Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutumia Django ORM kufanya mahesabu mbalimbali kama Sum, Avg, Count, Max, Min, pamoja na kupunguza idadi ya items zinazoonekana kwenye dashboard (LIMIT). Pia tutajifunza namna ya kutengeneza “difference” kati ya thamani kubwa na ndogo bila kubadilisha functions zozote ulizokwisha ziandika.
Katika kazi za mifumo, mara nyingi tunahitaji kuonyesha takwimu kama jumla ya bei, wastani, au idadi ya vitu. Django inatoa njia rahisi kupitia ORM bila kuandika SQL moja kwa moja. Somo hili litakuonyesha hatua kwa hatua jinsi ya kupata mahesabu hayo kutoka kwenye jedwali la MenuItem.
Django inatoa method maalumu kwa ajili ya mahesabu:
Sum() — kupata jumla ya data fulani
Avg() — kupata wastani
Count() — kuhesabu idadi
Max() — kupata thamani kubwa
Min() — kupata thamani ndogo
Tunaziingiza kwa:
from django.db.models import Avg, Sum, Count, Max, Min
Mfano tukitumia model yako:
MenuItem.objects.aggregate(Sum('bei'))
Lakini matokeo huja kama dictionary:
{'bei__sum': 45000}
Kwa hiyo tunachukua thamani moja kwa moja:
jumla = MenuItem.objects.aggregate(Sum('bei'))['bei__sum']
Vivyo hivyo kwa mahesabu mengine:
wastani = MenuItem.objects.aggregate(Avg('bei'))['bei__avg']
idadi = MenuItem.objects.aggregate(Count('id'))['id__count']
bei_kubwa = MenuItem.objects.aggregate(Max('bei'))['bei__max']
bei_ndogo = MenuItem.objects.aggregate(Min('bei'))['bei__min']
Kwa kuwa baadhi ya data inaweza kuwa tupu (None), tunalinda kwa kutumia or 0:
tofauti = (bei_kubwa or 0) - (bei_ndogo or 0)
Kama tunataka kuonyesha item 10 tu, tunatumia slicing:
items = MenuItem.objects.all()[:10]
Hii haiathiri data wala pagination, ni limit ya kuonyesha tu.
Hii ndiyo view ambayo unaweza kuitumia bila kubomoa code zako zilizopo:
...Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili tutajifunza namna ya kusoma data kutoka kwenye database kupitia Django ORM, jinsi ya kuzipeleka kwenye view, na jinsi ya kuzionyesha kwenye HTML template.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku host website ya Django. Hapa tutakwenda kutuma plaform ya pythonanywhere.com.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza maana ya polymorphism na sheria za uandishi wake
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza vipi django inaweza kuwasiliana na database, utajifunza kuusu orm na model
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz ajinsi ya kutumia html kwneye python
Soma Zaidi...Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kuunda dashboard rahisi ndani ya Django ambayo itaruhusu mtumiaji kuongeza, kusoma, kuhariri na kufuta taarifa za MenuItem bila kutumia Django built-in admin, bali kwa kutumia HTML templates na views tulizotengeneza sisi wenyewe.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutajifunza jinsi Django hutumia migrations kuunda na kubadilisha tables kwenye database kulingana na models tunazoandika. Tutapitia maana ya migration, hatua za kuitumia, umuhimu wake, misingi ya makemigrations na migrate, pamoja na mfano halisi kutoka kwenye project yetu ya pybongo (app: menu).
Soma Zaidi...Katika somo hili uatkwenda kujifunz anamna ambavyo mtu anaweza kuingiza input kwneye system
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kupokea na kuchakata fomu
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujfunza operator nyingine kama assignment operator logical, identity operator na membership operator.
Soma Zaidi...