Katika somo hili utakwend akujifunza ktengeneza model kwa ajili ya database table ya menu yetu.
Katika Django, model ni darasa (class) linalotumika kuunda jedwali (table) kwenye database. Kila kipengele kwenye model ni field inayowakilisha safu (column) ya data.
Tuna mfano wa model yetu kama ifuatavyo:
from django.db import models
class MenuItem(models.Model):
jina = models.CharField(max_length=100)
maelezo = models.TextField(blank=True)
muda_upatikanaji = models.CharField(max_length=50)
bei = models.DecimalField(max_digits=10, decimal_places=2)
def __str__(self):
return self.jina
Hebu tuchambue kila sehemu ya model hii kwa undani:
jina = models.CharField(max_length=100)
CharField hutumika kuhifadhi maandishi mafupi kama majina.
max_length=100 inaweka ukomo wa herufi 100 kwa jina hili.
✅ Mfano wa data: "Chips Mayai"
maelezo = models.TextField(blank=True)
TextField hukusanya maandishi marefu kama maelezo au maudhui marefu.
blank=True ina maana sehemu hii inaweza kuachwa wazi wakati wa kuingiza data.
✅ Mfano wa data: "Chakula hiki hutolewa na maziwa safi."
muda_upatikanaji = models.CharField(max_length=50)
Hii pia ni CharField kwa kuwa muda tunaouandika ni maandishi.
max_length=50 inatosha kwa maandishi kama:
✅ Mfano wa data: "Asubuhi hadi saa 8"
, ...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili uatajifunza jinsi gani unaweza kutumia view kma logic kuuma data kwenye template
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunz ajinsi ya kutengeneza folda, faili na kuweka data kwneye faili
Soma Zaidi...Hapa tunakwenda kujifunza kuhusu OOP ambapo ni miongoni mwa mitindo ya uandishi wa code
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwend akujifunza jinsi ya kutumia while loop kwneye python
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza maana ya encapsulation na sheria za uandishi wake
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz amaana ya inheritance na sheria za kuiandika inheritance.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza syntaxy za python yaani sheria na kanuni za kuandika code za python
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz anamna ya kuwez akupata taarifa zinazohusu faili
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza maana ya polymorphism na sheria za uandishi wake
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza aina mbalimbali za function ambazo tunaweza kuzitumia kwenye python.
Soma Zaidi...