Katika somo hili utakwenda kujifundisha kuhus matumizi ya function kwenye php. Pia utajifunza jinsi ya kuandika function
PHP FUNCTIONS:
Function ni kikundi cha code ambazo huweza kutumika kwa zaidi ya mara moja. Function zipo katika aina mbi ambazo ni:-
Zile ambazo zimekuja moja kwa moja katika php yenyewe hizi huitwa built in functions
Zile ambazo unaweza kuzitengeneza wewe mwenyewe. Hizi huitwa user defined functions
Sifa za Functions:
Huweza kutumika zaidi ya mara moja
Haiload kila page inapoload
Hutumika pale tu itakapoitwa
USER DEFINED FUNCTIONS:
Sasa hebu tuone jinsi ya kutengeneza function yako mwenyewe. Ili uweze kufanya hivi itahitajika kutumia kanuni ifuatayo:-
function jina() {
//weka code hapa
}
Jinsi ya kuandika function yako:
Kwanza anza na neno keyword function likifuatiwa na jina la hiyo function. Kwa mfano tunataka function ya kujumlisha namba mbili. Hivyo tutaipa jina la jumlisha. Kwahyo itakuwa kama hivi: function jumlisha kisha utaweka mabano haya (). Pia jina la function halitakiwi lianze na namba au special character. Kama ile ya dola tulioitumia kwenye variable.Baada ya hapo utaweka mabano haya {} ambapo ndani yake ndipo kutakuwa na code za hiyo function.
Mfano 1
Function jumlisha(){
Code zinakaa hapa.
}
Hebu sasa tuone mfano halisi wa function ya kujumlisha namba mbili:
Mfano 2:
<?php
function jumlisha() {
$a = 4;
$b = 5;
$c = $a + $b;
echo "$c";
}
?>
Hapo tumeshatengeneza function kwa ajili ya kujumlisha namba mbili. Sasa endappo uta load huo ukurasa hautaonyesha chochote, ni kwa sababu function haionyeshi kitu mpaka iitwe. Ili kuiita hiyo function unatakiwa urudie kuliandika jina lake likifuatiwa na mabano (). Mfano katika code hapo juu utaandakia jumlisha () hapo utakuwa umeiita function na itakupa majibu. Hivyo basi code nzima itakuwa:-
<?php
function jumlisha() {
$a = 4;
$b = 5;
$c = $a + $b;
echo "$c";
}
jumlisha()
?>
Jinsi ya kutatua matatizo kwa kutumia PHP function
Chukulia mfano unaandika program ya kuorodhesha majina ya wanafunzi kwa jinsia zao. Sasa una jinsia mbili ya kike na ya kiume. Sasa baada ya kila inapotaja jina la mwanafunzi uandike na jinsia yake. Kwa kutumia function hatutakuwa na haja ya kutaja jinsia kila wakati.
Mfano: 3
<?php
function mv() {
echo "Mvulana <br>";
}
function ms() {
echo "Msichana <br>";
}
echo "Juma " . "jinsia "; mv() ; echo "<br>";
echo "Aisha " . "jinsia "; ms() ; echo "<br>";
echo "Baraka " . "jinsia "; mv() ; echo "<br>";
echo "Neema" . "jinsia "; ms() ; echo "<br>";
echo "Joharia" . "jinsia "; ms() ; echo "<br>"
?>
...
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kuona namna ya kutuia if else kwenye data zilizopo kwenye database kwa kutumia PHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu syntax za PHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza Jinsi ya utengeneza json data kwa utumia php
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutuma email kwa kutumia php function ya email()
Soma Zaidi...Somo hili litakwenda kukutajia baadhi ya library za php ambazo hutumika kwa matumizi ya ORM
Soma Zaidi...HApa utakwenda kujifunza sasa namna ya kuzisoma post kutoka kwenye blog
Soma Zaidi...Katika soko hili takwenda kujufunza jinsi ya kutuma sms kwa kutumia PHP. Hii itasaidia kama unataka kutuma OTP yaqni Onetime password
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend kujifunza kuhusu static property na jnsi inavyotumika
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kupangilia data wakati wa kuzisoma kwenye database kw akutumia PHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu aina za loop DO, FOR, FOREACH LOOPS kwenye PHP
Soma Zaidi...