Katika somo hili utakwend akujifunz amaana ya module, kazi zake, aina zake na jinsi ya kuandika modile
Module kwenye Python ni faili la Python linaloweza kuwa na msimbo wa programu (code), vigezo, kazi (functions), au madarasa (classes) ambayo yanaweza kutumika tena katika miradi tofauti ya programu.
Kwa maneno rahisi, module ni njia ya kugawa msimbo (code) wako katika vipande vidogo vilivyoandaliwa vizuri ili kurahisisha utunzaji na utumiaji wa msimbo huo.
Faili yoyote la .py linaweza kuchukuliwa kama module.
Mfano: Faili linaloitwa salamu.py linaweza kuwa module yenye kazi za kutoa salamu.
Kwa maelezo rahisi:, tuseme tuna program ya mahesau, ambayo ina mafaili 3 na kila faili likawa na kazi yake. Mfano tukawa na faili la addition.py, division.py na multiplication.py ikawa tuapotaka kujumlisha tunatumia function zilizopo kwneye addition.py, kugawanya tunatumia divisionn.py na hivyo hayo mafaili yote yanajulikana kama module.
Kuna aina kuu mbili za modules kwenye Python:
Built-in Modules (Zilizo tayari kwenye Python): Hizi ni modules zinazokuja na Python. Mfano:
math: Kwa hesabu za kisayansi.
os: Kwa kushughulikia faili na mfumo wa kompyuta.
random: Kwa kuchagua thamani za bahati nasibu.
datetime: Kwa kushughulikia tarehe na muda.
User-defined Modules (Zilizoandikwa na mtumiaji): Hizi ni modules unazotengeneza mwenyewe kulingana na mahitaji ya mradi wako.
Modules zina faida nyingi, ikiwa ni pamoja na:
Urejelevu wa msimbo (Code Reusability): Module inakuruhusu kutumia tena msimbo uleule kwenye miradi tofauti.
Kupunguza ukubwa wa programu: Kwa kugawa msimbo katika modules ndogo, programu yako inakuwa rahisi kudhibiti.
Kukuza urahisi wa kushirikiana: Developers wanaweza kushirikiana kwa kutumia modules tofauti kwa kazi tofauti.
Kupunguza makosa: Kwa kuweka msimbo katika modules, ni rahisi kufuatilia na kurekebisha makosa.
Ili kutumia module, unahitaji kuiingiza kwenye programu yako kwa kutumia import.
Unapoiingiza module, Python hutafuta faili hiyo katika sehemu tofauti:
Sehemu ya sasa (current directory).
Sehemu zilizoorodheshwa kwenye PYTHONPATH.
Standard Library ya Python.
import math
print(math.sqrt(16)) # Mzizi wa pili wa 16
print(math.pi) # Thamani ya pi
import random
print(random.randint(1, 10)) # Chagua namba ya bahati nasibu kati ya 1 na 10
import datetime
sasa = datetime.datetime.now()
print(f"Tarehe na muda wa sasa: {sasa}")
Wacha tuone Jinsi ya kutengeneza module yako mwneyewe na kuitumia kwenye project. Kwa mfano tunataka kutengeneza module ambayo tutaitumia katika kutoa salamu.
# salamu.py
def asubuhi(jina):
return f"Habari za asubuhi, {jina}!"
def jioni(jina):
return f"Habari za jioni, {jina}!"
Utaanza kwanza ku import modile ya salamu kwa kuandika jina la module. Mfano import salamu
# main.py
import salamu
print(salamu.asubuhi("Amina"))
print(salamu.jioni("John"))
Module ni faili la .py. Kwa mfano, unda faili linaloitwa hesabu.py na uandike kazi kadhaa ndani yake:
# hesabu.py
def jumla(a, b):
return a + b
def tofauti(a, b):
return a - b
def eneo_mraba(urefu, upana):
return urefu * upana
Unda faili lingine main.py na ulete kazi kutoka kwenye hesabu.py:
# main.py
import hesabu
print(hesabu.jumla(5, 3)) # 8
print(hesabu.tofauti(10, 4)) # 6
print(hesabu.eneo_mraba(4, 5)) # 20
Pia unaweza ku import module zaidi ya moja na kufaya kazi kwenye ukurasa mmoja. Kwa mfano tutatumia module zote mbili hapo juu kwneye main.py
# main.py
import salamu
import hesabu
print(salamu.asubuhi("Amina"))
print(salamu.jioni("John"))
print(hesabu.jumla(5, 3)) # 8
print(hesabu.tofauti(10, 4)) # 6
print(hesabu.eneo_mraba(4, 5)) # 20
Unaweza kuchagua kazi maalum kutoka kwenye module badala ya kuleta kila kitu: Yaani mfano hapo kwenye module yetu ya hesabu kuna function 3, sasa badala ya ku import faili zima, tunaweza ku imprt sehemu tu ya hiyo module. Mfano tunataka kutumia function mbili tu ambazo ni jumla na eneo_mraba. Kufanya hivi tutatumia keyword from ikifuatiwa na import ikifuatiwa na hiyo function tunayoitaka. Na sio tu function inaweza kuwa class n.k
from hesabu import jumla, eneo_mraba
print(jumla(7, 2)) # 9
print(eneo_mraba(6, 3)) # 18
Unaweza kutumia as kubadilisha jina la module au kazi:
import hesabu as h
print(h.jumla(10, 5)) # 15
Modules kwenye Python ni zana muhimu kwa urahisi wa kupanga na kutumia tena msimbo. Zinakuja katika aina mbili:
Built-in modules kama math na random.
User-defined modules unazoweza kutengeneza mwenyewe.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-11-27 14:02:42 Topic: Python Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 183
Sponsored links
👉1
Madrasa kiganjani
👉2
kitabu cha Simulizi
👉3
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4
Kitau cha Fiqh
👉5
Simulizi za Hadithi Audio
👉6
Kitabu cha Afya
Python somo la 29: Encaosulation kwneye python
Katika somo hili utajifunza maana ya encapsulation na sheria za uandishi wake Soma Zaidi...
Python somo la 24: Nini maana ya Object Oriented Programming
Hapa tunakwenda kujifunza kuhusu OOP ambapo ni miongoni mwa mitindo ya uandishi wa code Soma Zaidi...
Python somo la 13: Kutumia condition statement - if, else, elif
Katika somo hili tutakwend akuziona aina za condition statement kwneye python na jinsi ya kuzitumia Soma Zaidi...
Python somo la 23: Library kwenye python
Hapa utajifunza maana ya library, kazi zake aina zake na jinsi ya ku install lirary Soma Zaidi...
PYTHON - somo la 2: Sheria za uandishi wa pyhton yaani syntax za python
Katika somo hili utakwenda kujifunza syntaxy za python yaani sheria na kanuni za kuandika code za python Soma Zaidi...
PYTHON - somo la 6: Jinsi ya kujuwa aina ya data iliyotumika
Katika somo hili utajifunza jisni ya kujuwa aina ya data iliyotumika kwenye python Soma Zaidi...
PYTHON - somo la 9: indexing katika strinfg
Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu string indexing. Kama tulivyojifunza kuhusu namba katika somo lililopita, basi hapa tutakwenda kucheza na string. Soma Zaidi...
Python somo la 17: Jinsi ya kutumia user input
Katika somo hili uatkwenda kujifunz anamna ambavyo mtu anaweza kuingiza input kwneye system Soma Zaidi...
Python somo la 26: Sheria za uandishi wa object
Katika somo hili utakwend akujifunza maana ya object, na sheria za kuandika object. Soma Zaidi...
Python somo la 31: Jinsi ya kutengeneza faili na folder
Katika somo hili utajifunz ajinsi ya kutengeneza folda, faili na kuweka data kwneye faili Soma Zaidi...