Katika somo hili utajifunza kuhusu maana ya python na kazi zake. pia jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya somo.
Python ni moja katika lugha za kikompyuta zilizo maarufu. Ilianzishwa mwaka 1991 na Guido van Rossum. Python ni moja katika high level programming language ambayo ni general programming language yaani inatumika kwenye field nyingi.
Python imekuwa ikifanyiwa marekebisho mengi toka ilipoanzishwa na sasa tupo katika toleo la 3 yaani python 3. Katika course hii tutakwenda kutumia toleo la 3 la python.
Matumizi ya python
Python file extension:
Kama ilivyo kuwa language zote zina extension kama ilivyo hatml ni .html, php ni .php, basi na python ni .py. Mfano main.py
Maandalizi kwa ajili ya course hii:
Kwa watumiaji wa kompyuta:
Course zinazopatikana bongoclass zinalenga wanafunzi wa aina zote. Kwa wale wanaotumia kompyuta na wale waotumia simu janja. Sasa kwa wale wanaotumia kompyuta fuata maelekezo haya:-
Hapo bofya palipoandika New Project.kisha utakuja ukurasa mwingine ambao ni huu
Kama ndio mara yako ya kwanza hapo usiset kitu chochote zaidi ya jina la project yako tu. hapo mwanzoni kabisha kuna palipoandikwa pythonProject
Badili jina la project yako kutoka pythonProject kuwa jina unalotaka wewe. Kwa mfano mimi nitasema pythonMafunzo
Baada ya hapo bofya create kwa chini upande wa kulia. Itaanza kuload ili kuandaa mazngira ya hiyo project yako. Baada ya kumaliza utakutana na ukurasa mkubwa ambao ndio uwanja wa kuanzika code zako.
Kwa upande wa kushoto kuna project root. Ambapo kuna faili linaonekana limefungka kwa upande wa kulia na kuna code utaziona. Faili hilo linaita main.py hilo ndio faili la kwanza la project yako.
Sasa fanuya hivi. Kwenye huo ukurasa uliofunguka upande wa kulia futa kila kitu kisha weka code hizi:
print("haloo bongoclass")
Baada ya hapo run hizo code kwa kubofya kialama cha ku play kilicho upande wa kulia kwa juu
Angalia kwa chini kuna ukurasa umefunguka. Ukurasa huo utaochesha vitu vitatu:-
Hiyo namba 1 inaonyesha hilo faili linapatikana wapi kwenye kompyuta yako. Hiyo namba 2 ndio matokeo ya code zetu. Kwa mfano hapo utaona haloo bongoclass hayo ni matokeo ya code ambayo tumeandika hapo juu. Ha hiyo namba tatu utaona kuwa code 0 kumaanisa kuwa hakuna tatizo. Kama umefiika hapo basi kompyuta yako ipo tayari kuendelea ku code python.
Location ya project yako:
Ili kujuwa mahali ilipo project yako utakwenda kwenye local disc c, kisha user kisha jina la user wa kompyuta yako, kisha shuka mpaka chini utakuta folder limeandika pycharmProject. Hapo ndipo project yako utaikuta.
Kwa watumiaji wa kompyuta somo letu limeishia hapa. Tkutane somo la pili ambapo tutakwenda kuzungumzsia sheria za kuandika code ya python.
Kwa watumiaji wa simu:
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Katika somo hili utakwend akujifunza matumizi ya for loop kwneye python
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunz akutumia database kwenye python
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kuandika function, kuweka parameter na kuitumia function
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujfunza operator nyingine kama assignment operator logical, identity operator na membership operator.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jisni ya kujuwa aina ya data iliyotumika kwenye python
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza aina mbalimbali za function ambazo tunaweza kuzitumia kwenye python.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza maana ya library, kazi zake aina zake na jinsi ya ku install lirary
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data ambazo hutumika kwenye python. hapa utajifunza aina kuu 3 za data.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu number method yaani function zinazofanya kazi kwenye namba.
Soma Zaidi...Katika somo hili tunakwenda kujifunza matumizi ya break na continue kwenye loop
Soma Zaidi...