Waumini wa kweli wa Mitume wa Allah (s.
Waumini wa kweli wa Mitume wa Allah (s.w) ni wale wenye tabia ifuatayo:
1. Kuwatii Mitume ipasavyo kwa kufanya yale yote waliyoamrisha na kuacha yale yote waliyoyakataza kama Qur’an inavyosisitiza:“... Na anachokupeni Mtume basi pokeeni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho...” (59:7)Sem a: “Ikiw a nyinyi mnampenda Mw enyezi Mungu, basi nifuateni;(hapo)Mw enyezi Mungu atakupendeni na atakughufirieni madhambi yenu.Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira, mwenye rehema.Sema: “Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume. Na kama mkikengeuka, (Mw enyezi Mungu atakutieni adabu), kw ani Mw enyezi Mungu haw apendi Makafiri” (3 :31-32)
2.Kuwafanya Mitume vigezo vya maisha yao kibinafsi, kifamilia na kijamii kama inavyosisitizwa katika Qur-an:“Bila shaka mnao mfano mwema (wa kuiga) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na kumtaja Mwenyezi Mungu sana ”. (33:21)
3.Kuwapenda Mitume kuliko nafsi zao kama Qur-an inavyosistiza:“Sema “Kama baba zenu na wana wenu na ndugu zenu na wake zenu na jamaa zenu na mali m lizozichum a na biashara mnazoogopa kuharibikiw a,na majumba mnayoyapenda; (ikiwa vitu hivi) ni vipenzi zaidi kw enu kuliko Mw enyezi Mungu na Mtume wake na kupigania dini yake, basi ngojeni mpaka Mw enyezi Mungu alete am ri yake; na Mw enyezi Mungu hawaongozi watu maasi” (9:24)
Kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume si jambo lingine zaidi ya kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa unyenyekevu na upendo. Muumini wa kweli hatakuwa tayari kuifurahisha nafsi yake au kumfurahisha yeyote awaye kinyume na kumfurahisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Ni katika maana hii Mtume (s.a.w) anasema:
“Hatakuwa mmoja wenu ni Muumini wa kweli mpaka anipende zaidi kuliko chochote kile ikiwa ni pamoja na familia yake, mali yake na watu wote”.(Sahihi Muslim)
“Yeyote yule anayependa Sunnah yangu ananipenda, na yeyote yule anayenipenda atajikuta yuko ubavuni kw angu huko Peponi.” (Tirm idh)
4. Kuwafanya Mitume kuwa Mahakimu wao pale wanapohitilafiana katika jambo lolote lile kama tunavyojifunza katika Qur-an:“Naapa kwa (haki ya) Mola wako (Ewe Muhammad); wao hawawi wenye kuamini mpaka wakufanye hakimu katika yale wanayokhitalifiana, kisha wasione uzito nyoyoni mwao juu ya hukumu uliyopitisha, na wanyenyekee kabisa.” (4:65)“Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiyari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake hakika amepotea upotofu (upotevu) ulio wazi. ” (33:3 6)
5.Kuwa na yakini kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) ndiye Mtume wa mwisho kama Qur-an inavyosisitiza:“Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa Mitume, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu.” (33:40)
6.Kumswalia Mtume(s.a.w) mara kwa mara katika swala na kila anapotajwa. Kumswalia Mtume(s.a.w) ni amri ya Allah(s.w) kama inavyotuelekeza ifuatavyo:Hakika Mwenyezi Mungu anamteremshia Rehema Mtume;na Malaika wake. Basi; Enyi mlioamini, msalieni Mtume na muombeeni amani.(33:56)
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1822
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Kitabu cha Afya
👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Athari za vita vya Uhud
Vita vya uhudi viliweza kuleta athari nyingi. Post hii itakuletea athari baadhi za vita hivyo. Soma Zaidi...
Ushahidi juu ya kosa la Uzinifu
Ushahidi wa kuthibitisha kutendeka kwa kosa la uzinifu unapatikana kwa namna tatu zifuatzo: (i)Kushuhudia tendo hilo likifanyika kwa wakati mmoja watu wanne Mukalafu (Walio baleghe na wenye akili timamu), wakiwa ni Waislamu waadilifu. Soma Zaidi...
Dalili Kubwa za kukaribia Siku ya kiama
Soma Zaidi...
Mgawanyiko wa Elimu kwa mtazamo wa kikafiri
Kwa mtazamo wa kikafiri elimu imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Elimu ya dunia na Elimu ya akhera. Soma Zaidi...
Kujiepusha na ubadhirifu (israfu) na ubakhili
Soma Zaidi...
Dalili (Alama) za Qiyama
Soma Zaidi...
Lengo la kuletwa mitume
Mitume wameletwa kuwa Waalimu na viongozi wa kuwafundisha watu Uislamu na kuwaelekeza kuusimamisha Uislamu katika jamii kinadharia na kimatendo kama tunavyojifunza katika Qur-an:“Kwa hakika Tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na Tukavitere.. Soma Zaidi...
Mazingatio kabla ya kuosha maiti
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Neema Alizotunukiwa Nabii Daudi(a.s)
Soma Zaidi...
Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat at-Tawbah
Mwenyezi Mungu amekuwia radhi (amekusamehe). Soma Zaidi...