Katika somo hili utajifunza jinsi ya kukusanya taarifa ambazo watu wamezijaza kwa kutumia fomu ya html. Kisha utajifunza jinsi ya kuzisoma hizo taarifa.
Katika somo hili ninakwenda kukufundisha jinsi ya kukusanya madodoso kwa kutumia html form na PHP. Katika somo hili utakwenda kuongeza data kwenye menu yetu kwa kutumia html form. Kufanya hivi tutatengeneza file la php lenye sehemu kuu 2. Moja ni kwa ajili ya kukusanya taarifa, na nyingine ni kwa ajili ya ku process taarifa na kuziweka kwenye database.
Sehemu ya kwanza (HTML FORM)
Kumbuka kuwa tumejifunza kwenye mafunzo ya php level 1 kuwa html form ina sehemu mbalimbali ambazo ni method, action, submit na sehemu ya kuweka data. Method nazo zipo mbili kuna POST na GET. Hizi ni njia ambazo taarifa zako hubebwa kutoka kwenye html form kwenda kwenye code za ku process hizo taarifa na kuziweka kwenye database.
Tafadhali rejea mafunzo ya PHP level 1 somo la 10 hadi 12 utajifunza jinsi html firm ilivyo na jinsi inavyokusanya taarifa. Faili tutakalolitengeneza kwenye somo hili litakuwa na sehemu kuu 2 kama nilivyokwisha kukueleza hapo awali.
Sehemu ya kwanza: html code
Sehemu hii ni kwa ajili ya kukusanya taarifa kwa kutumia html form. Form yetu itakuwa hivi
<form method="post" action="">
<input type="hidden" name="add" value="1">
<label>Name</label><br>
<input placeholder="Name la menu" name="name"><br>
<label>Description</label><br>
<input placeholder="Inahusu Nini" name="description"><br>
<label>Price</label><br>
<inputtype="number" placeholder="Weka Price " name="price"><br>
<input type="submit" value="save">
</form>
Kama html form inavyojionesha hapao, Method (njia) itakafotumika kubeba taarifa ni method="post" na kwakuwa faili letu litajiprocess lenyewe hivyo kwenye action hatuhitaji kuweka chochote kama unavyoona hpo patupu action="" tungeweka link ya faili ambalo lina code za ku process data tutakazo kusanya, ila sisi hatuhitaji faili lengine.
form yetu ina user input 5, yaani taarifa zinazotakiwa kubebwa.
<input type="hidden" name="add" value="1">
Hii ni kwa ajili ya kuwezesha utumwaji wa taarifa. Taarifa zote hapa zitachakatwa kwa kuanzia hapa. Nimeipa jina la add name="add" na haiwezi kuonekana wakati wa kujaza.
<input placeholder="Name la menu" name="name">
Hii ni kwa ajili ya kukusanya taarifa zinazohusu jina la menu unayotaka kuweka. Place holder ni sehemu ambay inabeba jina ambalo mtumiaji ataliona nalitamjulisha kuwa kijumba hicho kinahitaji kujaza nini. Usern input hapa imepewa jina la name name="name
Pia <input type="number" placeholder="Weka Price " name="price"> hapa utaona kuna kitu kimeongezeka a,bacho ni type="number" type maana yake ni aina unaweza kusema kuwa ni aina gani ya data unahitaji ziweze kuwekwa kwenye hiyo sehemu. hapo kwa kuwa ni price himeamuwa iwe namba. Hivyo hutaruhusiwa kuweka herufi hapo.
Mwisho kuna <input type="submit" value="save"> Hii kazi yake ni ku submit, yaani kutuma taarifa, Yaani hiyo ni kama batani, ukiibofya taarifa zinatumwa na kupelekwa kwenye sehemu ambayo kuna code za ku process. Sehemu hii ndio inayotajwa kwenye action.
sehemu ya pili: php codes
<?php
$servername = "localhost";
$username = "root";
$password = "";
$dbname = "hotel";
if(isset($_POST["add"])){
$conn = mysqli_connect($servername, $username, $password, $dbname);
$name = ($_POST['name']);
$description = ($_POST['description']);
$price = ($_POST['price']);
$sql = "INSERT INTO menu (name, description, price) VALUES ('$name', '$description', '$price')";
if (mysqli_query($conn, $sql)) {
echo "Data added";
} else {
echo "Error: " . $sql . "<br>" . mysqli_error($conn);
}
mysqli_close($conn);
}
?>
Hapa kuna vitu unatakiwa uvielewe mapema kabla ya kuenda mbele. NItakuchambulia kila part na kazi zake ili kwamba tuwe pamoja.
if">...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza aina kuu 3 za variable katika PHP mabzo ni local variable, global variable na static variable.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi jinsi ya ku edit ama ku update data na kuzifuta kwenye database kwa kutumia PDO
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuzungumza na server ili kutengeneza mafaili, mafolda, kufuta na ku edit kwa kutumia PHP.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kuona namna ya kutuia if else kwenye data zilizopo kwenye database kwa kutumia PHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kusoma muda kama saa na tarehe kwa kutumia PHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kazi na matumizi ya construct function na desctruct function kwenye OOP
Soma Zaidi...HApa utakwenda kujifunza sasa namna ya kuzisoma post kutoka kwenye blog
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ktumia baadhi ya function za php
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kukusanya taarifa za watumiaji kwa kutumia html form.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Authentication header, najinsi ya kutuma taarifa hizo na kuzisoma
Soma Zaidi...