Python somo la 14: Jinsi ya kutumia For loop
Katika somo hili utakwend akujifunza matumizi ya for loop kwneye python
Jinsi ya kutumia for loop katika Python
Katika somo hili, tutajifunza jinsi ya kutumia for loop katika Python. Loop hutusaidia kurudia utekelezaji wa code mara nyingi kulingana na masharti husika. Python inatoa aina tofauti za loop, na leo tutaangazia for loop na for-in loop.
For Loop
For loop hutumika pale ambapo tunajua idadi ya mara ambayo code inapaswa kurudiwa. Kwa mfano, kama tunataka kutengeneza jedwali la kuzidisha la namba 7, ambapo tutazidisha 7 kwa namba kutoka 1 hadi 12, tunaweza kutumia for loop.
Kwenye kufanya loop kwneye python tutatumia method ya range() kumaanisha kuanzia namba fulani hadi namba fulani. Mfano kwa maelezo niliotoa hapo juu, hii loop itakuwa kati ya 1 hadi 13 ni kwa sababu tebo ya saba itakuwa 1 hadi 12, hivyo hapo ni kati ya moja na 13, ila hiyo 13 yenyewe haipo kwenye loop.
Mfano:
print("TEBO YA 7:")
for x in range(1, 13): # range(1, 13) ina maana kuanzia 1 hadi 12
print(7 * x)
Matokeo ya code hii ni jedwali la 7. Hii ni kwa sababu loop itazidisha 7 na kila namba kuanzia 1 hadi 12.
Kuboreshwa kwa kutumia Interpolation:
Unaweza kuboresha jinsi matokeo yanavyoonekana kwa kutumia f-string, ambayo inaruhusu kuongeza maelezo zaidi.
print("TEBO YA 7 ILIYOBORESHWA:")
for x in range(1, 13):
print(f"{x} * 7 = {x * 7}")
Code hii itatoa matokeo yaliyoeleweka zaidi kama:
1 * 7 = 7
2 * 7 = 14
...
12 * 7 = 84
For-in Loop
For-in loop hutumika wakati tunafanya kazi na data kama vile list au map. Tofauti na for loop ya kawaida, hapa tunarudia moja kwa moja kila kipengele kilichopo kwenye data.
Mfano: Loop kwenye List
Tunaweza kutumia for-in loop kuonyesha jedwali la 7 moja kwa moja kutoka kwenye listi ya thamani zake.
print("TEBO YA 7 KWA KUTUMIA LIST:")
tebo = [7, 14, 21, 28, 35, 42, 49, 56, 63, 70, 77, 84]
for x in tebo:
print(x)
Kufanya Mahesabu Ndani ya List:
Unaweza pia kutumia for-in loop kufanya mahesabu kwa kila kipengele cha list badala ya kuandika thamani zote.
print("TEBO YA 7 KWA MAHESABU NDANI YA LIST:")
tebo = [1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11, 12]
for x in tebo:
print(f"{x} * 7 = {x * 7}")
Hitimisho
Kufikia hapa, umejifunza jinsi ya kutumia for loop na for-in loop katika Python. Unaweza kuendelea kufanya mazoezi zaidi kwa kutumia data tofauti na hali tofauti. Katika somo linalofuata, tutajifunza kuhusu while loop, ambayo hutumika pale ambapo idadi ya marudio haijulikani mapema.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Python somo la 34: Kutumia html kwneye python
Katika somo hili utakwend akujifunz ajinsi ya kutumia html kwneye python
Soma Zaidi...Python somo la 39: Jinsi ya Kuongeza Kurasa Nyingine Katika Django View
Katika somo hili utakwenda kujifunza zaidi kuhusu Jinsi ya Kuongeza Kurasa Nyingine Katika Django View
Soma Zaidi...Python somo la 22: Package kwenye Python
Hapa utakwenda kujifunz amaana ya package, aina zake na jinsi ya kuandika package.
Soma Zaidi...Python somo la 19: Aina za Function
Katika somo hili utakwend akujifunza aina mbalimbali za function ambazo tunaweza kuzitumia kwenye python.
Soma Zaidi...PYTHON - somo la 8: method za namba zinazotumika kwenye python
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu number method yaani function zinazofanya kazi kwenye namba.
Soma Zaidi...