picha

PHP - somo la 43: Jinsi ya kutuma email kwa kutumia PHP

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutuma email kwa kutumia email() function ya PHP. Hii ni njia rahisi zaidi ya kutuma email. Ila hufanya kazi kwenye hosting.

KUTUMA EMAIL:

Katika somo hili tunakqenda kujifunza jinsi ya kutuma email kwa kutumia php. Kuna njia kama tatu za kutuma email kwa kutumia php. Ila katika somo hili .nitakufundisha njia moja ambayo ni kwa kutumai mail().

 

Njia hii ni nyepesi, ila itahitaji uwe umeshahost. Haifanyikazi kwenye localhost. Hivyo hakikisha unahost faili lako live ndipo liweze kufanya kazi.

 

Function hii ina sehemu kuu tano yaani parameta 5 ambazo ni:-

  1. To

  2. From

  3. Header

  4. Message

  5. Subject

 

To hii itabeba email ya mpokeaji wa hiyo email. From hutumika kubeba email ya mtumaji. Header hii hubeba meta information.kama wapi ukumbe umetoka, na wapi utaweza ku reply. Massage hapa ndipo ambapo utaandika meseji yako. Subject hubeba kicha cha habari. 

 

Mfano:

mail($to,$subject,$message, $headers)

  1. Wacha tuone jinsi ya kutuma plain text email:

<?php

$from = "non-reply@bongoclass.com";

$to = "josh@example.com";

$subject = "greetings from Bongoclass";

$message = "haloo karibu bongoclass";

$headers = "From:" . $from;

if(mail($to,$subject,$message, $headers)) {

   echo "Email imetumwa";

} else {

   echo "Email imeshindwa kwenda";

}

?>

 

Hapo kwenye josh@example.com utaweka emaili ya unayemtumia na hapo kwenye non-reply@bongoclass.com  utaweka emaili ya mtumaji. Nimrtumia if() ili kcheki kama ujumbe umetumwa ama laa. Kama umetumwa basi italeta ujumbe kuwa email imetuwa.      

 

  1. Jinsi ya kutuma html

Sasa kama unataka kuboresha muonekano wa meseji yako jinsi itakavyoonekana na ukataka kutumia style, wama kutumia html hapa nitakwenda kukujuza. Html zitatakiw akukaa hapo kwenye ujumbe. Ila changamoto ni kuwa kwa code zetu hapo juu utatuma html file kama text file hivyo haitakuwa na muonekano wa ujumbe bali ni code.

 

Ili kutatuwa tatizo hilo tutatakiwa kuongeza metadata info kwenye header. Tutakwenda kutumia utf-8. $headers = "From:" . $from .

   "Content-type:text/html;charset=UTF-8" . " ";

Kisha tutaweka html code kwenye message. Hivyo faili letu litaonekana hivi:-

<?php

$from = "non-reply@bongoclass.com";

$to = "josh@example.com";

$subject = "greetings from Bongoclass";

$message = "<html>

<head>

   <title>Karibu Bongoclass</title>

</head>

<body>

<h1>tunakutakia siku njema</h1>

<table cellspacing="0" style="border: 2px dashed #FB4314; width: 100%;">

   <tr>

       <th>Web:</th><td>Bongoclass</td>

   </tr>

   <tr style="background-color: #e0e0e0;">

       <th>Email:</th><td>mafunzo@bongoclass.com</td>

   </tr>

   <tr>

       <th>url:</th><td><a href="http://www.bongoclass.com">www.bongoclass.com</a></td>

   </tr>

</table>

</body>

</html>";

$headers = "From:" . $from ." ".

   "Content-type:text/html;charset=UTF-8";

if(mail($to,$subject,$message, $headers)) {

   echo "Email imetumwa";

} else {

   echo "Email imeshindwa kwenda";

}

?>

 

2. Kutuma ujumbe kutoka kwenye html file

Sasa endapo ujumbe wako upo kwenye faili la html, na unataka kutuma faili kama lilivyo ili huko ambape maudhui ya faili hilo. Kufanya hivi tutatumia zile function za mafaili kama tulivyojifunza kwenye masomo yaliotangulia.

 

Sasa tutatengeneza html file kisha tutaliita mail.html

mail.html

<html>

<head>

   <title>Karibu Bongoclass</title>

</head>

<body>

<h1>tunakutakia siku njema</h1>

<table cellspacing="0" style="border: 2px dashed ">...

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2023-10-19 Topic: PHP Main: ICT File: Download PDF Views 865

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

PHP - somo la 22: Kutafuta jumla, wastani na idani ya vitu kwenye database kw akutumia PHP

Katika somo hili utakwenda jifunza jinsi ya kuhesabu row kwenye database, kutafuta wastani wa taarifa kwenye database na kutafuta idadi yake.

Soma Zaidi...
PHP somo la 82: Content-Disposition

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu aina ya header inayoitwa Content-Disposition

Soma Zaidi...
PHP somo la 64: Jinsi ya kutengeneza database na kuingiza data kwa kuumia PDO

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia PDO kutengeneza database, kuteneneza table na kuingiza data moja na zaidi ya moja.

Soma Zaidi...
PHP - somo la 27: aina za variable kwenye PHP

Katika somo hili utakwenda kujifunza aina kuu 3 za variable katika PHP mabzo ni local variable, global variable na static variable.

Soma Zaidi...
PHP - somo la 13: Jinsi ya kuunganisha database na website

Katika somo hili utajifunza jinsi ya ku connect database, kwa kutumia php

Soma Zaidi...
PHP - somo la 48: Jinsi ya kuzuia hacking kwenye sytem ya kujisajili na ku login

Katika somo hili utajifunza jinsi ambavyo utaweza kutengeneza mfumo wa kuisajiki na ku login, kisha kuangalia usalama wa mfumo kwa kuzuia sql injection.

Soma Zaidi...
PHP BLOG - somo la 11: Jinsi ya kutumia prepared statement

Katika somo hili utajifnza jinsi ya kufanya prepared statement kama njia ya kuzuia sql ingection kwenye PHP blog

Soma Zaidi...
PHP somo la 73: Maana ya http header

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu http header, maana yake na jinsi ya kusoma taarifa zilizopo kwenye http header.

Soma Zaidi...
PHP somo la 52: Aina za access modifire na zinavyotofautiana.

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu access modifier ili kuweza kuthibiti nama ya kuzitumia properties kwenye class.

Soma Zaidi...
PHP -somo la 33: Matumizi ya while loop kwenye PHP

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika while loop kwenye PHP

Soma Zaidi...