Hapa tunakwenda kujifunza kuhusu OOP ambapo ni miongoni mwa mitindo ya uandishi wa code
Katika somo hili, utajifunza:
Maana ya Object-Oriented Programming (OOP).
Faida za kutumia OOP.
Features za msingi za OOP.
OOP ni kifupisho cha maneno Object-Oriented Programming. Hii ni moja ya mitindo ya programming paradigm inayotumika kuunda programu kwa kuzingatia dhana ya vitu (objects). Mbali na OOP, kuna mitindo mingine ya programming kama:
Imperative Programming: Njia ya kuandika programu kwa maagizo ya hatua kwa hatua.
Declarative Programming: Kuelezea kile kinachotakiwa kufanyika badala ya jinsi ya kukifanya.
Procedural Programming: Kuandika programu kwa kutumia taratibu (procedures).
Functional Programming: Kutoa msisitizo kwa functions zisizo na hali (stateless functions).
Python ni lugha ya programu inayounga mkono OOP, ambapo kila kitu kinaweza kuchukuliwa kama object. Katika OOP, object inaweza kuwa kitu chochote, kwa mfano gari, simu, au mbuzi. Kila object huwa na:
Sifa zake (attributes), kama vile rangi, ukubwa, au uzito.
Tabia zake (behaviors), kama vile kutembea, kuimba, au kufungua.
Rahisi kuelewa na kuzitumia: Code inakuwa rahisi kusoma kwa sababu ya upangaji mzuri.
Kufanya kazi katika timu: Rahisi kushirikiana kwani kila sehemu ya programu inaweza kutengenezwa kama module.
Kupunguza kurudia code: Hutumia reusability kupitia inheritance na methods.
Inarahisisha programu kubwa: Inatoa mfumo wa kugawanya kazi ngumu kuwa ndogo kwa kutumia classes.
Utunzaji wa code (maintenance): Ni rahisi kusahihisha makosa au kuongeza vipengele vipya.
Dhana kuu za OOP ambazo ni msingi wa Python ni:
Class: Kiolezo cha kuunda objects. Hii ni kama ramani.
Object: Ni mfano wa class. Inawakilisha kitu halisi.
Encapsulation: Kuwasilisha data na tabia kama kitu kimoja huku ukilinda data kwa kutumia private attributes.
Inheritance: Uwezo wa class kurithi sifa na tabia za class nyingine.
Polymorphism: Uwezo wa kutumia jina moja la method kwa behavior tofauti.
Abstraction: Kuficha maelezo yasiyo ya lazima na kuonyesha mambo muhimu tu.
Properties: Hizi ni kama variables ndani ya class ambazo huhifadhi sifa za object.
Methods: Hizi ni kama functions ndani ya class zinazowakilisha tabia au vitendo vya object.
Somo linalofuata litahusu jinsi ya kuunda class na object kwa kutumia Python
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwend akujifunza matumizi ya for loop kwneye python
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza maana ya polymorphism na sheria za uandishi wake
Soma Zaidi...Hapa utakwenda kujifunz amaana ya package, aina zake na jinsi ya kuandika package.
Soma Zaidi...Katika somo hili tunakwenda kujifunza matumizi ya break na continue kwenye loop
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu number method yaani function zinazofanya kazi kwenye namba.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz amaana ya inheritance na sheria za kuiandika inheritance.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunz ajinsi ya kutengeneza folda, faili na kuweka data kwneye faili
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwend akujifunza jinsi ya kutumia while loop kwneye python
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu string indexing. Kama tulivyojifunza kuhusu namba katika somo lililopita, basi hapa tutakwenda kucheza na string.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu operator. Hasa hapa tutakwend akujifunz akuhusu comparison operaor.
Soma Zaidi...