Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu aina za loop DO, FOR, FOREACH LOOPS kwenye PHP
DO, FOR, FOREACH LOOPS
Kama tulivyojifunza katika somo la 7 hivyo somo hili ni muendelezo ya tulipoishia. Hivyo tutatumia mifano inayolingana.
DO LOOP:
Hii inafanana sana na while loop ila utofauti wake ni kuwa kwenye do kwanza code zitaleta matokeo kisha ndipo zitaanza kutest sharti zilizopewa. Yaani kwanza utapata matokeoa ya code halafu ndipo ianze kutest conditions.
Mfano
Unataka kuorodhesha namba zilizo chini ama sawa na 14. Hapa kama condition yetu ni 17 kwa tulivyojifunza kwenye while hapo huwezi pata matokeo lakini kwenye do kwanza italeta matokeo kwa ku display 17 kisha itastop baada ya kuwa test hazijafikiwa.
Jinsi ya kuandika do loops
Utaweka keyword do likifuatiwa na mabano {} kisha utafanye increment sura decrement ili kupata matokeo kwanza kisha ndipo utatest condition kwa kuweka while(). Code zitaoneka hivi.
Mfano huu ni endapo variable ni ndogo kuliko test yetu.
$x = 1;
do{echo $x++, "
";}
while($x<=14);
?>
Sasa endapo variable ni kubwa kuliko test yetu pia tutapata matokeo kwa kuwa kwanza itadisplay hiyo variable yetu kisha ndipo itaendelea kutest.
$x = 20;
do{echo $x++, "
";}
while($x<=14);
?>
Hapo itadisplay namba 20.
FOR LOOP
For loop hutumika utakuwa unajuwa idadi ya code zako unataka zitest mara ngapi. Kwa mfano tuna list ya array array("muembe", "mnazi", "mpapai") sasa tunataka kupata list hii. Hapa tunajuwa fika kuwa listvyetu ina item tatu hivyo code sita run mara 3. Pia unaweza kupata list ya hizo item ndani ya array kwa kutumia count function.
Kuweka for loop
For loop ipo tofauti kidogo na loop tulizojifunza. Yenyewe ina sehemu kuu tatu ambazo ni: -
Initiative counter haa nibpale ambapo unakwenda kuweka mwanzo wa test yako. Mfano unataka itest kuanzia 0 ama 2.
Test counter hapa ndipo ambapo utaanza ku test condition yao
Increment counter hapa ni pale ambapo unakwenda kufanya increment ama decrement.
Kanuni
fo(initiate counter; test counter; increment counter).
Mfano
Sasa tutumie mfano wetu wa hapo juu wa array yetu yenye item 3. Ili tuweze kupata list ya hizo items.
$x = array("muembe", "mnazi", "mpapai");
$b =count($x);
for($c=0; $c<$b; $c++){
echo $x[$c] ." "."";
">...
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utajifunza kuhusu syntax za PHP
Soma Zaidi...HApa utakwenda kujifunza sasa namna ya kuzisoma post kutoka kwenye blog
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku update na kufuta data kwenye database kwa kutumia PHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function za PHP kama require() na iclude()
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kufanya encryption na decryption kwa kutumia PHP. hii itakusaidia kuongeza usalama kwenye taarifa za watu
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutuma email kwa kutumia email() function ya PHP. Hii ni njia rahisi zaidi ya kutuma email. Ila hufanya kazi kwenye hosting.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu condition statements if, ifelse na switch case. Hata utajifunza jnsi ya kuziandika na zinavyofanya kazi
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kuhifunza kuhusu Custom header na aina zake
Soma Zaidi...Katika somo hilibutajifunza maana ya cURL pamoja na matumini yake
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu http redirect header
Soma Zaidi...