PHP somo la 94: Maana ya ORM na kazi zake

Katika somo hili utakwenda kujifunzo kuhusu teknolojia ya ORM na inavyotumika kulinda usalama wa database

Utangulizi wa ORM katika PHP na MySQL

1. Maana ya ORM

ORM ni kifupi cha Object-Relational Mapping. Ni mbinu inayotumika kuunganisha mfumo wa database ya uhusiano (Relational Database) na programu inayotumia lugha ya Object-Oriented Programming (OOP). Kwa kutumia ORM, badala ya kuandika queries za SQL moja kwa moja, unatumia objects na methods za PHP kushughulikia data kutoka kwenye database.

 

2. Kazi za ORM

ORM ina kazi mbalimbali, zikiwemo:

 

3. ORM Inavyofanya Kazi

ORM inafanya kazi kwa kubadilisha database tables kuwa objects ndani ya PHP. Kwa mfano:

Bila ORM (SQL ya moja kwa moja)

$query = "SELECT * FROM customers WHERE id = 1";
$result = mysqli_query($conn, $query);
$customer = mysqli_fetch_assoc($result);
echo $customer['name'];

 

Kwa ORM

$customer = Customer::find(1);
echo $customer->name;

Hapa, ORM inachukua data kutoka MySQL na kuibadilisha kuwa object ya PHP inayoitwa Customer.

 

4. Usalama wa ORM