Haki ya ElimuKatika Uislamu kujielimisha ni faradhi inayowahusu Waislamu wote, wanaume na wanawake: "Soma kwa jina ?
Haki ya Elimu
Katika Uislamu kujielimisha ni faradhi inayowahusu Waislamu wote, wanaume na wanawake: "Soma kwa jina ?a Mola wako aliyeumba" (96: 1). Aya hii na nyingi nyinginezo zinazosisitiza elimu katika Uislamu hazikumbagua mwanamke. Pia Mtume (s.a.w) katika kusisitiza elimu amesema: "Kutafuta elimu ni faradhi kwa kila Muislam mwanamume na kila Muilsm mwanamke ".
Bali kutokana na tabia ya jamii nyingine ulimwenguni ya kuwanyanyasa wan awake na kuwaona kuwa ni nuksi, wasiostahiki kulelewa vizuri na kuelimishwa, Uislamu umetoa motisha mkubwa wa ahadi ya kupata malipo makubwa kutoka kwa Allah (s.w) kwa kuwalelea watoto wa kike vizuri na kuwaelimisha ipasavyo. Katika Hadith iliyosimuliwa na Imam Ahmed, Mtume (s.a.w) amesema:
Yeyote atakayewalea mabinti wawili hadi wakakua, yeye na mimi Siku ya Kiyama tutakuwa kama hivi. (Akaonesha vidole vyake viwili iii kupigia mfano watakavyokuwa karibu sana huko Peponi). (Ahmad)
Lengo Ia mafundisho haya ya Mtume (s.a.w) ni kuwaondosha watu katika zile fikra dhaifu za kuwaona watoto wa kike kama kwamba si watu. Na katika Hadith nyingine iliyosimuliwa pia na Ahmed, Mtume (s.a.w) amesema: Yeyote ambaye amemzaa binti, na hakumzika yungali hai, na hakumtukana au kumkashfu, na hakumpendelea mtoto wake wa kiume zaidi kuliko huyo wa kike, Allah atamuingiza Peponi. (Ahmad)
Zaidi ya mafundisho haya Mtume (s.a.w) alionesha mfano katika maisha yake mwenyewe, kwa kuwaheshimu na kuwatendea vizuri binti zake, kiasi ambacho aliwahi kusema juu ya binti yake, Fatma; "Fatma ni sehemu yangu mimi, furaha yake ni yangu, na ghadhabu zake ni uchungu wangu ".
Umuhimu wa kuwaelimisha watoto wa kike uko wazi. Tumeona kuwa katika jamii ya Kiislamu hapana budi kuwepo wanawake madaktari, wauguzi, walimu n.k. Ni dhahiri kuwa itabidi waelimishwe kwanza ndio waweze kupata ujuzi wa kufanya kazi hizo.
Wanawake wajifunze fani zipi za Elimu? Qur'an haijaweka mipaka yoyote inayowakataza wanawake fani fulani fulani za elimu. Kama kuna fani ya elimu ambayo ni haramu kwa wanawake basi fani hiyo itakuwa pia haramu kwa wanaume. Kwa mfano kujifundisha uchawi ni haramu kwa Waislamu wote (wanaume na wanawake),Qur'an (2: 102).
Ingawa kila mtu anayohaki ya kujipatia elimu, katika fani na kiwango chochote anachoweza, kipo kiwango fulani cha elimu ambacho ni lazima kila mtu awe nacho. Elimu ya lazima ni pamoja na kujua misingi ya Uislamu - Imani na Nguzo za Uislamu, namna ya kutekeleza Kwa ukamilifu Ibada maalum kama vile, kusimamisha swala, zakati, funga, hija, n.k., kujua wajibu katika familia na katika jamii, kujua katika maisha yetu ya kila siku lipi ni halali kulitenda na lipi ni haramu kwa mujibu wa Qur'an na Sunnah. Kwa ujumla elimu juu ya mambo haya ya msingi, tunaiita elimu ya mwongozo". Elimu hii ni faradh am kwa kila muislamu mwanamume na mwanamke.
Ingawa wanawake hawajazuiliwa kusomea fani yoyote ya elimu, bado tunaweza kusema kuwa zipo baadhi ya fani za elimu ambazo .ni vizuri sana wanawake wakizisomea kwani zitawafaa sana katika kutimiza jukumu Ia uzazi na malezi ya jamii, kama vile elimu ya tiba (medicine) uuguzi (nursing), ualimu, uendeshaji wa nyumba (home management), saikolojia, n.k. Fani nyingine za elimu zinabakia kuwa ni halali kwao kama zilivyo halali kwa wanaume.
Kutokana na mifano hii michache katika maeneo haya ya haki tuliyojaribu kuyabainsiha humu, Uislam kama ulivyo Dini ya haki, humpa kila mtu haki yake bila ya ubaguzi wa ama yoyote.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 558
Sponsored links
π1
Kitabu cha Afya
π2
Simulizi za Hadithi Audio
π3
Kitau cha Fiqh
π4
kitabu cha Simulizi
π5
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
π6
Madrasa kiganjani
Ni nini maana ya Ilhamu katika uislamu?
Ilhamu ni moja katika njia ambazo Allah huwasiliana na wanadamu na kuwafundisha mambo mablimbali. Soma Zaidi...
KUMUAMINI MWENYEZIMUNGU
Soma Zaidi...
Mtazamo wa Uislamu juu ya maana ya dini
Uislamu unaitazama dini katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Hii ni tofauti na mtazamo wa kikafiri juu ya dini. Soma Zaidi...
Kuamini Qadar ya Allah (s.w)
Soma Zaidi...
mgawanyiko wa elimu
Soma Zaidi...
Ni ipi maana ya Imani katika Uislamu, na ni zipi sifa za muumini.
Katika Uislamu imani inanguzo kuu 6.Pia muumini anatakiwa ajipambe na sifa za waumini. Posti hii itakufundisha kuhusu imani katika Uislamu. Soma Zaidi...
NJIA ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU (S.W)
Zifuatazo ni njia nyingi za kumjua Mwenyezi Mungu (EDK form 2:dhana ya elimu katika uislamu) Soma Zaidi...
Kujiepusha na kuua nafsi bila ya Haki
Kuua nafsi bila ya Haki, ni kuiua nafsi isiyo na kosa linalostahiki hukumu ya kifo. Soma Zaidi...
Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Muβuminuun (23:1-11)
Soma Zaidi...
Maswali juu ya mtazamo wa uislamu kuhusu dini
Mtazamo wa uislamu kuhusu dini (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...