Katika somo hili uatkwenda kujifunz anamna ambavyo mtu anaweza kuingiza input kwneye system
User input ni taarifa ambazo mtumiaji wa programu huingiza kwenye programu. Python, kama Kotlin, hutoa njia rahisi za kushughulikia user input. Tofauti kubwa ni kwamba Python hutumia input() kwa kazi hii. Hapa kuna jinsi unavyoweza kutekeleza mambo hayo katika Python:
User input ni kila kitu ambacho mtumiaji wa programu anaingiza kama sehemu ya mwingiliano wake na programu. Hii inaweza kuwa jina, namba, au data nyingine yoyote.
Katika Python, tunatumia input() kwa ajili ya kuchukua user input. Maandishi yanayoonekana ndani ya input() hutumika kama ujumbe kwa mtumiaji.
Mfano:
# Kuomba jina kutoka kwa mtumiaji
print("Andika jina lako na kisha bonyeza Enter:")
name = input()
print(f"Jina lako ni {name}")
Python huchukulia input zote kama string. Ikiwa unahitaji aina tofauti ya data, kama vile namba, unapaswa kubadilisha aina ya data kwa kutumia int(), float(), au method nyingine zinazofaa.
Mfano wa Kuhesabu Umri:
# Kuomba mwaka wa kuzaliwa
print("Andika mwaka uliozaliwa:")
year_of_birth = int(input())
current_year = 2023
age = current_year - year_of_birth
print(f"Umri wako ni miaka {age}.")
Changamoto ambayo ipo kwneye code hizo hapo juu endapo mtu atainginza herufi badala ya namba, code zitaleta mrundikano wa error ambazo zitaprint mpaka location ya faili. Sasa hii sio namna nzuri ya kuonyesha error.
Sasa ili kuweza kudhibiti error vizuri. Kwa mfano mtu anaweza kuweka herufi badala ya namba. Ama akaweka namba katika mpangilio sio. Kudhibiti error tutatumia njia ya try na except value error. Katika try tutajaribu kufanya kile tunachokitaka. Na katuka except value error tutaangalia kama tunachokitaka hakikufanikiwa tutaprint messeji ya error kiustaarabu.
# Kuomba mwaka wa kuzaliwa
print("Andika mwaka uliozaliwa:")
try:
year_of_birth = int(input())
current_year = 2023
age = current_year - year_of_birth
print(f"Umri wako ni miaka {age}.")
except ValueError:
print("Tafadhali ingiza mwaka sahihi kwa nambari.")
Endapo kuna error itaonekana kama hivi hapo chini
Katika Python, unaweza kubadilisha string kuwa namba kwa kutumia method kama int() au float(). Kama user input ni tupu au si namba, unaweza kutumia mbinu za kushughulikia makosa.
Mfano wa Kubadilisha Thamani ya Pesa:
# Kubadilisha TSH kuwa USD
print("Andika kiasi cha pesa za Kitanzania:")
try:
tsh_amount = float(input())
usd_amount = tsh_amount / 2500
print(f"Tsh {tsh_amount} ni sawa na USD {usd_amount}.")
except ValueError:
print("Tafadhali ingiza kiasi cha pesa kwa namba.")
Python inaruhusu ukaguzi wa data kwa kutumia if statement. Hii inasaidia kuhakikisha mtumiaji anaingiza data inayotarajiwa. Kwa mfano hapa tutatumia method ya isdigit() ili kuthibitisha kuwa je data zilizoingizwa zipo katika digit yaani namba. Kwa kutumia mfano huu unawez akutumia method nynginezo ambazo tumesha jifunza huko nyuma.
Mfano wa If Statement:
# Kuomba mwaka wa kuzaliwa na kuhakikisha input sahihi
print("Andika mwaka uliozaliwa:")
year_of_birth = input()
if year_of_birth.isdigit():
age = 2023 - int(year_of_birth)
print(f"Umri wako ni miaka {age}.")
else:
print("Tafadhali ingiza mwaka kwa nambari.")
Katika Python, unaweza kutumia or operator ni njia rahisi ya kutoa thamani ya msingi ikiwa user input ni tupu.
Mfano:
# Kutumia default value
print("Andika kiasi cha pesa za Kitanzania:")
tsh_amount = input() or "0"
try:
tsh_amount = float(tsh_amount)
usd_amount = tsh_amount / 2500
print(f"Tsh {tsh_amount} ni sawa na USD {usd_amount:.2f}.")
except ValueError:
print("Tafadhali ingiza kiasi cha pesa kwa namba.")
Utaona kwenye picha hapo chini, sikuweka thamani yeyote lakini sikupata error ni kwa saabu thamani ya default imetumika ambayo ni 0.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhsu Template Tag nini na kazi zake. Pia utajifunza sheria za uandishi wake.
Soma Zaidi...Katika soo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubaduli aina moja ya data kwena aina nyingine. Kwa mfano unaweza kubadili namba kuwa string ama kubadili string kuwa nanda ama kubadili float kuwa int.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kupokea na kuchakata fomu
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kucheza na data kuzibadili kwa namna mbali mbali kwenye template
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kuandika function, kuweka parameter na kuitumia function
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza ktengeneza model kwa ajili ya database table ya menu yetu.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujfunza operator nyingine kama assignment operator logical, identity operator na membership operator.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza maana ya object, na sheria za kuandika object.
Soma Zaidi...Katika somo hili tunakwenda kujifunza matumizi ya break na continue kwenye loop
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza syntaxy za python yaani sheria na kanuni za kuandika code za python
Soma Zaidi...