image

Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika Surat ahzab

Na waliposema wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, "Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu.

Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika Surat ahzab

Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika Surat ahzab



Na waliposema wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, "Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu." Na taifa moja miongoni mwao liliposema "Enyi, wenyeji wa Yathribu (Madina)! Hamna mahali pa kukaa nyinyi, basi rudini Na kundi jingine miongoni mwao likaomba ruhusa kwa Mtume kwa kusema: "Hakika nyumba zetu ni tupu, (hapana watu, tunakwenda zetu)," lakini hazikuwa tupu, hawakutaka ila kukimbia tu. Na lau kama yaliingia (Majeshi ya makafiri) juu yao katika pande zote , kisha wakaombwa kufanya vita (juu ya Waislamu) wangevifanya, na wasingelikaa humo (Madina tena) ila muda kidogo tu (33:12-1 4)


Na kwa yakini walikwishafanya ahadi na Mwenyezi Mungu zamani ya kwamba hawatageuza migongo ; na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni yenye kuulizwa. (33:15)



Sema: "Kukimbia hakutakufaeni kama mkikimbia mauti au kuuawa, na kwa hivyo, hamtastareheshwa ila kidogo tu, (kisha mara mtakufa)." Sema: "Ni nani ambaye aweza kukulindeni na Mwenyezi Mungu kama (Mungu) akikutakieni uovu, au akikutakieni rehema?" Wala hawatapata mlinzi wala msaidizi kinyume cha Mwenyezi Mungu.Bila shaka Mwenyezi Mungu anawajua wale wanaojizuia miongoni mwenu (wasende vitani pamoja na Mtume) na wawaambiao ndugu zao; "Njooni kwetu (wala msende kwa Muhammad);" wala hawendi katika mapigano ila kidogo tu (ili kuwadanganya Waislamu). (33:16-1 8)


Wakakufanyieni choyo (kukusaidieni) lakini inapokuja hofu, utawaona wanakutazama, macho yao yanazungukazunguka kama yule aliyezimia kwa mauti; lakini hofu inapoondoka, wanakuudhini kwa ndimi zao kali, wanaifanyia choyo kheri, (hawataki kusaidia). Hao hawakuamini, kwa hivyo Mwenyezi Mungu ameviondoshea thawabu vitendo vyao; na hayo ni sahali kwa Mwenyezi Mungu. (Mpaka sasa kwa woga wao) Wanafikiri yale makundi (ya maadui) hayajaondoka. Na kama makundi hayo yangekuja (tena), wangependa laiti wangekua wako jangwani pamoja na Mabedui, wakiuliza tu habari zenu. Na kama wangalikuwa pamoja nanyi wasingalipigana ila kidogo tu. (Mara wangelikimbia kwa woga wao). (33:19-20)



Sifa za wanafiki zilizoainishwa katika aya hizi ni hizi zifuatazo:
(i) Humdhania Mwenyezi Mungu na Mtume wake dhana mbaya. Walisema wakati ule wa Mtume (s.a.w): "Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu."
(ii) Huwahofisha na kuwakatisha tamaa waumini ili warudi nyuma wasipambane na maadui wa Uislamu.
(iii) Hutoa nyudhuru za uwongo ili kuepa majukumu ya kuuhami Uislamu na kuuendeleza.
(iv) Huvunja ahadi kila wanapoahidi.
(v) Hawako tayari kupata misukosuko kwa ajili ya Uislamu na huogopa kufa. Hivyo hujitenga mbali na mapigano dhidi ya maadui wa Uislamu.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 259


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

vigawanyo vya elimu
Soma Zaidi...

Maana ya muislamu.
Kwenye kipengele hichi tutajifunza ni nani muislamu. Soma Zaidi...

Shirk na aina zake
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Maswali juu ya mtazamo wa uislamu kuhusu dini
Mtazamo wa uislamu kuhusu dini (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kuwa mwenye Kumtegemea Allah
35. Soma Zaidi...

SIFA ZA WAUMINI
Soma Zaidi...

Sifa za Waumini zilizotajwa katika surat Ahzab
Bila shaka wanaume wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanawake wanaozifuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanaume wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanawake wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanaume wanaotii, na wanawake wanaotii, na wanaume wa Soma Zaidi...

Dalili za kuwepo mwenyezi Mungu
Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Maadili katika surat luqman
Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Furqaan (25:64-76)
Soma Zaidi...

Kwa nini Elimu imepewa nafasi ya kwanza katika Uislamu?
Kwa nini katika uislamu elimu imepewa nafasi ya kwanza ( EDK form 1 Dahana ya elimu) Soma Zaidi...

Elimu ya mwingozo na elimu ya mazingira katika uislamu
Mahusiano kati ya elimu ya mwongizo na elimu ya mazingira katika uislamu. Soma Zaidi...