Katika somo hili tutajifunza: Tofauti kati ya hashing na encryption Jinsi ya kufunga packages muhimu Jinsi ya kufanya hashing kwa maneno ya kawaida (mfano “bongoclass”) Jinsi ya kufanya encryption na decrypt kutumia Fernet Jinsi Django inahash password kupitia User model Mazoezi ya vitendo
Katika mifumo ya kisasa ya web, usalama wa data ni jambo la lazima. Django imeshawekewa mifumo thabiti ya kusimamia usalama wa password, na tunao uwezo wa kuongeza hashing na encryption ya data yoyote tunayotaka kulinda. Tutatumia shell ili ku run mifano.
Kabla ya kuanza, ni muhimu kujua kwamba:
Hashing ni “one way”—haiwezi kurejeshwa.
Encryption ni “two way”—unaweza kusimba na kufumbua (encrypt na decrypt).
Sasa tuingie kwenye maelezo ya kina.
| Kigezo | Hashing | Encryption |
|---|---|---|
| Maana | Kubadilisha data kuwa mfuatano wa herufi zisizorejesheka | Kusimba data ili isomeke, lakini inaweza kufumbuliwa |
| Mwelekeo | One-way | Two-way |
| Matumizi | Kusalimisha password, tokens | Kulinda data nyeti kama namba za kadi, emails n.k. |
| Mfano | SHA256, bcrypt | AES, Fernet |
pip install cryptography
Hashing ni kubadilisha maneno tusiyopenda yasomeke kuwa “hash code” isiyoweza kurudishwa katika hali yake ya awali.
Django inakuja na hashing nyingi tayari:
SHA256
SHA1
PBKDF2 (default ya Django)
BCrypt
Argon2 (salama zaidi)
import hashlib
data = "bongoclass"
hash1 = hashlib.sha256(data.encode()).hexdigest()
hash2 = hashlib.sha1(data.encode()).hexdigest()
hash3 = hashlib.md5(data.encode()).hexdigest()
print("SHA256:", hash1)
print("SHA1:", hash2)
print("MD5:", hash3)
👏 Hii inafanya hashing—HAIWEZI KUREJESHWA KINYUME.
Django haibebi password kama ulivyoitoa.
Badala yake, hutumia hashing yenye salt. Hii tutakuja kujifunza zaidi tutakapokuwa tunafanya project.
Mfano wa kuweka password:
from django.contrib.auth.models import User
user = User.objects.create(username="sky")
user.set_password("bongoclass123")
user.save()
💡 set_password() inafanya:
Kuongeza salt
Kutumia PBKDF2 (default)
Kutengeneza hash yenye usalama mkubwa
Hakuna developer anayeweza kuona password halisi.
Tofauti na hashing, encryption inaweza kufumbuliwa kurudisha data ya mwanzo. Nikukumbushe tu kuwa tunapofanya encryption maana yake tunaficha data kwa kuziweka kwenye string maalumu ili mtu asiweze kuona data halisi. Hivyo ili kuirudisha data hiyo katika hali ya kawaida tunatakiwa tufanye decryption. hivyo decryption ni kinyume cha encryption. Jambo la kuzingatia ni kutumia key moja.
Key ni kama password za hiyo data yako. Bila ya kuwa na key zilizo sahihi huwezi kuifunguwa data iliyofanyiwa hashing. Key zinatakiwa ziwe 32, na njia bora ya kutengeneza key hizo ni kwa ku run command hiyo hapo chini.
from cryptography.fernet import Fernet
print(Fernet.generate_key())
Itatoa kitu kama:
b'd4q6iHZaYe1pME1TYuRaeCCEe4bO4AUgOTaTSj9Bzg8='
settings.pyFERNET_KEY = b'd4q6iHZaYe1pME1TYuRaeCCEe4bO4AUgOTaTSj9Bzg8='
from cryptography.fernet import Fernet
from django.conf import settings
cipher = Fernet(settings.FERNET_KEY)
email = "mafunzo@bongoclass.com"
encrypted = cipher.encrypt(email.encode())
print(encrypted)
Output inaweza kuwa kitu kama:
b'gAAAAABnggk0zJ7FT....'
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utajifunza Jinsi ya Kuunda Simple Navigation Menu Katika Django kwa kutumia template
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujfnza kuhusu string method nyinginezo. Katika somo lililopita tulijifunza kuhusu string indexing.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza maana ya object, na sheria za kuandika object.
Soma Zaidi...Somo hili linazungumzia hatua ya kuunda navigation menu na kutumia template inheritance kwa njia ya kitaalamu katika Django.
Soma Zaidi...Hapa utakwenda kujifunz amaana ya package, aina zake na jinsi ya kuandika package.
Soma Zaidi...Katika somo ili utajifunza hatuwa kwa hatuwa za ku install Django, kutengeneza project na kutengeneza app
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza vipi django inaweza kuwasiliana na database, utajifunza kuusu orm na model
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhsu Template Tag nini na kazi zake. Pia utajifunza sheria za uandishi wake.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kucheza na data kuzibadili kwa namna mbali mbali kwenye template
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza maana ya polymorphism na sheria za uandishi wake
Soma Zaidi...