Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Maana ya JSON na sheria za kuandika faili la json
JSON (JavaScript Object Notation) ni format ya kuhifadhi na kubadilishana data ambayo ni rahisi kusoma na kuandika na binadamu, na pia rahisi kwa mashine kuzichakata. Data kwenye JSON huandikwa kwenye jozi yaani key na value . key ni jina la hiyo data yaani name na value ni thamani ya hiyo data. Mfano naweza kusema umri : 30 hii ina maana umri ni key na value yae n 30
Json ni lugha kikompyuta ambayo ni format ya kubadilishana data. Json ni rahisi kuandikwa na binadamu na kusomwa. Yani data zilizopo kwneye JSON unaweza ukazisoma na kuelewa kilichiandikwa hata bila ya kuhitaji msaada wa mashine
Mfano:
{
"jina": "John",
"umri": 30,
"ndoa": true,
"watoto": ["Anna", "Ella"],
"anwani": {
"mtaa": "Kigonzi",
"mji": "Mpanda",
"post": "30"
}
}
Katika mfano huu:
- `jina` ni "key" yenye thamani (`value`) ya "John".
- `umri` ni "key" yenye thamani (`value`) ya 30.
- `ndoa` ni "key" yenye thamani (`value`) ya true.
- `watoto` ni "key" yenye thamani (`value`) ya orodha (`array`) inayojumuisha "Anna" na "Ella".
- `anwani` ni "key" yenye thamani (`value`) ya kitu (`object`) chenye jozi kadhaa za "key" na "value".
Ukiangalia hapo hizo data kwa haraka TU unaweza kuelewa hapo hizo data zinamuhusi John,mwenye umri wa miaa 30 na yupo kwneye ndoa, an watoto wawili ambayo ni Ana na Ella. John anaishi Mtaa wa Kigonzi huko mjini Mpanda na anaweza kupatikana kwa address ya 30.
Matumizi ya JSON
Json imekuwa na matumizi makubwa na hata imefikia kuwa mbadala wa xml kwa baadhi ya maeneo. Miongoni mwa matumizi ya json ni kama:-
Kubadilishana data kwenye network
Hutumika ye API
Hutuma uhifadhi data
Pia hutumika kwenye setting za program
Sheria za uandishi wa JSON:
1.Json huandikwa kwenye jozi yaan key na value kama nilivyo onyesha hapo awali. Key inatakiwa iwe ndani ya double quotation mark yaani alama za funga semi. Na endapo value ni string pia itakuwa na alama hizo. Ila ikiwa value ni sio string hatutatumia alam hizo. Baada ya kuandika key itafuatiwa na nykta pacha (:). Endapo value ni zaidi ya moja utatenganisha kwa alama ya koma (,)
Mfano:
"name": "John Doe",
"age": 30,
"isStudent": false
2.Data za json huandikwa ndani ya mabano ambayo ni curly braces {}
Mfano:
{
"jina": "John",
"umri": 30,
"ndoa": true,
"watoto": ["Anna", "Ella"],
"anwani": {
"mtaa": "Kigonzi",
"mji": "Mpanda",
"post": "30"
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza concept ya interface na concept ya polymorphism kwenye PHP OOP.
Soma Zaidi...Katika somo hil utawenda kujifunza jinsi ya ku edit post kwenye databse
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifundisha jinsi ya kutafuta taarifa maalumu kwenye database kwa kutumia PHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika while loop kwenye PHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku update na kufuta data kwenye database kwa kutumia PHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuzungumza na server ili kutengeneza mafaili, mafolda, kufuta na ku edit kwa kutumia PHP.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ambavyo utaweza kutengeneza mfumo wa kuisajiki na ku login, kisha kuangalia usalama wa mfumo kwa kuzuia sql injection.
Soma Zaidi...atika somo hli tutakwenda kujifunza kuhusu kitu kinachitwa cron job. ni moja ya teknolojia zinazotumika kufanya kazi zinazofanyika automatic
Soma Zaidi...Katika somo hili unakwenda kujifunza jinsi y kutengeneza database na kuungansha kwenye blog yetu.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kupangilia data wakati wa kuzisoma kwenye database kw akutumia PHP
Soma Zaidi...