Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kuandika function, kuweka parameter na kuitumia function
Katika somo hili, tutajifunza maana ya function, jinsi ya kuandika function, na jinsi ya kuweka parameters kwenye function katika Python.
Function ni block ya code inayofanya kazi maalumu. Inasaidia kupunguza marudio ya code kwa kuruhusu matumizi yake mara nyingi bila kuiandika tena.
Mambo ya Kuzingatia kuhusu Functions:
Function hutumika zaidi ya mara moja.
Function haifanyi kazi mpaka iitwe (invoked).
Function inaweza kupokea parameters ili kubadilisha tabia yake kulingana na mahitaji.
Katika Python, function huandikwa kwa kutumia def ikifuatiwa na jina la function, mabano ya mviringo (), yakifuatiwa na alama ya ( : ) yaani nukta pacha bouble colon kisha ndipo body ya function inafuata.
Mfano wa Msingi:
# Function rahisi inayochapisha ujumbe
def bongo():
print("Bongoclass")
# Kuitwa kwa function
bongo()
Function inaweza kuitwa mara nyingi kwa kutumia for loop.
Mfano:
# Function inayochapisha "Bongoclass"
def bongo():
print("Bongoclass")
# Kuitumia mara 10
for i in range(10):
bongo()
Parameters ni viingilio vinavyotumwa kwa function wakati wa kuitwa, na vinaweza kubadilisha tabia ya function.
Mfano:
# Function inayochapisha ujumbe mara kadhaa
def bongo(idadi):
for i in range(idadi):
print("Bongoclass")
# Kuitumia function
idadi = int(input("Andika idadi ya mara za kuchapisha: "))
bongo(idadi)
Parameter na argument
Katika mfano hapo juu parameter ni idadi na argument ni hiyo namba utakayoweka. ina maana argument ni value ya hiyo parameter. mfano hapo nikiweka 6, ina maana parameter na idadi na argument ni 6. Nimeliweka wazi hili kwa sababu programmer wengi wanaoanza kujifunza wanapata tabu sana kutofautisha kati ya argument na parameter.
Unaweza kutumia parameters zaidi ya moja kwa kuzitenganisha kwa koma.
Mfano: Kujumlisha Namba Mbili:
# Function inayojumlisha namba mbili
def jumlisha(x, y):
print(f"Jumla ya {x} na {y} ni: {x + y}")
# Kuitumia function
jumlisha(5, 7)
Hii ni programu inayotumia parameters tatu: namba ya kwanza, operator ya hesabu, na namba ya pili.
Kwa kutumia if statement:
# Function ya calculator
def calculator(x, y, z):
if y == "+":
return x + z
elif y == "-":
return x - z
elif y == "*":
return x * z
elif y == "/":
return x / z
else:
return "Invalid operator"
# Kuitumia function
x = int(input("Namba ya kwanza: "))
y = input("Weka operator ya hesabu (+, -, *, /): ")
z = int(input("Namba ya pili: "))
print(f"Matokeo: {calculator(x, y, z)}")
Kwa kutumia match statement (Python 3.10+):
# Function ya calculator
def calculator(x, y, z):
match y:
case "+":
return x + z
case "-":
return x - z
case "*":
return x * z
case "/":
return x / z
case _:
return "Invalid operator"
# Kuitumia function
x = int(input("Namba ya kwanza: "))
y = input("Weka operator ya hesabu (+, -, *, /): ")
z = int(input("Namba ya pili: "))
print(f"Matokeo: {calculator(x, y, z)}")
Function inaweza kurudisha thamani badala ya kuchapisha moja kwa moja.
Mfano:
# Function inayojumlisha namba mbili
def jumlisha(x, y):
return x + y
# Kuitumia function
result = jumlisha(5, 7)
print(f"Jumla: {result}")
Hii ni calculator inayorudisha thamani badala ya kuichapisha.
def calculator(x, y, z):
if y == "+":
return x + z
elif y == "-":
return x - z
elif y == "*":
return x * z
elif y == "/":
return x / z
else:
return "Invalid operator"
x = int(input("Namba ya kwanza: "))
y = input("Weka operator ya hesabu (+, -, *, /): ")
z = int(input("Namba ya pili: "))
result = calculator(x, y, z)
print(f"Matokeo: {result}")
Katika somo hili, tumejifunza:
Maana ya function.
Jinsi ya kuandika function.
Jinsi ya kutumia parameters na kurudisha thamani.
Somo linalofuata litaelezea aina za functions na mbinu za juu za kuzitumia kwa ufanisi zaidi.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-11-26 15:17:32 Topic: Python Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 21
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 Kitau cha Fiqh
👉6 Simulizi za Hadithi Audio
PYTHON - somo la 9: indexing katika strinfg
Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu string indexing. Kama tulivyojifunza kuhusu namba katika somo lililopita, basi hapa tutakwenda kucheza na string. Soma Zaidi...
Python somo la 24: Nini maana ya Object Oriented Programming
Hapa tunakwenda kujifunza kuhusu OOP ambapo ni miongoni mwa mitindo ya uandishi wa code Soma Zaidi...
Python somo la 30: Data abstraction
Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu nadharia ya data abstraction na kazi zake kwenye OOP Soma Zaidi...
PYTHON - somo la 4: Aina za data kwenye python
Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data ambazo hutumika kwenye python. hapa utajifunza aina kuu 3 za data. Soma Zaidi...
Python somo la 25: Sheria za uandishi wa class
Katika somo hili utajifunza maana ya class, sheria za uandishi wake na mifano halisi Soma Zaidi...
PYHON - somo la 5: Aina za data list, turple, dictionary na boolean
Katika somo hili tunakwenda kujifunza aina nyingine za data ambazo hutumika kwenye python. Soma Zaidi...
PYTHON - somo la 1: Jinsi ya ku install python
Katika somo hili utajifunza kuhusu maana ya python na kazi zake. pia jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya somo. Soma Zaidi...
Python somo la 17: Jinsi ya kutumia user input
Katika somo hili uatkwenda kujifunz anamna ambavyo mtu anaweza kuingiza input kwneye system Soma Zaidi...
Python somo la 14: Jinsi ya kutumia For loop
Katika somo hili utakwend akujifunza matumizi ya for loop kwneye python Soma Zaidi...
Python somo la 28: inheritance kwenye OOP
Katika somo hili utakwenda kujifunz amaana ya inheritance na sheria za kuiandika inheritance. Soma Zaidi...
PYTHON - somo la 6: Jinsi ya kujuwa aina ya data iliyotumika
Katika somo hili utajifunza jisni ya kujuwa aina ya data iliyotumika kwenye python Soma Zaidi...
Python somo la 15: Jinsi ya kutumia while loop
Katika somo hili tutakwend akujifunza jinsi ya kutumia while loop kwneye python Soma Zaidi...