PHP somo la 50: Jinsi ya kutengeneza CLASS na OBJECT kwenye PHP OOP
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza class na object. Tunakwenda kutumia mfano wetu wa hapo juu kwa ajili ya kukamilisha somo hili.
Kutengeneza class utaanza na kuandika neno class likifuatiwa na jina la hiyo class, ikifuatiwa na mabano mawili, ambapo ndani ya mabano hayo ndio utaweka code za hiyo class.
class gari{
}
Mwanzo utaanza kuandika property za hiyo class. Property itaandikea kwa kuanza na access modifier yake. Mfano property ni jina, modifier ni public. Elewa public maana yake hiyo property inaweza kutumia kwenye hiyo class bila ya kizuizi.
class gari{
public $name;
public $speed;
public $transition;
}
Kinachofuata hapo ni kuweka method (functions) kwa ajili ya ku access hizo property
kama method itawekwa ndani ya class tutatumia $this keyword. Kama itakuwa nje hatutatumia. Sasa Wacha tuanze ya ndani ya class.
Tunaposema ndani ya class tunamanisha ndani ya mabano ya hiyo class Yako.
class gari {
//mwanzo wa class
function set_name($name){
$this->name = $name;
}
function set_speed($speed){
$this->speed = $speed;
}
function set_transition($transition){
$this->transition = $transition;
}
//mwisho wa class
}
Sasa tutakwenda kutengeneza function kwa ajili ya kupata value za Kila object. Function yetu ita return value ya object.
function get_name(){
return $this->name;
}
function get_speed(){
return $this->speed;
}
function get_transition (){
return $this->transition ;
}
Mpaka kufikia hapa tayari tumesha set propert za kila class yetu. ila bado hatujatengeneza object . hivyo sasa hatuwa inayofuata ni kutengeneza object
Object tunaweka nje ya class. Ili kutengeneza object tutatumia new keyword likifuatiwa na jina la class.
$toyota = new gari()
$speed = new gari()
$transition = new gari()
Mpaka kufikia hapo tumesha tengeneza object zeta tatu. Sasa kinachofuata ni kutengeneza method kwa ajili ya ku access hizo object ili kuzipa values. Tunaweza kurahisisha kwa kusema kuwa hatuwa inayofuata ni kuweka value kwenye object kutokana na propert zetu. prperty ni name, speed na transition.
$toyota -> set_name("toyota")
$speed ->set_speed("180")
$transition-> set_transition('manual')
Hapo tayari tumeshaipa Kila object value yake. Hatuwa inayofuata ni matumizi ya hizo object. Kwa mfano ngoja tuangalie value hizo
Code zote hizi hapa:
<?php
class gari{
public $name;
public $speed;
public $transition;
function set_name($name){
$this->name = $name;
}
function set_speed($sp...
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 ai web app 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
PHP somo la 80: Authentication header
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Authentication header, najinsi ya kutuma taarifa hizo na kuzisoma
Soma Zaidi...PHP somo la 90: Jinsi ya kutumia json data kama blog post
Katika somo hili utaweza kujifunza ni kwa nambna gani utaweza kutengeneza blog post na kuisoma kwa kutumia data za json
Soma Zaidi...PHP somo la 68: Jinsi ya kutuma email kwa kutumia PHPMailer
Katika somo hili utakwenda kujifunza jisniya kutuma email kwa kutumia PHPMailer kwenye project ya PHP. Katika somo hili tutakwend akutuma email kwa kutumia localhost.
Soma Zaidi...PHP somo la 96: Jinsi ya kutengeneza ORM inayofanya CDRUDE operation
Katika somo hili utakwenda Jinsi ya kutengeneza ORM inayofanya CDRUDE operation.
Soma Zaidi...PHP - somo la 45: Jinsi ya kutuma sms kwa kutumia PHP
Katika soko hili takwenda kujufunza jinsi ya kutuma sms kwa kutumia PHP. Hii itasaidia kama unataka kutuma OTP yaqni Onetime password
Soma Zaidi...PHP somo la 94: Maana ya ORM na kazi zake
Katika somo hili utakwenda kujifunzo kuhusu teknolojia ya ORM na inavyotumika kulinda usalama wa database
Soma Zaidi...