PHP - somo la 13: Jinsi ya kuunganisha database na website
Katika somo hili utajifunza jinsi ya ku connect database, kwa kutumia php
Katika somo lililotangulia ulikuwa ni utangulizi wa course. hapa sasa ndipo tunakwenda kuanza somo letu rasmi. katika somo hili utakwenda kujifunza namna ya kuunganisha database kwenye faili la PHP. Hii ni hatuwa ya kwanza na muhimu unatakiwa uijuwe kama unataka kujifunza utengenezaji wa website na blog.
Ni kwa nini tunaunganisha PHP na databae?
Hili ni swali muhimu na ni la msingi sana. Jibu fupi ni kuwa ili uweze kuzisoma data zilizopo kwenye database kwenye blog yako ama website unahitaji uconnect na hiyo databse ili upate ruhusa ya kuziona hizo data,
Yaani ipo hivi, Fikiria kuwa una database inaitwa blog na kwenye hiyo database kuna post kwa ajili ya blog yako. Sasa unataka hizo post zionekane kwenye blog yako. Kwanza utahitajika kuunganisha hiyo blog yako na hiyo database yako. kufanya hivi tutatumia php pamoja na ujuzi wa SQL kama tulivyojifunza katika course ya database. baada ya kuunganisha ndipo utaweza kuziweka hizo post kwenye ukurasa wa wavuti (web page)
Njia zinazotumika kuunganisha PHP na MySQL database
kwa maelezo ya w3school kuna njia kuu mbili za kuunganisha PHP na MySQL database. njia hizo ni:-
- MySQLi
- PDO
Hiyi ya kwanza herufi i ina maana improved, na hiyo ya pili kirefu chake ni PHP Data Object) unaweza kutumia nji yeyote kati ya hizi. ila hii yenye MySQLi yenyewe inafanyakazi kwenye MySQL tu, lakini hiyo ya PDO inafanyakazi kwenye aina nyinginezo za database pamoja na hii ya MySQL.
Mambo muhimu kwenye wakati wa kkonect na database:
- kjuwa jina la database, passowd, na server
- kuanda variable kwa ajili ya kuunganisha na database.
- kufunguwa connection (open connection)
- kukonect kwenyewe (database connection)
- alert message hii ni kwa ajili ya kutoa taarifa kama kuna error ama kama umefanikiwa kukonnect
- kufunga connection
Kukonekt database kwa kutumia MySQLi:
kuna namna mbili ya kuunga database kwa kutumia MySQLi ambazo ni kama tutakavyoziona hapo chini. Unaweza kuchaguwa yeyote kati ya hizo. Utajifunza zaidi kuhusu njia hizi kwenye masomo yetu ya mbele.
- MySQLi object oriented
- MySQLi procedural
hatuwa kwa hatuwa kukonekt database:
- Maandalizi ya variable:
tulisha jifunza namna ya kuandaa variable kwenye course ya PHP somo la 3. katika kukonekt na databse variable zako ni tatu, kwa ajili ya server, kwa ajili ya database (jina la database) na kwa ajili ya password. Variable zako zinaweza kuwa hizi:
$servername = "localhost";
$username = "username";
$password = "password"
localhost ni jina la server ambayo databse yetu ipo. kama unatumia wapserver, ama xamp au aWevServer kwa watumiaji wa simu basi jina la server yako ni localhost. uername ni jina la mtumiaji wa hiyo database. Hii ni akaunt inayomiliki hiyo databse. kama hujabadili jina ama username kwenye database yako basi jina lililopo ni root. na password kama unatumia local host mara nyingi password hakuna unaacha kama ilivyo, hivyo variable hapo zitasomeka hivi
$servername = "localhost";
$username = "root";
$password = ""
- kufunguwa database na kuconnect
Bada ya kuziweka variable zako sasa ni muda wa kuunganisha PHP na database kwa kutumia hizo variable. Kuna variable nyingine sasa tunatakiwa kuijuwa na hii ni muhimu kwa ajili ya kufanya hiki tunachokitaka. variable hii hutumiaka kuunganisha database. variable hii ni
$conn = new mysqli($servername, $username, $password);
variable $conn inakwenda kuwakilisha function new mysqli()ambapo ndani yake utawka variable zako za database name, server name na username. hivyo kusomeka
$conn = new mysqli($servername, $username, $password);
- Kuangalia kama connection imefanikiwa ama imefeli
Hapa kuna jambo unatakiwa ulijuwe, ni kuwa unatakiwa uweke meseji ambayo itakueleza kama connection imefanikiwa ikuambie mfani you are connected. na kama connection imefele inatakiwa iseme mfano connection failed. kwa haraka haraka hapa utajuwa kuwa panatakiwa patumike condition sentenses kama tulivyojifunza kwenye php matumizi ya if, else, ifelse n.k.
kufanya hivi tutatumia
if (mysqli_connect_error()) {
die("connection failed " . mysqli_connect_error());
}
echo "you are connected";
Hapo panajionyesah wazi kuwa mysqli_connect_error() ni kwa ajili ya kuangalia kama connection imefanikiwa ama imefeli. kama imefele itareject (die) hivyo if itatupa matokeo connection failed. Na kama connection imefaniliwa if itatupa matokeo ya else itatupa matokeo ya you are connected.
- Kufunga connection
Katika hali ya kawaida, connection hijifunga automatik. lakini pia unaweza kuifunga wewe mwenyewe punde tu b...
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 ai web app 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
PHP BLOG - somo la 1: Utangulizi na jinsi ya kuandaa kwa ajili ya somo
Katika course hii utakwenda kujifundisha jinsi ya lutengeneza blog kutoka mwanzo hadi mwisho.
Soma Zaidi...Fida za kutumia Framework katika usalama wa webApp
Kwa kuwa ni ngumu kuthibiti usalama wa program, tunahitaji framework kutupunguzia kazi hii
Soma Zaidi...PHP somola 78: Cookie Headers
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Cookie Headers
Soma Zaidi...PHP somo la 70: jinsi ya kutuma email yenye html, picha na attachment
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutuma email ambayo ina HTML, pia utajifunza kutuma email yenye picha na attachment nyinginezo kama pdf
Soma Zaidi...PHP - somo la 44: Nini cURL na ni yapi matumizi yake?
Katika somo hilibutajifunza maana ya cURL pamoja na matumini yake
Soma Zaidi...PHP BLOG - somo la 9: Jinsi ya ku edit poost
Katika somo hil utawenda kujifunza jinsi ya ku edit post kwenye databse
Soma Zaidi...