Katika soko hili takwenda kujufunza jinsi ya kutuma sms kwa kutumia PHP. Hii itasaidia kama unataka kutuma OTP yaqni Onetime password
Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutuma sms kwa kutumia PHP. unaweza kutuma na kupokea sms kwa kutumia PHP ila katika somo hili tutajifunza tu jinsi ya kutuma sms. Kitu cha msingi unachotakiwa kukijuwa ni kuwa kutuma sms ni gharama kuliko kutuma email. Kwa kuwa kutuma sms utahitajika kuwa na API pamoja na TOKEN.
Kwa nini tunahitaji kutuma sms
Kwa ajili ya kuwataarifu na kuwakumbusha wateja
Kwa ajili ya kutuma OTP
Kwa ajili ya kutangaza biashara yako
Kufanya huduma ya bulk sms
Kabla ya kuanza somo hakikisha umefanya yafuatayo:-
Umeshapata API na TOKEN hizi unaweza kuzipata kwa kujisajili kwenye pltform zinazofanya huduma hii. Kuna platform nyingi ikiwemo twilio ambayo ni maarufu sana. Katika somo hili tutatumia sinch unaweza kujiunga kupitia sinch.com utaanza na Free account. Baada ya kujisajili utanunua namba ya kutumia. Kisha utapewa token na Api baada ya hapo njoo tuendelee na somo.
Hakikisha unatumia PHP version ya 7.4.3 ama zaidi ya hapo.
Hakukuwa server yako inatumia cURL
Baada ya kukamilisha mahitaji hayo utakuwa tayari kuendelea pamoja nami. Kumbuka utakughatimu kiasi cha pesa kukamilisha setting hizo kama kupata namba, API na token.
Utumaji wa sms kutoka kwenye web
Kuna njia mbili nitakwenda kuzifundisha hapa za kutuma sms kupitia web. Njia ya kwanza ni kwa kutumia html anchor kwenye link ambayobinafunguwa sms app. Njia hii itatumia sms kwa kupitia simu yako mwenyewe. Njia hii haina gharama za ziada, yenyewe inatumia bando lako la kawaida. Wala pia haihitaji kujisajili kwenye platform nyinginezo za kupata API na TOKEN.
Njia ya pili ni kwa kutumia cURL ambapo tutakwenda kutumia sinch platform. Njia hii ndio itahitaji API na TOKEN. Njia hiibjna gharama na inatumia sms moja kwa moja kwenye website na sio kupitia sms app.
Kwa kutumia html anchor tag.
Hapa kwanza tutatengeneza html form ya kuandika ujumbe wetu. Kisha tutaweka ukurasa wa kutumia ambapo mtu atabofya batani ya kutuma. Batani hiyo itakuwa na anchor tag. Anchor tag ni tag hii itakuwa na attribute kama sms ili kuweza kutuma sms pia itakuwa na body ambapo hukaa ujumbe.
sms.html
Hii ni html form ambayo itakuwa na input mbili tu ambazo ni namba ya simu, na body ambapo utaweza kuandika sms. Kwenye ndamba ya simu endapo zitakuwa nyingi utatengenisha kwa alama ya (;)
sms
Phone Number
Message Body
sms.php
Hapa kutakuwa na code za php ambazo zitachukuwa namba ya simu na ujumbe na kuziingiza kwenye anchor attribute. Kisha mtu akibofta neno tuma app ya sms itafunguka ikiwa na ujumbe pamoja na namba za siku. Unachotakiwa ni kutuma kawaida.
$phone_number = $_POST['phone'];
$sms_body = $_POST['body'];
?>
sms
Kwa kutumia cURL
Hapa sasa ndipo tunakwenda kutumia API, NAMBA, pamoja na P">...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu static method na inavtotumika kwenye OOP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data ambazo hutumika kwenye PHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu http header, maana yake na jinsi ya kusoma taarifa zilizopo kwenye http header.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifnza jinsi ya kufanya prepared statement kama njia ya kuzuia sql ingection kwenye PHP blog
Soma Zaidi...Katika somo il utajifunza kutuma email kwa watu wengi kwa kutumia PHPMailer. Pia utajifunza jinsi ya kuweka Carbon Copy na Blind Carbon Copy
Soma Zaidi...Katika somo hili uatakwenda kujifunza jinsi ya kutumia htaccess ili kubadili muonekano wa link ya website ama blog ili kuifanya iwe rafiki zaidi.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuingiza data kwenye dtabase kwa kutumia PHP.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu array kwenye php, na jinsi zinavyoweza kufanya kazi
Soma Zaidi...Katika ukurasa huu utakwenda kujifunz jinsi ya kuandika code za php kwa ajili ya kutuma post yetu kwenye blog.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia PDO kutengeneza database, kuteneneza table na kuingiza data moja na zaidi ya moja.
Soma Zaidi...