image

Muhtasari wa sifa za waumini

Lengo tarajiwa la Muhtasari huu ni kutuwezesha kuzibaini fika sifa za Waumini zilizoainishwa katika Qur'an, kisha kujipamba nazo ili tuwe waja wema watakaorehemewa na kuridhiwa na Allah (s.

Muhtasari wa sifa za waumini

Muhtasari wa sifa za wauminiLengo tarajiwa la Muhtasari huu ni kutuwezesha kuzibaini fika sifa za Waumini zilizoainishwa katika Qur'an, kisha kujipamba nazo ili tuwe waja wema watakaorehemewa na kuridhiwa na Allah (s.w).1. Al-Anfal (8:2-4).
(i) Anapotajwa Allah (s.w) nyoyo zao hujawa na khofu
(ii)Wanaposomewa aya za Allah (s.w) huwazidishia Imani.
(iii)Wanamtegemea Mola wao tu basi katika kila jambo lao.
(iv)Wanasimamisha swala.
(v)Wanatoa katika yale walioruzukiwa na Mola wao ikiwa ni pamoja na Zakat, Sadaqaat, n.k. kwa ajili ya Allah (s.w).


2. Ar-Raad (13:19-24)
(i)Huamini na kuyafuata yaliyotoka kwa Allah (mafundisho ya Qur'an na Sunnah).
(ii)Hutimiza Ahadi ya Allah (s.w) (6:162:163), (7:172-173), (33:72-73).
(iii)Hawavunji ahadi za wanadamu wenzao kwa hali yoyote ile.
(iv)Huyaunga aliyoamuru Allah (s.w) yaungwe .
(v)Humuogopa Mola wao kwa kuzingatia uwezo wake, nguvu zake, na mamlaka yake yasiyo na kikomo.
(vi)Huiogopa siku ngumu ya Hesabu na Hesabu mbaya ikawa sababu ya kuyakimbia maovu na kuyaendea mema na mazuri.
(vii)Ambao pia huwa na subira na uvumilivu katika mazito yanayowakabili katika maisha.
(viii)Husimamisha swala.
(ix) Hutoa katika vile walivyoruzukiwa na Allah (s.w) kwa siri na dhahiri.3. Al-Mu'uminuuna (23:1-11).
(i)Huwa wanyenyekevu katika swala zao.
(ii)Hujiepusha na mambo ya upuuzi (laghwi) - Upuuzi ni jambo lolote ambalo humtoa mtu katika lengo la kumuabudu Allah (s.w) na kusimamisha Ukhalifa katika jamii.
(iii)Hutoa katika yale waliyoruzukiwa na Allah (s.w).
(iv)Huhifadhi tupu zao kwa kusitiri uchi na kujiepusha na zinaa.
(v)Huchunga amana zao.
(vi)Hutekeleza ahadi zao.
(vii)Huhifadhi swala zao.


4. Al-Furqaan (25:63-77).
(i)Huwa ni wanyenyekevu (walioepukana na kibri, majivuno,(n.k.) na wenye nidhamu katika kuendesha maisha yao ya kila siku.(ii)Watu wajinga (wasio na nidhamu wala ustaarabu katika maisha yao) wakiwakorofisha huwasiliana nao kwa njia ya amani (husema nao maneno ya salama).(iii)Hupitisha baadhi ya saa zao za usiku kwa ajili ya Mola wao kwa kusujudu na kusimama (kuswali Tahajjud/Qiyaamullayl).(iv)Humuomba Mola wao awaepushe na adhabu ya Jahannam kwa kujua kwamba ni pahala pabaya pa kukaa Mja.(v)Wanapotumia hawafanyi Israaf (kutumia kwa fujo) wala hawatumii kwa ubakhili bali hutumia kwa kadiri ( kati kwakati).(vi)Hawamuombi mungu mwingine pamoja na Allah(s.w) na hawamshirikishi Allah (s.w) katika aina zote za shiriki. (vii)Hawaui nafsi iliyoharamishwa kuuawa ila kwa haki. (viii)Hawakaribii zinaa wala kuzini.(ix)Huwa na tabia ya kuleta toba ya kweli kila wanapokosea kosa dogo au kubwa kwa kufuata masharti yake ambayo ni (1) Kumuamini Allah (s.w) ipasavyo, (2) Kudumu katika kutenda vitendo vizuri, (3) Kujutia dhambi waliyofanya, (4) Kuchukuwa ahadi na azma ya kutorejea tena dhambi hiyo (5) Kurejesha haki kwa wenyewe (6) Kisha kumuelekea Mola na kumuomba msamaha kwa khushui.(x)Hawashuhudii shahada za uongo (hawatoi ushuhuda wa uongo) hata kama ni juu ya nafsi zao au watu wao wa karibu. (xi)Wanapopita penye upuuzi, hupita kwa heshima zao.


(xii)Wanapokumbushwa Aya za Mola wao hawaziangukii kwa uziwi na upofu (huziingiza katika utendaji).(xiii)Humuomba Mola wao awape wake wema na watoto we ma.(xiv)Humuomba Allah (s.w) awajaalie kuwa viongozi wa wamchao yeye (Allah) ambao ni wapesi kuelekea katika njia iliyonyooka.


5.As-Sajdah (32:12-20).
(i) Wanapokumbushwa Aya za Mwenyezi Mungu huzitii na kuzitekeleza ipasavyo
(ii)Humtukuza Mola wao kwa sifa zake tukufu (huleta mara kwa mara tasbihi, tahmid, tahlili, takbir, n.k.)
(iii)Hawafanyi kiburi katika ardhi (Hawatakabari).
(iv)Huinua mbavu zao usiku kutoka vitandani mwao kwa ajili ya kuswali Tahajjud, kwa kuogopa Moto na kutaraji Pepo. (v) Hutoa katika vile walivyoruzukiwa na Mola wao.
6.Al-Ahzaab (33:35-36)
(i)Husimamisha nguzo za Uislamu ipasavyo.
(ii)Huamini nguzo zote za Imani ipasavyo kimatendo.
(iii)Ni watiifu kwa Allah (s.w) ipasavyo katika kuendesha maisha yao ya kila siku.
(iv)Husema kweli na kusimamia ukweli.
(v)Huwa na subira.
(vi)Ni wanyenyekevu kwa Allah (s.w) katika kuendesha maisha yao.
(vii)Hutoa vile walivyoruzukiwa na Allah (s.w) kuwapa wanaostahiki.
(viii)Hufunga swaumu ya mwezi wa Ramadhani na funga za Sunnah.
(ix)Huhifadhi tupu zao na hujiepusha na zinaa.
(x)Humkumbuka Allah (s.w) kwa wingi na kumtaja kwa wingi. (xi)Hawawi na khiyari katika mashauri ambayo Allah (s.w) na Mtume wake wameshapitisha hukukumu juu yake (yaani hutii bila ubishi au bila kuhoji).

7.Ash-Shu'ura (42:30-43).
(i)Wanamuamini Allah (s.w) na Mtume wake na nguzo zote za Imani.
(ii)Humtegemea Mola wao katika kila jambo lao
(iii) Wanajiepusha na Madhambi makubwa na hujiepusha na mambo mabaya.
(iv)Wanapokasirika husamehe.
(v)Huitikia amri za Mola wao kila wanapoamrishwa.
(vi)Husimamisha swala.
(vii)Hushauriana katika mambo yao.
(viii)Hutoa katika vile walivyoruzukiwa na Mola wao. (ix)Jeuri inapowafikia huzitetea nafsi zao.
(x) Husuluhisha ugomvi baina yao.
(xi)Hulipiza kisasi baada ya kudhulumiwa.
(xii)Huwa na Subira.8.Al-Maarij (70:19-35).
(i) Husimamisha swala.
(ii)Hudumisha sala zao.
(iii)Katika Mali zao iko sehemu maalumu ya kuwapa
wanaostahiki.
(iv)Husadiki siku ya Malipo.
(v)Huogopa adhabu itokayo kwa Mola wao.
(vi)Huhifadhi tupu zao. (vii)Huzichunga amana zao. (viii)Huziangalia ahadi zao.
(ix)Wako Imara katika Ushahidi wao (husimamia ushahidi
vilivyo).9.Al-Hujuraat (49:15).
(i) Humuamini Allah na Mtume wake ipasavyo kwa kufuata kwa unyenyekevu maamrisho yao yote na kuacha kwa unyenyekevu makatazo yao yote.
(ii)Hupigania dini ya Allah kwa mali zao na nafsi zao.
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 343


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Historia ya Mwanadamu
Soma Zaidi...

Nafsi ya mwanaadamu
Soma Zaidi...

Kwa namna gani nabii Musa na Bi Mariam waliweza kuzungumza na Allah nyuma ya pazia
Nabii Musa na Mama yake nabii Isa bi Mariam waliweza kuwasiliana na Allah nyuma ya pazia. Soma Zaidi...

Maana ya Kumuamini Allah (s.w) katika Utendaji wa kila siku
Soma Zaidi...

“Allah (s.w) humwingiza katika rahma zake amtakaye na kumwacha kupotea amtakaye”
Soma Zaidi...

NJIA ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU (S.W)
Zifuatazo ni njia nyingi za kumjua Mwenyezi Mungu (EDK form 2:dhana ya elimu katika uislamu) Soma Zaidi...

Sifa za malaika
Soma Zaidi...

Nguzo za imani
Zifuatazo ni nguzo za imani (EDK form 2: elimu ya dini ya kiislamu) Soma Zaidi...

Njia ambazo Allah hufundisha wanadamu elimu mbalimbali
Ni kipi chanzo cha Elimu, na ni kwa namna gani Allah hufundisha Elimu kwa wanadamu? Soma Zaidi...

mwanadamu hawezi kuishi bila ya Dini
Soma Zaidi...

Maadili na malezi ya jamii
Soma Zaidi...

Mtazamo wa kikafiri juu ya maana ya dini.
Maana ya dini kwa mujibu wa makafiri ina utofauti mkubwa na vile ambavyo uislamu unaamini kuhusu dini. Soma Zaidi...