picha

Python somo la 61: Jinsi ya kutuma email kwenye django

Katika maeneo ya development, tunahitaji kutuma email mara nyingi kwa madhumuni ya: Kujaribu mfumo wa OTP Password reset System notifications Activation codes Lakini mara nyingi hatutaki emails ziondoke kwenda kwa watu halisi wakati bado tupo kwenye majaribio.

Utangulizi

Django hutupatia njia mbili:

  1. Console/Backend email (bila SMTP) – kwa majaribio

  2. SMTP (Mailtrap) – kwa majaribio salama bila kutuma email kwa watu halisi

Tutaeleza zote kwa kina na hatua kwa hatua.


 


SEHEMU YA 1 — Kutuma Email Django Bila SMTP (Console Backend)

Hii ni njia ya majaribio. Email haitatumwa nje; badala yake itachapishwa kama text kwenye terminal.

1. Kwanini Console Backend?


Hatua kwa hatua:

STEP 1 — Fungua settings.py

Ongeza:

EMAIL_BACKEND = "django.core.mail.backends.console.EmailBackend"

Kazi ya Email Backend:

Hakuna configuration nyingine inayohitajika.


STEP 2 — Kutuma Email (mfano wa Django view)

from django.core.mail import send_mail
from django.http import HttpResponse

def test_console_email(request):
    send_mail(
        subject="Test Email - Bongoclass",
        message="Hii ni email ya majaribio kutoka Django bila kutumia SMTP.",
        from_email="mafunzo@bongoclass.com",
        recipient_list=["test@bongoclass.com"],
    )
    return HttpResponse("Email imechapishwa kwenye terminal!")

Matokeo yatakuwaje?

Ukifungua browser kwenye URL ya view hii, terminal itaonyesha:

Subject: Test Email - Bongoclass
From: mafunzo@bongoclass.com
To: test@bongoclass.com

Hii ni email ya majaribio kutoka Django bila kutumia SMTP.

Hakuna email inayotumwa, ni kwa testing tu.


 

SEHEMU YA 2 — Kutuma Email Django Kutumia SMTP (Mailtrap)

Ili kupata configuration za smtp tutatumia platform ya mail trap ili kupata free configuration. Hata hivyo unaweza kutumia za mail ama platform nyingine yeyote ile. Mailtrap ni platform tutakayoitumia kupata configuration za SMTP kwa kutuma email za majaribio bila kuzifikisha kwa watu halisi. Ina Inbox bandia (virtual) inayopokea kila email.

 

smtp ni nini?

SMTP ni kifupi cha Simple Mail Transfer Protocol.

Ni mfumo wa kutuma barua pepe (emails) kwenye mtandao.
Kwa kifupi, ni “lugha” au sheria ambazo server hutumia kutuma email kutoka kompyuta moja kwenda nyingine.

 

Kabla ya kuendelea na somo, kwanza tunahitaji kupata configuration za smtp hivyo kwanza nenda kwenye tovuti ya mailtrap.io jisajili hapo kisha nenda kwenye sandboxes, kisha tengeneza boxes utaona configuration za smtp utachaguwa language python kisha chaguwa django. utakopi hizo configuration.


Faida za Kutumia Mailtrap


Hatua kwa hatua:


STEP 1 — Pata SMTP Setting za Mailtrap

Nenda:
Mailtrap → Email Testing → Inbox → Integrations → Django

Utapata mfano:

Host: sandbox.smtp.mailtrap.io  
Port: 2525  
Username: xxxx  
Password: yyyy  

STEP 2 — Andika configuration kwenye settings.py

EMAIL_BACKEND = "django.core.mail.backends.smtp.EmailBackend"

EMAIL_HOST = "sandbox.smtp.mailtrap.io"       # Server ya Mailtrap
EMAIL_HOST_USER = "USERNAME_YAKO"             # Toka Mailtrap
EMAIL_HOST_PASSWORD = "PASSWORD_YAKO"         # Toka Mailtrap
EMAIL_PORT = 2525                             # Port salama ya SMTP
EMAIL_USE_TLS = True                          # Kuweka connection salama
EMAIL_FROM = "mafunzo@bongoclass.com"         # From email yako

Kazi ya kila kipengele:

Kipengele Kazi
EMAIL_BACKEND Django atumie SMTP badala ya console
EMAIL_HOST Server ambayo Django itatuma email
EMAIL_HOST_USER Username ya authentication Mailtrap
EMAIL_HOST_PASSWORD Password ya SMTP Mailtrap
EMAIL_PORT Njia ya kuwasiliana na server
EMAIL_USE_TLS Kuhakikisha usalama wa data
EMAIL_FROM Email itakayoonekana kama mtumaji

STEP 3 — Django View ya Kutuma Email

from django.core.mail import send_mail
from django.conf import settings
from django.http import HttpResponse

def test_mailtrap_email(request):
    send_mail(
        subject="Bongoclass - Mailtrap Test",
        message="Hii ni barua pepe ya mafunzo kutoka Django kwenda Mailtrap.",
        from_email=settings.EMAIL_FROM,
        recipient_list=["test@bongoclass.com"],
        fail_silently=False,
    )
    return HttpResponse("Email imeenda Mailtrap!")

STEP 4 — Angalia Mailtrap Inbox


Je wajua…


Hitimisho

Katika somo linalofuata tutakwenda kujifunza jinsi ya ku upload picha kwenye django. Pia tutajifunza ku display picha.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2025-12-05 09:03:49 Topic: Python Main: Masomo File: Download PDF Views 893

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 web hosting     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Python somo la 54: Jinsi ya Kusoma Data Kutoka Database kwenye Django

Katika somo hili tutajifunza namna ya kusoma data kutoka kwenye database kupitia Django ORM, jinsi ya kuzipeleka kwenye view, na jinsi ya kuzionyesha kwenye HTML template.

Soma Zaidi...
Python somo la 29: Encaosulation kwneye python

Katika somo hili utajifunza maana ya encapsulation na sheria za uandishi wake

Soma Zaidi...
Python somo la 23: Library kwenye python

Hapa utajifunza maana ya library, kazi zake aina zake na jinsi ya ku install lirary

Soma Zaidi...
Python somo la 20: Aina za parameter kwenye function

Katika somo hili tutakwend akujifunza kwa urefu zaidi kuhusu parameter ambazo hutumika kwenye functions

Soma Zaidi...
Python somo la 44: Data Manipulation katika Django Templates

Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kucheza na data kuzibadili kwa namna mbali mbali kwenye template

Soma Zaidi...