Python somo la 13: Kutumia condition statement - if, else, elif
Katika somo hili tutakwend akuziona aina za condition statement kwneye python na jinsi ya kuzitumia
Jinsi ya Kutumia if, if-else, na elif katika Python
Katika somo hili, utajifunza jinsi ya kutumia if, if-else, na elif kwenye Python ili kuruhusu programu kufanya maamuzi kulingana na masharti fulani. Hii inajulikana kama decision-making statements (maamuzi ya programu). Aidha, utajifunza pia kuhusu mzunguko wa loops kwa kutekeleza kazi zinazorudiwa.
Aina za Flow Control Statements katika Python
-
Decision Making (Maamuzi ya Programu):
-
Hapa programu huamua nini cha kufanya kulingana na masharti yaliyopewa.
-
Mfano:
-
if
-
if-else
- match case
-
elif
-
Looping (Mzunguko):
-
Hutumika kurudia kutekeleza msimbo mara kadhaa kulingana na masharti.
-
Mfano:
-
for
-
while
-
Jumping (Kuruka Msimbo):
-
Hutumika kuacha sehemu fulani ya msimbo au kuruka kwenye sehemu nyingine.
-
Mfano:
-
break
-
continue
Maamuzi kwa Kutumia if
Maneno muhimu: ikiwa. Mfano, ikiwa umri wa mtoto ni miaka 7, aseme "aende shule."
Python Code:
umri = 7
if umri == 7:
print("Aende shule.")
Kutumia if-else
Ikiwa umri si miaka 7, aseme "hajafikia umri."
Python Code:
umri = 3
if umri == 7:
print("Aende shule.")
else:
print("Hajafikia umri.")
Kutumia elif kwa Masharti Mengi
Tutaongeza masharti:
-
Umri chini ya 7: "Hajafikia umri."
-
Umri sawa na 7: "Aende shule."
-
Umri zaidi ya 7: "Umri ni mkubwa zaidi."
Python Code:
umri = 10
if umri < 7:
print("Hajafikia umri.")
elif umri == 7:
print("Aende shule.")
else:
print("Umri ni mkubwa zaidi.")
Mfano wa Masharti Mengi Zaidi
Ikiwa umri ni kati ya 7 na 14, aseme "Akanze memkwa," vinginevyo aseme "Umri ni mkubwa zaidi."
Python Code:
umri = 10
if umri < 7:
print("Hajafikia umri.")
elif umri == 7:
print("Aende shule.")
elif 7 < umri <= 14:
print("Akanze memkwa.")
else:
print("Umri ni mkubwa zaidi.")
Matc case
tofauti na kutumia if else, nyingi unaweza kuzikatisha kw akutumia match case. Match case yenyewe itakuwa inaangalia kama hiyo case (hicho unachokifanyia logic au statement) ipo true. Mfano huo hapo juu kwa kutumia match case utakuw ahivi:-
Mfano Rahisi:
umri = 10match umri: case 10: print("anza memkwa") case 7: print('anza darasa la kwanza') case _: print("wasiliana na mwalimu mkuu")
Mfano wa kuchanganya if
umri = 10
match True: # Tunalinganisha na True ili kutumia masharti moja kwa moja case _ if umri < 7: print("Hajafikia umri.") case _ if umri == 7: print("Aende shule.") case _ if 7 < umri <= 14: print("Akanze memkwa.") case _: print("Umri ni mkubwa zaidi.")
Pia mfano kama huo tunaweza kuuandika vingine kwa kutumia temporary variable. Angalia mfano hapo chini
umri = 10
match umri: case x if x < 7: print("Hajafikia umri.") case 7: print("Aende shule.") case x if 7 < x <= 14: print("Akanze memkwa.") case _: print("Umri ni mkubwa zaidi.")
Maelezo ya match-case kwenye mfano huu:
case x if x < 7: Hii inalinganisha ikiwa umri ni chini ya 7.case 7: Hii inalinganisha umri na thamani ya 7 moja kwa moja.case x if 7 < x <= 14: Hii inahakikisha umri uko kati ya 8 na 14 (inclusive).case _: Hii ni sawa naelsekwa hali zote ambazo hazilingani na masharti yaliyotangulia.
Hitimisho
Katika Python, unaweza kutumia if, if-else, na elif kwa maamuzi ya programu kulingana na masharti. Pia, loops hutumika kurudia kazi zinazofanana. Jambo muhimu ni kuelewa jinsi ya kutumia maneno muhimu (if, elif, else, for, na while) pamoja na waendeshaji wa masharti kama >, <, >=, <=, ==, na !=.
Endelea kufanya mazoezi ili kuelewa zaidi!
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Python somo la 53: Kutengeneza HTML Form na Django View kwa ajili ya kuingiza data
Katika somo hili tutaangalia jinsi ya kutengeneza fomu ya HTML kwa ajili ya kuingiza data kwenye jedwali la MenuItem, pamoja na kutengeneza view itakayopokea data hiyo na kuihifadhi kwenye database. Pia tutaunganisha form na URL route.
Soma Zaidi...Python somo la 33: Jinsi ya kupata taarifa za faili
Katika somo hili utakwend akujifunz anamna ya kuwez akupata taarifa zinazohusu faili
Soma Zaidi...Python somo la 38: Kubadilisha landing page ya Django Framework
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubadili ukurasa wa landing page wa Django na kuweka ukurasa tunaoutaka sisi.
Soma Zaidi...Python somo la 22: Package kwenye Python
Hapa utakwenda kujifunz amaana ya package, aina zake na jinsi ya kuandika package.
Soma Zaidi...Python somo la 34: Kutumia html kwneye python
Katika somo hili utakwend akujifunz ajinsi ya kutumia html kwneye python
Soma Zaidi...Python somo la 27: polymorphism kwneye python
Katika somo hili utajifunza maana ya polymorphism na sheria za uandishi wake
Soma Zaidi...