picha

Python somo la 19: Aina za Function

Katika somo hili utakwend akujifunza aina mbalimbali za function ambazo tunaweza kuzitumia kwenye python.

Aina za Functions kwenye Python

Katika somo hili, tutachambua kwa kina aina za functions kwenye Python. Functions ni msingi muhimu wa programu, zikisaidia kuandaa msimbo ulioratibiwa vizuri na kurahisisha matumizi tena.

 


 

Aina Kuu za Functions

Functions zinaweza kugawanywa katika makundi mawili makuu:

1. User-defined Functions

Hizi ni functions unazotengeneza mwenyewe kulingana na mahitaji yako. Mfano:

 

def salamu():

    print("Habari ya muda huu!")

    

salamu()

 

2. Built-in Functions

Hizi ni functions zilizojengwa ndani ya Python, kama vile print(), len(), na nyinginezo. Mfano:

print("Hii ni built-in function.")

 

 


 

Aina za Functions kulingana na Parameter na Return Type

1. Functions zisizo na Parameter wala Return

Hizi ni functions rahisi zisizohitaji pembejeo wala kurudisha thamani yoyote.

def salamu_bila_kitu():

    print("Habari! Hakuna parameter wala return.")

salamu_bila_kitu()

 

 


 

2. Functions zenye Parameter bila Return

Hizi hupokea pembejeo kutoka kwa mtumiaji lakini hazirudishi thamani.

def jumlisha(x, y):

    print(f"Jumla ya {x} na {y} ni: {x + y}")

 

jumlisha(4, 9)

 

 


 

3. Functions zisizo na Parameter lakini zenye Return

Hizi hazihitaji pembejeo, lakini hurejesha thamani.

 

def jumla_bila_input():

    x, y = 4, 6

    return x + y

 

print(f"Jumla ni: {jumla_bila_input()}")

 

 


 

4. Functions zenye Parameter na Return

Hizi hupokea pembejeo na pia hurejesha thamani.

 

def eneo(urefu, upana):

    return urefu * upana

 

print(f"Eneo ni: {eneo(6, 8)}")

 

 


 

Anonymous Functions (Lambda)

Anonymous function, pia hujulikana kama lambda, haina jina rasmi na hutumika kwa misimbo rahisi. 

Tunapotumia anonymous functions kwenye Python, tunatumia keyword lambda. Hii ni kwa sababu Python haitoi njia nyingine ya kutengeneza functions zisizo na jina moja kwa moja, tofauti na lugha zingine kama Kotlin.

Hapa kuna maelezo ya haraka kuhusu lambda functions kwenye Python:

 

Sifa za Lambda Functions

  1. Haina jina: Ndiyo maana inaitwa "anonymous function".

  2. Rahisi na mfupi: Huandikwa kwa mstari mmoja.

  3. Hutumia neno kuu (lambda): Neno hili linaonyesha tunatengeneza function isiyo na jina.

  4. Hurejesha thamani moja kwa moja: Hakuna haja ya kutumia neno return — jibu la expression linarejeshwa moja kwa moja.

 

Mfano:

jumlisha = lambda x, y: x + y

print(f"Jumla ni: {jumlisha(4, 6)}")

 

Lambda pia inaweza kutumika bila parameter:

salamu = lambda: print("Salamu sana!")

salamu()

 

 


 

Programu ya Kubadili Mita kuwa Kilomita

Tunatumia function kubadili mita kuwa kilomita kwa kugawanya thamani kwa 1000.

Programu ya kawaida:

 

def badili_mita_kuwa_km(mita):

    return mita / 1000

 

mita = float(input("Andika mita: "))

print(f"Kilomita: {badili_mita_kuwa_km(mita)}")

 

Lambda Function:

 

badili = lambda mita: mita / 1000

 

mita = float(input("Andika mita: "))

print(f"Kilomita: {badili(mita)}")

 

 


 

Scope katika Python

Scope ni wigo ambapo variable au function inaweza kufikiwa.

Variable ndani ya function (Local Scope):

Variable ikitengenezwa ndani ya function itatumika ndani ya hiyo function tu. Hii inaitwa local variable. Kwa mfano hapo chini endapo uta print variable ujumbe nje ya function utapata error.

def salamu():

    ujumbe = "Hujambo"

    print(ujumbe)

 

salamu()

print(ujumbe)  

# Hii itatoa error kwa sababu ujumbe haipo nje ya function.



Variable ya kimataifa (Global Scope):

Hii ni variable ambayo itatumika ndani ya function na nje. Variable hii inatengenezwa nje ya function kabla ya kuandika hiyo function. Kwa mfano hapo chini unawez aku print variable ujumbe popote pale.

 

ujumbe = "Hujambo"

 

def salamu():

    print(ujumbe)

 

salamu()

print(ujumbe)

 

 


 

Recursive Functions

Recursive function hujiita yenyewe, mara nyingi hutumika kutatua matatizo kama factorial.

 

def factorial(n):

    return 1 if n <= 1 else n * factorial(n - 1)

 

print(f"Factorial ya 5 ni: {factorial(5)}")

 

 


 

Main Function

main() ni sehemu kuu ambapo programu huanza utekelezaji wake. Tutakuja kuzungumzia hapa kwa undani tutakapokuwa tunajifunz akuhusu module.

 

def main():

    print("Karibu kwenye Python!")

 

if __name__ == "__main__":

    main()

 

 


 

Hitimisho

Katika somo hili, tumeelewa aina mbalimbali za functions kwenye Python, kutoka kwa zile za kawaida, zenye parameter, zenye return, hadi lambda na recursive. Katika somo linalofuata, tutajifunza matumizi ya kina ya parameters.

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-11-26 16:54:15 Topic: Python Main: Masomo File: Download PDF Views 920

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 ai web app     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zinazofanana:

Python somo la 22: Package kwenye Python

Hapa utakwenda kujifunz amaana ya package, aina zake na jinsi ya kuandika package.

Soma Zaidi...
Python somo la 14: Jinsi ya kutumia For loop

Katika somo hili utakwend akujifunza matumizi ya for loop kwneye python

Soma Zaidi...
Python somo la 52: Kutengeneza table na kufanya Migrations Katika Django

Katika somo hili tutajifunza jinsi Django hutumia migrations kuunda na kubadilisha tables kwenye database kulingana na models tunazoandika. Tutapitia maana ya migration, hatua za kuitumia, umuhimu wake, misingi ya makemigrations na migrate, pamoja na mfano halisi kutoka kwenye project yetu ya pybongo (app: menu).

Soma Zaidi...
PYTHON - somo la 1: Jinsi ya ku install python

Katika somo hili utajifunza kuhusu maana ya python na kazi zake. pia jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya somo.

Soma Zaidi...
PYTHON - somo la 3: Jinsi ya kuandika variable kwenye python

Katika somo hili utajifunza maana ya variable, na sheria za kutengeneza variable kwenye python. Pia utajifunza maneno ambayo hayafai kutumiwa kama variable

Soma Zaidi...
Python somo la 45: Kutumia Loops na Conditions katika Django Templates

Katika somo hili utakwend akujifunza kuchakata data kwa Kutumia Loops na Conditions katika Django Templates

Soma Zaidi...