa nafasi kubwa sana katika uislamu. Soma Zaidi...

Tawhiid
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kwa nini Elimu imepewa nafasi ya kwanza katika Uislamu?
Kwa nini katika uislamu elimu imepewa nafasi ya kwanza ( EDK form 1 Dahana ya elimu) Soma Zaidi...

NGUZO ZA IMANI
Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:1 Kumuamini Allah (s. Soma Zaidi...

Mtazamo wa uislamu juu ya Elimu, nini maana ya elimu na nani aliye elimika.
Ni nini maana ya Elimu na ni nani aliye elimika? Uislamu una mtazamo gani juu ya Elimu? Soma Zaidi...

Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu
Njia ambazo Allah hutumia kuwasiliana na wanadamu nakuwafundisha elimu mbalimbali. (Edk form 1 dhana ya Elimu) Soma Zaidi...

Maana ya Kumuamini Allah (s.w) katika Utendaji wa kila siku
Soma Zaidi...

Mgawanyiko wa Elimu katika mtazamo wa Uislamu
Katika Uislamu elimu imegawanyika katika Elimu ya muongozo na elimu ya mazingira. Soma Zaidi...

Kina Cha uovu wa shirk
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika Surat ahzab
Na waliposema wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, "Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu. Soma Zaidi...

Elimu Yenye Manufaa
Kwenye kipengele hiki tutajifunza elimu yenye manufaa kwenye jamii na pia tutajifunza sifa za elimu yenye manufaa. Soma Zaidi...

Maswali juu ya nguzo za Imani
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...