Python somo la 31: Jinsi ya kutengeneza faili na folder
Katika somo hili utajifunz ajinsi ya kutengeneza folda, faili na kuweka data kwneye faili
Jinsi ya Kutengeneza Folda, Faili, na Kuingiza Data kwa Python
Katika somo hili, utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza folda (directory), faili, kuingiza data kwenye faili, na hata kufuta faili kwa kutumia Python.
1. Kutengeneza Folda
Katika Python, tunaweza kutumia moduli ya os kutengeneza folda. Ili kutengeneza directory, tunatumia method ya os.makedirs().
Mfano wa Kutengeneza Folda:
import os
# Kutengeneza folda mpya
os.makedirs('data', exist_ok=True)
print("Folda 'data' imetengenezwa.")
Ufafanuzi:
-
os.makedirs('data'): Inatengeneza folda inayoitwa data. -
exist_ok=True: Inazuia error kama folda tayari ipo.
2. Kutengeneza Faili na Kuingiza Data
Baada ya kutengeneza folda, tunaweza kutengeneza faili na kuingiza data kwa kutumia mode ya write (w). Kwanza tutafunguwa hilo faili kwa kutumia open() baada ya kulifunguwa ndipo tutaandika data kwa kutumia write()
Mfano:
# Kutengeneza faili na kuandika data
with open('data/tile.txt', 'w') as file:
file.write("Karibu Bongoclass\n")
file.write("Upate kujifunza mengi\n")
file.write("Bila malipo\n")
print("Faili limeundwa na data zimeingizwa.")
Ufafanuzi:
-
open('data/tile.txt', 'w'):Inafungua faili kwa mode ya kuandika. Faili jipya litatengenezwa kama halipo. -
file.write(): Inaandika data kwenye faili.
Writing mode
Unaweza kujiuliza hiyo ( w) kwenye open() na write() ni nini hasa. Hapo imetumika kama writing mode, inaonyesha kwa namna gani hiyo function ifanye kazi. Kazi ya mode ya w ni kufunguwa faili a kuandika. Hata hivyo haipo peke yake zipo mode nyingine kama a, a+, b, w, w+, r, r+ angalia kazi za kila mode kwenye jedwali hapo chini
3. Kuingiza Data kutoka kwa Mtumiaji
Tunaweza kutumia input() kwa kuingiza data kutoka kwa mtumiaji na kuiandika kwenye faili.
Mfano:
# Kufungua faili kwa mod...
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Python somo 57: Matumizi ya Python shell
Katika somo hili, tutajifunza: Maana ya Python shell na umuhimu wake. Tofauti kati ya shell na terminal ya kawaida. Matumizi ya shell, hususan kwenye Django. Amri muhimu zaidi za Python shell, zilizotokana na models na views zako za pybongo.
Soma Zaidi...Python somo la 43: Kutuma Data kutoka View kwenda Template katika Django
Katika somo hili uatajifunza jinsi gani unaweza kutumia view kma logic kuuma data kwenye template
Soma Zaidi...Python somo la 15: Jinsi ya kutumia while loop
Katika somo hili tutakwend akujifunza jinsi ya kutumia while loop kwneye python
Soma Zaidi...Python somo la 32: Jinsi ya kusoma mafaili
Katika somo hili utakwenda kujifunz ajinsi ya kusoma mafaili na mitindo mbalimbali ya kusoma data
Soma Zaidi...Python somo la 29: Encaosulation kwneye python
Katika somo hili utajifunza maana ya encapsulation na sheria za uandishi wake
Soma Zaidi...Python somo la 35: Jinsi ya kutumia MYSQL kwenye python
Katika somo hili utajifunz akutumia database kwenye python
Soma Zaidi...