Mgawanyo wa Elimu Usiokubalika katika uislamu.

Mgawanyo wa Elimu Usiokubalika katika uislamu.

Kipengele hichi kinahusu mgawanyiko wa elimu usiokubalika katika uislamu.sababu za mgawanyiko wa elimu udio sahihi katika uislamu.

           Mgawanyo wa Elimu usiokubalika katika Uislamu (usio           sahihi).

 -    Katika Uislamu, HAKUNA mgawanyo wa ‘Elimu Dunia’ na ‘Elimu Akhera’.

 -  Mgawanyo huu ni potofu wenye dhana ya kikafiri kuwa kuna maisha ya Dini yanayoongozwa na Mwenyezi Mungu na maisha ya Dunia yanayoongozwa na binaadamu.

 

  1. Nabii Adam (a.s) aliandaliwa yeye na kizazi chake kuwa Makhalifa (viongozi) na alifundishwa majina (fani zote) ya vitu vyote.

Rejea Qur’an (2:31) na (2:38-39).

2. Amri ya kusoma aliyopewa Mtume (s.a.w) na umma wake haibagui elimu ya dini na dunia.

 

3.Muasisi wa (chanzo cha) elimu na fani zote ni Mwenyezi Mungu (s.w). Hakuna mwanaadamu aliyeasisi elimu au fani yeyote ila ni mwendelezaji tu.

Rejea Qur’an (96:3-5).

 

4.Pia Qur’an inatufahamisha kuwa wanaomcha Allah (s.w) ipasavyo ni waumini wataalamu waliozama katika fani mbali mbali za kumjua Allah (s.w), sio tu fani za kidini za Fiqh, Tawhiid, n.k.

Rejea Qur’an (35:27-28).

 

5.Katika Qur’an Allah (s.w) anatufahamisha kuwa waumini wenye elimu ya fani mbali mbali ndio wenye daraja kubwa zaidi mbele yake.

Rejea Qur’an (58:11), (49:13).

 

6.Hakuna mgawanyo wa elimu unaooneshwa katika Hadith za Mtume (s.a.w) zinazoelezea fani za elimu.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Views: 2424

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 web hosting     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 ai web app     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zinazofanana:

KUAMINI MITUME WA ALLAH (S.W)

Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya Mitume wa Allah (s.

Soma Zaidi...
ALAMA YA MUUMINI WA UKWELI KATIKA UISLAMU

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم قَالَ: "مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاَللَّهِ وَالْيَوْمِ...

Soma Zaidi...
Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika surat Hashir

Huwaoni wale wanafiki wanawaambia ndugu zao walio makafiri miongoni mwa watu waliopewa Kitabu (kabla yenu) Mayahudi (Wanawaambia): "Kama mkitolewa, (mkifukuzwa hapa) tutaondoka pamoja nanyi, wala hat utamtii yoyote kabisa juu yenu.

Soma Zaidi...
Kujiepusha na kukaribia zinaa

Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.

Soma Zaidi...