35.
35. Kumtegemea Mwenyezi Mungu (s.w)
Muislamu wa kweli daima huwa jasiri kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu katika kila hali. Ana yakini kuwa hapana lolote litakalomfika, baya au zuri, ila litakuwa linatoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) na ana yakini kuwa ulinzi wa maisha yake na mahitajio yake yote ya kimaisha yako mikononi mwa Mwenyezi Mungu (s.w). Mwenyezi Mungu (s.w) anatuamrisha tumtegemee Yeye tu katika aya zifuatazo:
Na tegemea kwa Yule aliye na uhai wa milele ambaye hatakufa ”. (25:58)
“... Na kwa Mwenyezi Mungu wategemee Waislamu. Na tuna nini tusimtegemee Mwenyezi Mungu, na hali Ametuonyesha njia zetu. Na tutayavumilia maudhi yenu. Basi kw a Mw enyezi Mungu w ategemee wategemeao”. (14:11-1 2)
“...Na anayemuogopa Mw enyezi Mungu, (Allah) humtengenezea njia ya kuokoka (na kila balaa); na humpa riziki kwa namna asiyoitazamia. Na anayem tegemea Mw enyezi Mungu yeye hum toshea. Kw a yakini Mw enyezi Mungu anatimiza kusudio lake. Hakika Mwenyezi Mungu amekwisha kiwekea kila kitu kipimo chake”. (65:2-3).
Kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa kila jambo na hasa wakati wa dhiki na kuhitajia msaada, huzidisha imani na ujasiri kwa waumini. Hebu turejee aya zifuatazo:
“Wale ambao watu w aliwaambia: “Watu wamekukusanyikieni. Kwa hiyo waogopeni”. Lakini (maneno hay o) yakawazid ishia imani wakasema Mwenyezi Mungu anatutosha. Naye ni Mlinzi bora kabisa. Basi w akarudi (vitani na neema za Mwenyezi Mungu na fadhila zake), hakuna ubaya uliowagusa; na wakafuata yanayomridhisha Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kuu”. (3:173-174)
“Na Waislamu walipoyaona majeshi (ya makafiri) walisema, “Haya ndiyo aliyotuahidi Mw enyezi Mungu na Mtume wake. Mw enyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli,na (jambo hili) halikuwazidishia ila imani na utii. (33:22).
“Hakika waumini wa kweli ni wale ambao anapotajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa hofu; na wanaposomewa Aya Zake huwazidishia imani na wakamtegema Mola wao tu basi”. (8 : 2)
Hivyo Waislamu hatuna budi kumtegemea Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kila hali. Tukifanya hivyo imani yetu itazidi na tutakuwa na moyo wa ujasiri wa kutuwezesha kupambana na hali yoyote ngumu itakayotukabili kwa sababu tunayakini kuwa halitufikii lolote, baya au zuri, ila liko katika makadirio ya Mwenyezi Mungu (s.w). Ni vyema hapa tukumbushe kuwa kumtegemea Mwenyezi Mungu (s.w) ni kutekeleza wajibu wetu kwa juhudi na maarifa katika jambo lolote tunalolifanya kisha matokeo ya jitihada zetu tumuachie Mwenyezi Mungu (s.w). Hii hasa ndio maana ya kumtegemea Allah (s.w) kama tunavyojifunza.katika aya zifuatazo:
“Naam, wanaoelekeza nyuso zao kwa Mwenyezi Mungu na wakawa ni watendaji mema, basi wao watapata malipo yao kwa Mola wao, wala haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika. (2:112).
Na kwamba, mtu hatapata ila kwa yale anayoyafanya. (53:39).
Umeionaje Makala hii.. ?
Kwa nini katika uislamu elimu imepewa nafasi ya kwanza ( EDK form 1 Dahana ya elimu)
Soma Zaidi...Hii ni njia ambayo mwanaadamu huongeleshwa moja kwa moja na Allah (s.
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha dalili,sababu na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa aliyepata jeraha kwenye ngozi kwa kuingiliwa na kitu Kama mwiba,Pini,sindano n.k
Soma Zaidi...Yale tunayoamrishwa kushikamana nayo ni haya yafuatayo: (i)Kumuabudu Allah (s.
Soma Zaidi...Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...(v)Kuwaombea dua wazazi.
Soma Zaidi..."Hakika wanaoamini kweli ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa khofu; na wanaposomewa aya zake huwazidishia imani na wanamtegemea Mola wao tu basi.
Soma Zaidi...Kuamini Malaika ni imani ambayo pindi ikithibiti vema moyoni, huleta taathira kubwa sana katika maisha ya kila siku na hivyo kubadili kabisa tabia na mwenendo wa Muumini.
Soma Zaidi...