Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku host website ya Django. Hapa tutakwenda kutuma plaform ya pythonanywhere.com.
Jinsi ya Kuweka (Deploy) Django Project Kwenye PythonAnywhere – Hatua za Lazima Tu
Somo hili linaeleza hatua za lazima za kuchapisha Django project mtandaoni kwa kutumia PythonAnywhere. Tutatumia Bash Console, Virtual Environment, na GitHub (au upload ya project). Video nzima ya somo hili utaipata hapa https://bongoclass.com/learn/play/b8c833192312b34f08ab8327458f539054d97ac6
requirements.txt
Ikiwa tayari una Django project kwenye kompyuta yako, fungua terminal (cmd/bash), ingia kwenye folder la project, na andika:
pip freeze > requirements.txt
➡️ Hii itaweka list ya packages zote ulizotumia (kama Django, Pillow, etc) kwenye faili la requirements.txt
ili ziweze kusanikwa baadaye kwenye server ya PythonAnywhere.
Una chaguzi 2 hapa:
Fungua PythonAnywhere, login, nenda kwenye Files tab, bonyeza Upload, na weka project yako (zip au folder moja moja).
AU
Fungua Consoles > Bash, kisha clone repo yako:
git clone https://github.com/jinalako/projectyako.git
Mfano:
git clone https://github.com/skyclassbongo/pybongo.git
➡️ Hii itaweka project kwenye folder lenye jina la project.
python3.10 -m venv venv
➡️ Hii inaweka mazingira ya kujitegemea ya Python kwa ajili ya project yako (venv
).
source venv/bin/activate
➡️ Baada ya hapa, unaweza kusanikisha Django na mahitaji yako mengine.
requirements.txt
pip install -r yourproject/requirements.txt
Mfano:
pip install -r pybongo/requirements.txt
wsgi.py
na settings.py
Angalia kama wsgi.py
(ndani ya folder la project) lina">...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili tunakwenda kujifunza aina nyingine za data ambazo hutumika kwenye python.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza maana ya polymorphism na sheria za uandishi wake
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz ajinsi ya kusoma mafaili na mitindo mbalimbali ya kusoma data
Soma Zaidi...Katika somo ili utajifunza hatuwa kwa hatuwa za ku install Django, kutengeneza project na kutengeneza app
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza maana ya encapsulation na sheria za uandishi wake
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu string indexing. Kama tulivyojifunza kuhusu namba katika somo lililopita, basi hapa tutakwenda kucheza na string.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza aina mbalimbali za function ambazo tunaweza kuzitumia kwenye python.
Soma Zaidi...Hapa tunakwenda kujifunza kuhusu OOP ambapo ni miongoni mwa mitindo ya uandishi wa code
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza zaidi kuhusu Jinsi ya Kuongeza Kurasa Nyingine Katika Django View
Soma Zaidi...