Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu string indexing. Kama tulivyojifunza kuhusu namba katika somo lililopita, basi hapa tutakwenda kucheza na string.
Indexing:
Unapopewa string yeyote, katika python unaweza ku access yaani kufanyia kazi sehemu tu ya string hiyo na kuacha sehemu nyingine. Huko nyuma tulijifunza kuhusu habari hii ya indexing na nikakueleza kuwa string index inaanzia na 0. Sasa katika somo hili tutainga ndani zaidi katika kuijuwa indexing.
Katika somo letu hili tutakwenda kuifanyia kazi string hii βJifunze python na Bongoclassβ
Mfano 1:
Katika mfano huu tutaona jinsi ya kufanya index kwa character ya mwanzo tu. yaani tunataka ku dislay haerufi ya mwanzo tu ambayo ni j. Kama nilivyokueleza kuwa indexing inaanzia na 0. Kwa hiyo character ya mwanzo itakuwa na index ya 0.
string = 'Jifunze python na Bongoclass'
print(string[0])
Hii itatupa jibu j
Mfano 2:
Kwa kupitia mfano huo unaweza ku display character yeyote unayotaka kwenye string yetu. Sasa kwa mfano tunataka ku display character ya 12 kwenye string.
string = 'Jifunze python na Bongoclass'
print(string[12])
Hii itakupa jibu o
Mfano 3:
Saa kwa mfano tunataka kudisplay character ya mwisho to, hapa unaweza kuhesabu ilikujuwa ipo index ya ngapi kisha utatumia mfano uliotangulia. Njia nyingine ni kutumia negative number yaani namba hasi.
Index inapokuwa na namba hasi maana yake imeanza kuhesabiwa kutoka mwisho. Sasa ukihesabu kutoka mwisho index haianzi na -0 ila inaanza na -1 kwa kuwa -0 itakuwa ni ile character ya kwanza kwenye index. Hivyo basi kupata character ya mwisho tutaandika hivi
string = 'Jifunze python na Bongoclass'
print(string[-1])
Hii itatupa jibu s
Mfano 4:
Kwa mfano kama huo ukitaka ku display character ya 4 kutoka mwisho tutatumai -4
string = 'Jifunze python na Bongoclass'
print(string[-4])
Hii itakupa jibu l
Mfano 5:
Pia unaweza ku display character zilizobaki kuanzia index ulioitaka. Mfano ninataka ku display kutoka character ya 8 hadi mwisho. Kufanya hivi utaandika index ya 8 ikifuatiwa na nukta pacha.
string = 'Jifunze python na Bongoclass'
print(string[8:])
H">...
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza maana ya library, kazi zake aina zake na jinsi ya ku install lirary
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu number method yaani function zinazofanya kazi kwenye namba.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza syntaxy za python yaani sheria na kanuni za kuandika code za python
Soma Zaidi...Katika somo hili uatkwenda kujifunz anamna ambavyo mtu anaweza kuingiza input kwneye system
Soma Zaidi...Hapa tunakwenda kujifunza kuhusu OOP ambapo ni miongoni mwa mitindo ya uandishi wa code
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz amaana ya inheritance na sheria za kuiandika inheritance.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz amaana ya module, kazi zake, aina zake na jinsi ya kuandika modile
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz ajinsi ya kusoma mafaili na mitindo mbalimbali ya kusoma data
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu operator. Hasa hapa tutakwend akujifunz akuhusu comparison operaor.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza maana ya object, na sheria za kuandika object.
Soma Zaidi...