Katika somo hili tutakwend akujifunza jinsi ya kutumia while loop kwneye python
Katika somo hili, tutajifunza jinsi ya kutumia while loop na do while loop katika Python. Loop hizi hutumika kurudia utekelezaji wa code kulingana na masharti yaliyowekwa. Tofauti yao kuu ni jinsi wanavyoanza utekelezaji.
While loop hutumika pale ambapo hatujui idadi ya marudio, lakini tunataka code iendelee kurudiwa mradi sharti fulani limetimia.
Muundo wa while loop:
while condition:
# Code ya kurudiwa
# Increment/Decrement
print("ORODHA YA NAMBA")
x = 1
print(x)
while x < 12:
x += 1
print(x)
Hapa tutazidisha namba 7 kwa kila namba kuanzia 1 hadi 12.
print("TEBO YA 7")
x = 1
while x <= 12:
print(f"{x} * 7 = {x * 7}")
x += 1
Python haina do while loop kama ilivyo katika lugha kama Kotlin, lakini tunaweza kuunda dhana sawa kwa kutumia while loop pamoja na break. Katika do while loop, code huanza kutekelezwa mara moja hata kama sharti halijatimia, kisha sharti linakaguliwa. Tutajifunz akuhusu break na continue katika somo linalofuata.
While loop
: Sharti hukaguliwa kwanza kabla ya code kutekelezwa.
Do while loop
: Code hutekelezwa angalau mara moja kabla ya sharti kukaguliwa.
Katika somo hili, umejifunza jinsi ya kutumia while loop na jinsi ya kuunda do while loop katika Python. Unaweza kufanyia mazoezi kwa kubuni mifano yako, kama vile kuhesabu namba hata, kuunda jedwali la kuzidisha kwa namba nyingine, au kuonyesha orodha maalum.
Somo linalofuata: Tutaangazia jinsi ya kutumia break na continue kwenye loop ili kudhibiti mtiririko wa utekelezaji. Endelea kufanya mazoezi!
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili tunakwenda kujifunza aina nyingine za data ambazo hutumika kwenye python.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunz akutumia database kwenye python
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz ajinsi ya kusoma mafaili na mitindo mbalimbali ya kusoma data
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwend akujifunza kwa urefu zaidi kuhusu parameter ambazo hutumika kwenye functions
Soma Zaidi...Katika somo hili tunakwenda kujifunza matumizi ya break na continue kwenye loop
Soma Zaidi...Hapa utakwenda kujifunz amaana ya package, aina zake na jinsi ya kuandika package.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu string indexing. Kama tulivyojifunza kuhusu namba katika somo lililopita, basi hapa tutakwenda kucheza na string.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kuandika function, kuweka parameter na kuitumia function
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz anamna ya kuwez akupata taarifa zinazohusu faili
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu maana ya python na kazi zake. pia jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya somo.
Soma Zaidi...