Kubisha hodi katika nyakati za faragha katika familia

β€œEnyi mlioamini!

Kubisha hodi katika nyakati za faragha katika familia

(i) Kubisha hodi katika nyakati za faragha katika familia



β€œEnyi mlioamini! Nawakupigieni hodi wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume, (ya kulia), na wale wasiofikia baleghe miongoni mwenu, mara tatu: kabla ya Sala ya Alfajiri na mnapovua nguo zenu Adhuhuri, na baada ya Sala ya Isha; hizi ni nyakati tatu za faragha kwenu. Si vibaya juu yenu wala juu yao baada ya nyakati hizo (kuingia bila ya kupiga hodi:) mnazungukiana nyinyi kwa nyinyi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu Anavyokuelezeni Aya (zake); na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hikima.



β€œNa watoto miongoni mwenu, watakapobaleghe basi nawapige hodi kama walivyopiga hodi wale wa kabla yao. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyokubainishieni aya zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hikima. (24:58-59)



Katika aya hizi tunapewa maelekezo ya kinidhamu na kimaadili juu ya watoto na watumishi kuwatembelea wazazi wakiwa nyumbani mwao kama ifuatavyo:
(i)Waumini wanatakiwa wawaelekeze watoto wao ambao hawajafikia baleghe kuwa wabishe hodi wanapotaka kuingia vyumbani katika nyakati tatu za faragha zilizoainishwa:
1.Kabla ya Swala ya Al-fajiri
2.Kabla ya Swala ya Adhuhuri wakati wa kujitayarisha kwa swala.
3.Baada ya Swala ya Al-Ishaa.
(ii)Mida mingine nje ya hii watoto wanaruhusika kuingia bila ya hodi. Kwa maana nyingine wazazi wawe katika hali ya sitara ambayo haitakuwa ni chukizo watakapokutwa na watoto.
(iii)Watoto waliofikia baleghe hawaruhusiwi kuingia chumbani mwa wazazi wao pasina kubisha hodi katika nyakati zote.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 1332

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰2 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰3 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰4 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰5 Dua za Mitume na Manabii    πŸ‘‰6 web hosting   

Post zinazofanana:

Mambo muhimu anayofanyiwa muislamu kabla ya kufa

Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Kuamini vitabu vya mwenyezi Mungu (s.w)

Nguzo za Imani (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat al-Baqarah

Na katika watu, wako (wanafiki) wasemao: "Tumemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho"; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini.

Soma Zaidi...
Aina kuu za dini

Katika kipengele hichi tutajifunza aina kuu mbili za dini.

Soma Zaidi...
Mazingatio kabla ya kuosha maiti

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Vipi Allah huwasiliana na wanadamu kwa kupitia njia ya maandishi

Allah hutumia maandishi kuwafundisha wanadamu. Mfano mzuri ni nabii Musa ambaye alipewa vibao vya maandishi.

Soma Zaidi...