Enyi mlioamini!
Enyi mlioamini! Msiingie nyumba ambazo si nyumba zenu mpaka muombe ruhusa, (mpige hodi) na muwatolee salamu waliomo humo. Hayo ni bora kwenu; huenda mtakumbuka (mkaona ni mazuri haya mnayoambiwa).
Na kama hamtamkuta humo yeyote, basi msiingie mpaka mruhusiwe . na mkiambiwa "Rudini," basi rudini; hili ni takaso kwenu. Na Mwenyezi Mungu Anajua mnayoyaatenda. Si vibaya kwenu kuingia majumba yasiyokaliwa, (yasiyofanywa maskani: kama mahoteli, maktaba), ( bila kupiga hodi), ambamo humo mna manufaa yenu; na Mwenyezi Mungu Anajua mnayoyadhihirisha na mna yoyaficha. (24:27-29)
Kutokana na aya hizi tunajifunza adabu za kuingia katika nyumba za watu kama ifuatavyo:
(i)Hairuhusiwi mtu kuingia nyumba ya mtu bila ya kubisha hodi. Hata kama utaukuta mlango uko wazi, huruhusiwi kuangaza macho ndani. Hivyo wakati wa kubisha hodi unatakiwa uwe pembeni mwa mlango, kiasi kwamba hata kama mlango umefunguliwa usiweze kumuona mtu au vitu vilivyomo ndani. Vile vile hairuhusiwi kubisha hodi kupitia mlango wa uani au madirishani. Hekima ya amri hii ya kubisha hodi, ni kulinda haki ya faragha (privacy) ambayo ni haki ya msingi kwa binaadamu katika mambo mema.
(ii)Hata baada ya kuruhusiwa kuingia katika nyumba za watu,hatutaingia mpaka kwanza tuwatolee salamu waliomo ndani.
(iii)Kama mtu atabisha hodi mara tatu bila ya kuitikiwa, hata kama atakuwa anawasikia watu wakiongea ndani, asiingie bali aondoke aende zake bila kinyongo.
(iv)Iwapo mtu ataitikiwa baada ya kubisha hodi na badala ya kukaribishwa ndani akaambiwa arudi, hanabudi kurudi kwa moyo mkunjufu bila ya manung'uniko yoyote.
(v)Hatuhitajiki kubisha hodi kwenye nyumba zenye kutoa huduma za kijamii kama vile hoteli, maktaba, msikiti, n.k.
Umeionaje Makala hii.. ?
Kwenye kipengele hichi tutajifunza lengo la kuumbwa mwaanadamuengo la kuumbwa ulimwengu na viumbe vilivyomo.
Soma Zaidi...Kwa nini katika uislamu elimu imepewa nafasi ya kwanza ( EDK form 1 Dahana ya elimu)
Soma Zaidi...Na tukiutafiti Uislamu kwa makini kama mfumo kamili wa maisha tunaona unadhihiri ukweli wa aya hii ya Qur-an.
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hichi titajifunza maana ya uislamu,na maana nyingine tofauti.
Soma Zaidi...Ni nini maana ya Elimu na ni nani aliye elimika? Uislamu una mtazamo gani juu ya Elimu?
Soma Zaidi...Yale tunayoamrishwa kushikamana nayo ni haya yafuatayo: (i)Kumuabudu Allah (s.
Soma Zaidi...