PHP - somo la 44: Nini cURL na ni yapi matumizi yake?
Katika somo hilibutajifunza maana ya cURL pamoja na matumini yake
CLIENT URL (cURL)
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu curl. Hii ni php library ambayo tutaigusia kwa ufupi kulingna na matarajio ya course hii. Baada ya kujifunza somo hili itakuwa reahisi kuelewa somo ambalo litafuata baada ya hili.
cURL:
Ni kifupisho cha maneno Client url. Hii ni njia ambayo hutumika kwa ajili ya kusafirisha taarifa kutoka kwenye server ama kuelekea kwenye server. Inafanya kazi kwa kupitia clibrary.
curl inafanya kazi kwenye platform nyingi ikiwepo window, web, linux na zaidi. Kwa mfano kwa kutumia command line kwenye window unaweza ku access taarifa kwenye database kwa kutumia curl. Pia unaweza kutuma na kupokea taarifa hizo.
curl inafanya kazi vyema kupitia API hata hivyo sio lazima. Unaweza kutumia curl kwenye website kwa ajili ya ku load kurasa fulani kwenye kurasa nyingine. Nitakupa mfano hapo chini.
Kwa kutumia curl unaweza kuwasiliana na website mbalimbali na domain. Kwa kutumia curl unaweza kuwasiliana na server na kusafirisha taarifa kwa kutumia url.
Mfano wa curl:
$url = "https://www.bongoclass.com/";
$ch = curl_init();
curl_setopt($ch, CURLOPT_URL, $url);
curl_setopt($ch, CURLOPT_RETURNTRANSFER, 1);
$result = curl_exec($ch);
echo $result;
curl_close($ch);
?>
Ukiangalia vyema hapo utaona kuwa cURL ipo katika namna hii:
-
Kwanza ni mwanzo wa curl ambapo utaweka variable zako. Kwa mfano katika mfano hapo juu variable nilioweka ni ukurasa wa menu wa bongoclass. Hivyo hiyo link itafunguwa ukurasa huo moja kwa moja.
-
Baada ya kuweka variable sasa itawacha cURL ama uta initiate hii tunaita kuanzisha session ama session start. Huu ndio mwanzo wa curl inapoanza kufanya kazi. Bila ya kuiwasha haiwezi kufanya kazi. Sasa ili uweze kuiwasha utaanza na finction hii curl_init(); kama ulivyoona hapo juu. Sasa utaanza na kuiwekea variable yake ili uweze kuitumia huko mbele kama nilivyofanya hapo juu ambapo nimeipa variable $ch, unaweza kuipa jina lolote unalotaka. Hiyo ch ina maana cURL Handler.
-
Hapa sasa ndipo unapoanza nini hasa unataka kufanya. Function ya curl_setopt hutumika kuweka option zinazohitajika katika kuload data kutoka kwenye server. Function hiyo inabeba parameta 3 ambazo ni cURL handler ambayo ni $ch kwa mujibu wa hizo code hapo, parameter nyingine ni option hapa huwekwa taarifa zingine za ziada, kisha parameter nyingine ni option. Option inaweza kuwa 0 au 1. Kama ikiwa 0 hairu...
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 kitabu cha Simulizi 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 ai web app 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
PHP -somo la 6: Jinsi ya kusoma saa na tarehe kwenye PHP
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kusoma muda kama saa na tarehe kwa kutumia PHP
Soma Zaidi...PHP BLOG - somo la 8: Jinsi ya kufuta post kwenye database
katika post hii utajifunza jinsi ya kufuta post kwenye database. pia utajifunza jinsi ya kufuta picha kwenye server
Soma Zaidi...PHP - somo la 11: Jinsi ya kutuma tarifa zilizojazwa kwenye form
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kukusanya taarifa za watumiaji kwa kutumia html form.
Soma Zaidi...PHP somo la 58: static method kwenye PHP
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu static method na inavtotumika kwenye OOP
Soma Zaidi...PHP somo la 88: Jisnsi ya kutengeneza json data kutoka kwenye database
Katika somo ili utakwenda kujifunz ahatuwa kwa hatuwa jinsi ya kutengeneza json data kutkana na data ambazo zio kwenye database
Soma Zaidi...PHP - somo la 10: Jinsi ya kundika condition statement if, ifelse na switch case
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu condition statements if, ifelse na switch case. Hata utajifunza jnsi ya kuziandika na zinavyofanya kazi
Soma Zaidi...